WAZIRI NCHEMBA ASEMA HAYA KUHUSU MTU ALIYEMTISHIA BASTOLA NAPE
Baada
ya tukio la mtu ana anayedaiwa kuwa ni Askari kanzu kuonekana
akimtishia Bastola Waziri za zamani wa Habari, utamaduni, sanaa na
michezo na Mbunge wa Mtama Nape Nnauye February 23, 2017 wakati
alipotaka kuongea na Waandishi wa habari muda mchache baada ya taarifa
ya Rais Magufuli kufanya mabadiliko ya Wizara aliyokuwa akiiongoza.
Leo March 24, 2017 Waziri wa Mambo ya Ndani, ya nchi Mwigulu Nchemba alitumia ukurasa wake wa Intagram na kusema..>>’Mh.Nape Moses Nnauye sio jambazi, ni mtanzania, ni mbunge, mjumbe wa NEC wa CCM, hana record ya uhalifu‘
‘Kitendo
cha mtu kumtolea Bastola, Sio cha kiaskari, sio cha kitanzania na sio
cha ki Mungu, kama mtu ameweza kutoa Bastola mbele ya Kamera nawaza
mbali ingekuwa kwenye uchochoro angefanya nini‘ –Mwigulu Nchemba
‘Nahusika
na Usalama wa Raia wote wa Tanzania, nimemwelekeza IGP atumie picha
kumsaka mtu yule aliyeinua kufanya kitu cha kihalifu kwa kofia ya
uaskari. Na kama ni Askari basi sheria zinazoongoza taasisi husika
zichukue mkondo wake‘ –Mwigulu Nchemba
FU
Comments
Post a Comment