Posts

BREAKING NEWZZ….Sir. George Kahama afariki dunia!

Image
Mmoja wa waasisi wa Taifa la Tanzania, Sir. George Kahama amefariki dunia jioni ya leo ktk Hospitali ya Taifa, Muhimbili.

JK kuzindua taasisi yake ya maendeleo

Image
RAIS wa Serikali ya Awamu ya Nne, Dk Jakaya Kikwete kesho anatarajiwa kuzindua Taasisi ya Maendeleo ya Jakaya Mrisho Kikwete (JMKF) . Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na taasisi hiyo, uzinduzi huo utafanyika katika Hoteli ya Hyatt Kempinsk The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam na baada ya uzinduzi huo, Dk. Kikwete ataendesha kikao cha kwanza cha bodi ya taasisi hiyo. Taasisi hiyo imeundwa ili kusaidia Tanzania na Afrika katika kuimarisha amani, afya, utawala bora na maendeleo endelevu.Aidha taasisi hiyo itajikita katika maendeleo endelevu kwa kusaidiana na wadau wengine kukabiliana na umasikini, kusaidia mkulima mdogo, kulinda mazingira na kukabiliana na athari za tabianchi. Taasisi hiyo itasaidia pia katika afya ya mama na mtoto, kukabiliana na ugonjwa wa malaria na kuboresha lishe ya wananchi.Katika elimu, itaboresha elimu katika kuwasaidia wajasiriamali kwa mafunzo na pia itasaidia katika utawala bora na utafutaji amani. Taasisi hiyo imesajiliwa na itakuwa ch

MWENYEKITI WA CCM,RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI AONGOZA MKUTANO MKUU MAALUM MJINI DODOMA

Image
Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri wa Tanzania, Dk. Joseph Magufuli akiwahutubia wajumbe wapatao 2356,ambapo walipaswa kuwa wajumbe 2380 katika mkutano huo Mkuu Maalum wa CCM uliokuwa na lengo kuu la kufanya baadhi ya mabadiliko ndani ya Katiba ya chama hicho,ambapo mabadiliko hayo yamepitishwa kwa asilimia 100 na wajumbe hao waliohuhudria mkutano huo. Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza mambo mbalimbali mbele ya wajumbe waliohudhuria katika Mkutano Mkuu Maalum mjini Dodoma. Baadhi ya Wajumbe wa mkutano mkuu Maalum wa CCM wakishangilia kwa shangwe huku wakiwa na mabango yao yakionesha mikoa wanayoiwakilisha.  Sehemu ya baadhi ya wajumbe wa mkutano huo pamoja na wageni waalikwa wakiwa tayari ukumbini.  Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri wa Tanzania, Dk. Joseph Magufuli akisalimiana na aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho na Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete wakati

Ukumbi mpya wa CCM wapewa jina la Kikwete

Image
Dodoma. Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM wamekubaliana kuita ukumbi mpya uliopo eneo la Dodoma Makulu ‘Kikwete Hall’. Makubaliano hayo yametokana na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Rais Dk John Magufuli kupendekeza kwa wajumbe hao ukumbi huo uitwe Kikwete. “Leo tumekaa katika ukumbi huu mzuri kuna watu wamefanya kazi na miongoni mwao atakuwa ni Mzee wetu Jakaya Kikwete (Rais Mstaafu wa awamu ya nne). Mtakumbuka kabla ya hapa tulikuwa tukikaa kule yanatolewa magunia tunakaa,”amesema. Wajumbe hao walikubaliana na wazo hilo na baadaye Rais Magufuli walishikana mkono na Rais Kikwete.

Magufuli: Hatuna Muda wa Kumbembeleza Mtu Kukichangia Chama Chetu

Image
Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk John Magufuli amesema chama hicho hakitambembeleza mtu kukichangia katika shughuli mbalimbali. Akihutubia mkutano Mkuu wa CCM unaofanyika leo Dodoma, Dk Magufuli amewaambia wajumbe wa mkutano huo kuwa kwa miaka yote CCM kimekuwa kikiomba hata kwa watu ambao hawastahili. “Matokeo yake wamekuwa wakitumia nafasi hiyo kudhalilisha. Hakuna tena omba omba hatutaki kumbembeleza mtu akitaka kutuchangia atuchangie,” amesema. Amesema kuwa chama hicho kina utajiri unaokiwezesha kujitegemea na kwamba mwanachama atakayetumia mali za chama kwa maslahi binafsi atachukuliwa hatua kali.

Umoja wa Mataifa waingilia kati sakata la kupotea kwa Ben Saanane

Image
Sakata la kupotea kwa mkuu wa Idara ya Sera na Utafiti wa Chadema, Ben Saanane limechukua sura nyingine baada ya Umoja wa Mataifa (UN) kusema upo tayari kutuma watu nchini kwa ajili ya uchunguzi. Saanane, ambaye pia ni msaidizi wa mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alipotea katika mazingira ya kutatanisha Novemba 18 mwaka jana na hadi sasa haijaeleweka kuwa alitekwa au kuuawa, ingawa Chadema imehusisha kutoweka kwake na taarifa ambayo Saanane aliitoa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu utata wa elimu ya baadhi ya viongozi. Siku chache baada ya kupotea kwa Saanane, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu aliitaka Serikali kueleza kama inamshikilia kada huyo au ifanye uchunguzi wa kina kuhusu kupotea kwake. Sanjari na hilo, Lissu aliitaka Serikali kufuatilia ujumbe wa vitisho ambao Saanane aliwahi kutumiwa kwenye simu yake ya mkononi na mtu ambaye bado hajafahamika. Akisisitiza msimamo wa chama chake, Lissu alizitaka mamlaka zote husika na usalama wa raia ziseme h

MBUNGE BASHE:SINA HOFU NA TIMU TIMU NDANI YA CCM

Image
Mbunge wa Nzega Mjini Hussein Bashe amefunga mazito leo asubuhi kuhusiana na sakata la timua timua linaloendelea dhidi ya wanachama wasaliti ndani ya CCM huko Jijini Dodoma katika Mkutano Mkuu Maalum wa CCM. Mbunge huyo amesema hawezi kuwa na hofu ya aina yeyote kwa kuwa hana jambo baya alilolifanya ndani ya chama hicho hivyo hawezi kuteteleka na wanaotimuliwa wanachama. “Sina hofu na timua timua ya wanachama wasaliti kwasababau naamini wamefanya maamuzi kwa kupitia mchakato ndani ya chama, kwa hiyo sina hofu kwasababu chama chetu kinaongozwa na katiba pamoja  na kanuni zilizopo unakuwa na hofu pale unahisi kuna jambo umelifanya kinyume na taratibu”-Alisema Bashe  Kwa upande mwingine Mbunge huyo amegoma kuzungumzia sakata la yeye kushikiliwa na Jeshi la Polisi hapo jana na kusema suala hilo kamuachia Katibu Mkuu wa chama hicho ndugu Abdurahaman Kinana.

RAIS MAGUFULI NA MWENYEKITI WA CCM AWAPA MAKAVU WALIOIMBA WANA IMANI NA LOWASSA MBELE YA KIKWETE

Image
Mwenyekiti wa Taifa CCM, Rais John Magufuli amewataka makatibu wa mikoa wa chama hicho wanaotaka kuingia katika vikao vya Halmashauri Kuu (Nec) ya Taifa ya chama hicho wakagombee uenyekiti. Akizungumza jana (Jumamosi) wakati wa ufunguzi wa kikao cha Nec, Rais Magufuli amesema kuna watu wanaumuhimu wa kuingia katika vikao vya Halmashauri Kuu na kwamba wakikosa kutakosekana uwakilishi . “Nikawaambia mbona mwaka uliopita waliposimama wakimpinga mwenyekiti makatibu mlikuwepo? Wakati mwenyekiti anawalipa mshahara mbona hamkumtetea? Mbona hamkusimama kupigana na bado wakaendelea kuimba wanaimani na mtu fulani na wengine mkawa mnaitikia,”amesema. Amesema kwa kuwa mabadiliko ya Katiba na Kanuni ambayo yatapunguza idadi ya wajumbe wa vikao vya juu vya chama hicho walishayajadili katika kikao kilichofanyika Desemba 13 mwaka jana, ni matumaini yake kuwa kikao hicho hakitachukua muda mrefu kuyajadili.

VANESSA, DUMISHA HERI WAENDELEA KUSOTA POLISI KWA TUHUMA ZA DAWA ZA KULEVYA

Image
Kamanda Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari juu operesheni mbalimbali zilizofanyika na jeshi hilo kwa wiki moja leo jijini Dar es Salaam. Kamanda Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro akionyesha dawa za kulevya zilizokamatwa katika operesheni leo jijini Dar es Salaam. Kamanda Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro akinyesha gari lililokuwa linatumika kwa ajili ya utapeli na magari yaliyokamatwa kwa tuhuma mbalimbali leo jijini Dar es Salaam. Kamanda Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro akionyesha pikipiki zinazopita katika barabara ya mabasi yaendayo haraka leo jijini Dar es Salaam. Kamanda Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro akionyesha bunduki iliyoteleekezw

Je una herufi "M" katika kiganja chako? Hii ndio maana yake

Image
Watu wengi wanasema, mistari katika viganja vya kila binadamu vimebeba mambo mengi na maana nyingi kuhusu tabia yako na hatima yako kwa ujumla. Pia inasemekana watu wenye herufi  'M'  katika viganja vyao,ni watu wa aina muhimu sana.Inasemekana watu hawa wana sifa za ajabu.Wana ushirikiano mzuri na wafanyakazi katika aina yeyote ile ya biashara. Kama una mpenzi mwenye alama  'M'  katika kiganja chake,basi yakupasa kujua yupo makini katika uhusiano wenu.Hakuna utani,hakuna uongo na hakuna udanganyifu. Watu wenye herufi  'M'  katika viganja vyao, wana uwezo mkubwa wa kufanya mabadiliko katika maisha yao na daima utumia vizuri fursa wanazozipata katika maisha yao. Imekuwa ikijulikana kwa watu wa zamani, kwamba manabii wote walikuwa na alama hii katika mikono yao. Angalia mkoni wako na endapo ukijikuta una alama ya  'M'  basi tambua kwamba wewe ni mtu maalamu.

HIZI NDIO SENTENSI ZA MBUNGE LEMA KATIKA MKUTANO WAKE WA KWANZA ARUSHA

Image
Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema leo amefanya mkutano wa hadhara ukiwa ni mkutano wake wa kwanza tangu alipotoka mahabusu wiki moja iliyopita. Lema amefanya mkutano huo katika uwanja wa Shule ya Msingi Ngarenaro ili kuweza kuzungumza na wapiga kura wake kuhusu mambo mbalimbali yakiwemo ya maendeleo katika jimbo hilo. Miongoni mwa mengi aliyoyazungumza, Godbless Lema amezungumzia kukamatwa kwake ambapo amesema kuwa amekaa mahabusu kwa miezi minne pasipo kuwa na kosa kabisa. Aidha, ameeleza kuwa mahabusu kuwa watu wengi ambao wapo kule kwa kusingiziwa wengine wamewekwa tu kwa uonevu na hawana kosa, hivyo kama kiongozi ataendelea kuwapigania huku akiwasihi wakazi wa Arusha kuwaombea waliopo mahabusu. Mbali na Lema, mwingine aliyepata nafasi ya kuzungumza na umati huo uliojitokeza leo ni mwanachama mpya wa chama hicho, muigizaji Wema Sepetu. Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa

HUU NDIO UJUMBEE ALIOANDAKA STAA WEMA SEPETU KABLA YA MKUTANO WA MBUNGE LEMA

Image
MSANII wa filamu na malkia wa mtandao nchini Wema Sepetu ‘Madam’,  amejikita zaidi katika siasa baada ya kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hivi karibuni. Wema ameendelea kuzianika mitandaoni  baadhi ya harakati zake za kisiasa ikiwa ni pamoja na kujihusisha na shughuli za kijamii kama vile upandaji wa miti,  uliofanywa na baadhi ya viongozi wa chama hicho na leo kabla ya Lema kuhutubia, ameweka picha na ujumbe mtandaoni unaowahamasisha watu kufika katika mkutano huo. “All Ready Kwa Ajili ya Mkutano wa Mhe. GodBless Lema… See you there…. Giving MY Chadema A New Look… Y’all Know Black And Khaki Be our Colour…. A lil White to add Flavor wont Hurt Nobody…. #CallMeKamanda cc @upendosimwita1 @ _ elm _ @blowassa”, alimaliza Wema. Share this

UN SECRETARY GENERAL STOPS IN DAR ON HIS WAY TO NEW YORK

Image
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. Antonio Guterres (kushoto) kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar Es Salaam jana. Mhe. Guterres alisimama kwa muda katika uwanja huo akitokea nchini Kenya kwa ajili ya kufanya mazunguzmo na Balozi Mahiga.  Katika mazungumzo hayo pamoja na mambo mengine, Mhe Guterres aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa juhudi zake za kutafuta amani nchini Burundi kupitia kwa Msuluhishi wa Mgogoro huo Rais wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe. Benjamin Willium Mkapa. Aidha, Dkt. Mahiga aliwasilisha Salamu Maalum kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.  Waziri Mahiga akizungumza jambo huku Mhe. Guterres akimsikiliza kwa makini.  Dkt. Mahiga akiendelea kuzungumza na Mhe. Guterres huku Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa S