HAWA NDIO WALIOTIWA MBARONI KWA TUHUMA ZA KUHUSIKA NA BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA MKOANI KILIMANJARO
Baadhi ya watuhumiwa wa dawa za kulevya waliokamatwa katika msako uliofanyika kwa muda wa siku nne. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi Mwandamizi,Wilbroad Mutafungwa akitaja majina ya watu wanadaiwa kujihusisha na usafirishaji,uuzaji na matumizi ya dawa za kulevya. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini. JESHI la Polisi mkoa wa Kilimanjaro limetaja majina ya watu 47 wanaotuhumiwa kuhusika katika kusafirisha,kuuza na kutumia dawa za kulevya huku likifanikiwa kukamata misokoto 269 na miche 13 ya Bhangi,pamoja na kilogramu 32.9 za mirungi pia ikikamatwa. Kukamatwa kwa watuhumiwa hao pamoja na dawa hizo za kulevya kunatokana na msako mkali uliofanywa na kikosi maalumu cha jeshi hilo kwa muda wa siku nne katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kilimanjaro . Akitangaza majina hayo ofisini kwake ,Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,Kamishna Mwanadamizi Msaidizi wa Polisi,Wibroad Mutafungwa alisema watuhumiwa