Posts

MZEE WA UPAKO NAE AFUNGUA HAYA KUHUSU MADAWA YA KULEVYA

Image
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) Ubungo-Kibangu jijini Dar, Lusekelo Anthony ‘Mzee wa Upako’ amejitaja kuwa ni mmoja kati ya watu mashuhuri ambao wamewahi kutuhumiwa kuhusika na biashara ya dawa za kulevya. Amefunguka na kusema kuwa yeye ni mhanga wa suala hilo jambo ambalo lilimpa wakati mgumu sana katika maisha na kumfanya kunyanyapaliwa na jamii pamoja na watu wake wa karibu wakiwemo wachungaji wenzake. Mchungaji Lusekelo amesema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachofanyika kupitia ukurasa wa facebook wa EATV kila Jumatano. “Mimi ni mhanga wa dawa za kulevya mwaka 1997 nilituhumiwa kuwa nauza madawa, lakini wale askari walikuwa wastaarabu, waliniandikia samasi nikafika kutoa maelezo yangu, lakini baadaye niliwaambia kuwa wao ni polisi wafanye uchunguzi wao, walifanya uchunguzi na kugundua mimi sihusiki, watu walifuatilia na kugundua siyo kweli, na kila mtu akajitoa kwenye, ilionekana kuwa ni wivu tu, ila mbaya zaidi ile

SAKATA LA DAWA ZA KULEVYA ASKOFU GWAJIMA ATEMA CHECE ,ADAI DC MAKONDA ANATUMIKA

Image
Gwajima:   Nakumbuka Kuna siku Makonda alikuwa anahutubia, akamwambia Waziri mkuu eti nlipiga marufuku shisha lakini imerudi, hawa wavuta shisha waliniletea Milion 5 nikakataa akasema lakini naamini kamanda Siro hizi milioni tano tano zimepita kwao. Makonda alidiliki kumtuhumu Waziri MKuu eti Karudisha Shisha!?. DC Makonda ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar, kwanini hakuisemea kwenye Vikao, Kwanini alisubiri Media? Gwajima:   Safari hii kamfikia kiongozi wa Kiroho, huu ni unafiki sana. Huweze kumuita rafiki yako kaka yako namna hii. Gwajima:   Sasa leo nataka niwambie kwanini Makonda anafanya hivi; 1. Nataka niwambie, Rais hajamtuma Makonda atutuhumu sisi 2. System za Serikali zimeparalyse kwa sababu watendaji wa Serikali na Mawaziri wanamuona Makonda ni Mkono wa kiume wa Rais. Wanafikiri labda kwakuwa Makonda ni Msukuma basi atakuwa anatumwa na rais, Rais hawezi kufanya hivyo. Mawaziri wamekosa neno wamekaa Kimya. Gwaji

MANJI AJISALIMISHA POLISI

Image
Mwenyekiti wa klabu ya Yanga ,Yusufu Manji akiwasili katika kituo cha Polisi Kati jijini Dar es Salaam mara baada ya kuamua kujipeleka hapo yeye kwa ajili ya kuhojiwa baada ya kutajwa kwenye watu wanaotuhumiwa na madawa ya kulevya. Yusufu Manji akipokelewa na baadhi ya wanachama wa Yanga katika kituo cha Polisi kati mara baada ya kujipeleka leo badala ya kesho Manji akisalimiana na wanachama wa Yanga katika kituo cha Polisi Kati Mnaji akiwa akiwa ameongozana na mawakili wake na wasaidizi kuingia kituo cha kati jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Yanga Yusufu Manji akisalimiana na Waandishi wa Habari jijini Dar ess Salaam katika kituo cha Polisi Kati

BREAKING NEWS: ANGALIA TUNDU LISSI NAWEMA SEPETU WALIVYOFIKISHWA MAHAKAMANI MUDA HUU WAKIWA KWENYE GARI MOJA

Image
Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu pamoja na Mwigizaji Wema Sepetu wamefikishwa Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kujibu tuhuma zinazowakabili.Tundu Lissu anatuhumiwa kwa kutoa kauli za kichochezi mara kwa mara na Wema Sepetu ni kuhusu ishu za dawa za kulevya Wema Sepetu Tundu Lissu Tundu Lissu Tundu Lissu Wema Sepetu V

Wabunge Wapinga Mbowe Kutajwa na Makonda,Zitto Kabwe Atoa Povu Hili..!!!

Image
Hatua ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kumtaja Kiongozi wa Upinzani bungeni, Freeman Mbowe kufika katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini hapo kesho kuhojiwa, imewachefua baadhi ya wabunge. Wabunge waliohojiwa mjini Dodoma jana, walisema kinachoendelea ni siasa badala ya uhalisia. Mbunge wa Kigoma Mjini, (ACT – Wazalendo), Zitto Kabwe alisema kinachoendelea ni siasa za kuchafuana na kwamba Makonda ajiandae kubeba msalaba wake katika jambo hilo. “Juzi hapa nililalamika bungeni kwamba leo wanakamatwa wasanii, kesho watakamatwa wabunge. Mmeona leo Makonda amemtaja Mbowe. Kinachoendelea ni siasa za kuchafuana. Kitendo cha Makonda kumtaja Mbowe maana yake ni kwamba kazi anayoifanya si yake, ni kazi ambayo ametumwa na wakubwa wake na ndiyo maana wanamuunga mkono,” alisema. Zitto aliwataka wabunge wa upinzani bila kujali tofauti zao za vyama, kuliona suala la Mbowe kuwa si shambulio kwa mbunge huyo wa Hai pekee yake, bali ni mashambulizi dhidi ya wabunge wa

RAIS DKT MAGUFULI AFANYA ZIARA YA GHAFLA KUTEMBELEA UJENZI WA UWANJA WA NDEGE WA JULIUS NYERERE (TERMINAL III) DAR ES SALAAM

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipofanya ziara ya kustukiza katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa Terminal III kuona maendeleo ya ujenzi unaondelea leo Jumatano February 8, 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipofanya ziara ya kustukiza katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa Terminal III kuona maendeleo ya ujenzi unaondelea leo Jumatano February 8, 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipofanya ziara ya kustukiza katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa Terminal III kuona maendeleo ya ujenzi unaondelea leo Jumatano February 8, 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipofanya ziara ya kustukiza katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa Terminal III kuona maendeleo ya ujenzi unaondelea leo Jumatano February 8, 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na baadhi ya wahandisi na mak

RC MAKONDA ATAJA LISTI NYINGINE YA MAJINA 65 YA WANAOHUSIKA NA DAWA ZA KULEVYA

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametaja majina ya watuhumiwa wengine 65 wa madawa ya kulevya, wakiwemo Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Jimbo la Hai, Freeman Elikael Mbowe, Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, Askofu Josephat Gwajima na Mbunge Mstaafu wa Kinondoni, Idd Azzan. Makonda amesema hii ni awamu ya pili ya oparesheni ya kusaka watuhumiwa wa mtandao wa biashara haramu ya madawa ya kulevya, ambapo amesema awamu hii itakuwa ngumu ikilinganishwa na ile ya kwanza iliyohusisha polisi na wasanii kukamatwa. Makonda amewataka watu wote 65 waliotajwa, kuhakikisha wanaripoti kwenye Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam (Sentro) siku ya Ijumaa saa 5 asubuhi kwa mahojiano zaidi. Akizungumza na wanahabari ofisini kwake, Makonda amesema kuwa, waliokamatwa awali ndiyo waliofanikisha kupatikana kwa orodha hiyo mpya.

WIZARA YA HABARI YAZINDUA PROGRAMU YA WADAU TUZUNGUMZE

Image
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza na waandishi wa habari (hawapo Pichani) leo Februari 07, 2017 Jijini Dar es Salaam kuhusu mkakati wa Wizara kuanza kuzungumza na wadau katika sekta zinazosimamiwa na Wizara yake. Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (hayupo pichani) akizungumza leo Februari 07,2017 Jijini Dar es Salaa kuhusu mkakati wa Wizara kuanza kuzungumza na wadau wa sekta zinazosimamiwa na Wizara yake. Picha na Raymond Mushumbusi Na: Genofeva Matemu  Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imebuni na kutanganza Programu ya kushirikisha wadau inayoitwa wadau tuzungumze itakayosaidia wizara kupata vionjo, maoni, mawazo na fikra za wadau katika kuhakikisha kwamba Wizara inafanya kama wadau wake wanavyotegemea. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof.

MTOTO WA DARASA LA NNE AFANYIWA UKATILI KWA KUCHOMWA MOTO MIKONO JIJINI DAR ES SALAAM

Image
Bi.Tatu Rashid mkazi wa Kivule jijini Dar es Salaam amemfanyia ukatili mtoto wake wa kumzaa kwa kumfunga mikono yake miwili,kisha kumuwekea mifuko ya plastiki na kumchoma moto baada ya mtoto huyo kudaiwa kuchukua shilingi 1000. Tukio hilo la kikatili alilofanyiwa mwanafunzi wa darasa la nne jina linahifadhiwa, limetokea jana eneo la Kivule jijini Dar es Salaam,ambapo ITV baada ya kubaini ukatili huo ilifuatilia sakata hilo na kukuta suala hilo likiwa limefikishwa katika ofisi ya serikali ya mtaa wa huo, ambapo mtoto huyo ambaye jina lake limehifadhiwa ambaye ni mwanafunzi wa darasa la nne ameeleza kwamba licha ya licha kumuomba msamaha mama yake mzazi kwa kuchukua shilingi 600 bila kumuomba lakini mama yake hakumuhurumia na badala yake alilazimisha kuwa kachukua shilingi 1000 jambo ambalo limemuhuzunisha baba mzazi wa mtoto ambaye hakuwepo nyumbani wakati wa tukio. Majirani wa familia hiyo wamesema mama huyo baada ya kuona mtoto wake atagundulika kach

MAJALIWA AMTEMBELEA MALECELA DODOMA

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela wakati alipomtembelea nyumbani kwake, Kilimani mjini Dodoma Februari 1, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela wakati alipomtembelea nyumbani kwake, Kilimani mjini Dodoma Februari 1, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela wakati alipomtembelea nyumbani kwake, Kilimani mjini Dodoma Februari 1, 2017. baada ya kuzungumza naye (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA MWAKA MPYA WA KIMAHAKAMA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akihutubia wakati wa uzinduzi wa Mwaka Mpya wa Kimahakama katika viwanja vya Mahakama vya Mtaaa wa Chimala Ocean Road jijini Dar es salaam leo February 2, 2017. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamisi Juma wakati wa uzinduzi wa Mwaka Mpya wa Kimahakama katika viwanja vya Mahakama vya Mtaaa wa Chimala Ocean Road jijini Dar es salaam leo February 2, 2017. Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamisi Juma akihutubia wakati wa uzinduzi wa Mwaka Mpya wa Kimahakama katika viwanja vya Mahakama vya Mtaaa wa Chimala Ocean Road jijini Dar es salaam leo February 2, 2017 wakati wa uzinduzi wa Mwaka Mpya wa Kimahakama katika viwanja vya Mahakama vya Mtaaa wa Chimala Ocean Road jijini Dar es salaam leo February 2, 2017. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph M