WIZARA YA HABARI YAZINDUA PROGRAMU YA WADAU TUZUNGUMZE
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel akizungumza na waandishi wa habari (hawapo Pichani) leo Februari
07, 2017 Jijini Dar es Salaam kuhusu mkakati wa Wizara kuanza
kuzungumza na wadau katika sekta zinazosimamiwa na Wizara yake.
Waandishi
wa Habari wakifuatilia mkutano wa Katibu Mkuu Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (hayupo pichani)
akizungumza leo Februari 07,2017 Jijini Dar es Salaa kuhusu mkakati wa
Wizara kuanza kuzungumza na wadau wa sekta zinazosimamiwa na Wizara
yake. Picha na Raymond Mushumbusi
Na: Genofeva Matemu
Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imebuni na kutanganza Programu ya
kushirikisha wadau inayoitwa wadau tuzungumze itakayosaidia wizara
kupata vionjo, maoni, mawazo na fikra za wadau katika kuhakikisha kwamba
Wizara inafanya kama wadau wake wanavyotegemea.
Hayo
yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Prof. Elisante Ole Gabriel alipokua akizungumza na waandishi wa habari
kutangaza programu hiyo yenye kauli mbiu ya kuitoa wizara ofisini
kuipeleka kwa wadau leo Jijini Dar es Salaam.
Prof.
Gabriel amesema kuwa Wizara imekua na kauli mbiu ya kuitoa Wizara Dar es
Salaam kuipeleka mikoani na sasa inaendelea na mkakati wa kuitoa wizara
ofisini na kuipeleka kwa wadau kwani Shabaa kubwa ya wizara ni
kuhakikisha kwamba yale yanayofanywa na wizara jamii iyafahamu katika
kutekeleza nia na hari ya hapa kazi tuu ya serikali ya awamu ya tano.
“Mpango
wa programu ya wadau tuzungumze utafanyika kisekta ambapo utakua ni
mkutano utakaoshirikisha mmoja wa viongozi wa wizara kukutanana na wadau
na utakua na utaratibu madhubuti kwa kila mwezi siku ya jumanne saa nne
asubuhi ambapo viongozi hao watakutana na vyombo vya habari wakiwa na
wadau kujadili mambo ya kisekta” amesema Prof. Gabriel.
Mpango
huu utahusisha Jumanne ya kwanza ya mwezi sekta ya habari na wadau wote
wa habari, jumanne ya pili ya mwezi ni kwa ajili ya sekta ya Utamaduni
na wadau wote wa utamaduni, jumanne ya tatu ya mwezi ni kwa ajili ya
sekta ya sanaa na wadau wote wa sanaa na mwisho jumanne ya nne ya mwezi
ni kwa ajili ya sekta ya maendeleo ya michezo na wadau wake.
Pamoja na
mambo mengine program hii itatoa fursa kubwa sana kwa wadau kuleta
mawazo yao ili wizara iweze kuwaingiza kwenye mnyororo wa thamani wa
shughuli zake kwani wizara inatamani ifanye kwa mlengo ambao wadau weke
wanatamani ifanyike.
Progamu
hii itazinduliwa rasmi tarehe 14 Mwezi Februari mwaka 2017 hapa Jijini
Dar es Salaam ambapo itahushisha sekta ya Utamaduni na hapo baadaye
mikutano hii inaweza kufikiriwa na kufanywa kwa kanda. Mpango huu
utahusisha pia Taasisi zilizo chini ya wizara.
Comments
Post a Comment