Posts

WABUNGE WATOA POSHO KUSAIDIA MAAFA KAGERA

Image
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (Tamisemi) George Simbachawene amesema madaktari bingwa zaidi ya 15 kutoka Mwanza wamepelekwa Kagera kwa ajili ya kuongeza huduma kwenye hospitali. Kadhalika, wabunge wameunga mkono juhudi za serikali na wameridhia kukatwa posho ya siku moja ili kuchangia kusaidia maafa yao. Hatua hiyo inafuatia muongozo wa mbunge wa Mlalo CCM, Rashid Shangazi aliyeomba kiti kutoa muongozo ili wabunge watoe fedha hizo kama sehemu ya kuomboleza pamoja na waathirika. Hoja hiyo iliungwa mkono na wabunge wa pande zote bila kuangalia itikadi zao. Hata hivyo, Mbunge wa Tarime vijijini Chadema John Heche alisema chama chake kilishatoa Sh 100,000 kila mbunge lakini kufuatia hoja hiyo na wao wapo tayari kuchangia posho zao.

SELECTION ZA VYUO VIKUU KWA WANAFUNZI WALIOOMBA KUJIUNGA NA VYUO MBALIMBALI MWAKA HUU ZIMETOKA

Image
Selection za TCU kwa walioomba kujiunga na vyuo mbalimbali kwa mwaka wa masomo 2016/2017  z imetoka. Bofya hapa  kuangalia     Selection Status  NB:  Tumia index number yako na password

MAAJABU: HUYU NDIYE BINADAMU MWENYE VIDOLE 12 MIGUUNI NA MIKONONI!

Image
Vijay akionesha vidole vyake 12 vya mikono.  Mchapaji wa India Vijay Singh anaweza kuchapa zaidi ya maneno 100 kwa dakika kwa kutumia vidole vyake 12.  Lakini Vijay, ambaye pia ana vidole 12 vya miguuni kutokana na dosari yake hiyo ya kimaumbile, anasema hawezi kupata kazi katika nchi yake aliyozaliwa sababu waajiri wanataka tu wanawake wenye mvuto. Sasa anapanga kuhamia Uingereza kwa lengo la kutafuta ajira baada ya kuwa amekataliwa maombi yake ya kazi zaidi ya 50. Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 48, anayetokea Agra kaskazini mwa India, alisema: "Wanataka wanawake wenye mvuto, si wanaume wenye vidole 12." Miguuni pia, Vijay ana vidole 12.  Watu wenye dosari za kimaumbile wanaonekana wenye bahati nchini India na Vijay yuko kwenye hali nadra kutokana na vidole vyake vya ziada kufanya kazi kama kawaida.  Watu wengi wenye hali hiyo wana vipande vichache vya tishu laini ambazo zinaweza kuondolewa na mara chache huwa na mfupa

Jamhuri Yajibu Kesi Ya Dada’ke Msuya

Image
UPANDE wa Jamhuri leo umetoa majibu ya hoja ya kutaka kufutiwa mashtaka ya mauaji inayomkabili mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita na mfanyabiashara Revocatus Muyela. Awali, wakili wa washtakiwa, Peter Kibatala aliwasilisha maombi ya wateja wake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kile alichodai kuwa hati ya mashtaka ilikuwa ina mapungufu kwa kuwa haioneshi kama washitakiwa hao walikuwa wana nia ovu. Akijibu hoja hiyo ya Kibatala mahakamani hapo, wakili wa serikali, Diana Lukundo alisema hoja zote walizoziwasilisha na upande wa washtakiwa haziko kisheria na kuna aina mbalimbali za kuwasilisha mashtaka. Baada ya upande huo wa Jamhuri kujibu hoja hizo za upande wa washtakiwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkazi Mkuu, Magreth Bankika, mahakama hiyo inatarajia kutoa maamuzi ya hoja hiyo Septemba 27, mwaka huu. Awali ilidaiwa mahakamani hapo kuwa, mnamo Mei 25, mwaka huu maeneo ya Kibada Kigamboni jijini Dar es Salaam, Miriam Mrita na Revocatus Muye

TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KAGERA LAPELEKEA SHULE ZA SEKONDARI ZA IHUNGO NA NYAKATO KAFUNGWA KWA MUDA

Image
Shule ya Sekondari Ihungo iliyoko mjini Bukoba huko Kagera yafungwa hadi Septemba 26 baada ya miundombinu kuharibiwa na tetemeko la ardhi, diwani wa kata ya Nshambya Jimmy Karugendo athibitisha leo asubuhi. Mwenyekiti wa taifa wa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe aliishauri serikali kuifunga shule ya sekondari ya Ihungo ambayo imepata madhara makubwa kutokana na tetemeko la ardhi lilitokea mkoani Kagera na kuunda kamati ya kitaifa ya maafa itakayoshughulikia madhara yaliyotokana tetemeko hilo liliyoyakumba maeneo mbalimbali yaliyoko katika mkoa huo. Alitoa kauli hiyo baada ya kujionea madhara yaliyotokana na tetemeko hilo katika shule hiyo hali inayowalazimu wanafunzi kulala kwenye uwanja na madhara ya nyumba za makazi ambazo zimeharibika vibaya na nyingine kuanguka kabisa, amesema madhara ya tetemeko hilo serikali inapaswa kuyachukulia kama moja ya majanga la kitaifa.

Ummy Mwalimu: Marufuku Kuozesha Waliomaliza La 7

Image
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu. SERIKALI imewaonya wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kutowaozesha watoto wote wa kike waliohitimu darasa la saba mwaka huu wakati wa kipindi hiki cha kusubiri matokeo yao, iwe ni kwa sababu yoyote ile au kwa lengo la kujipatia mali kwa njia ya mahari. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema mkono wa serikali kisheria ni mrefu, hivyo wazazi au walezi watakaokwenda kinyume watahakikisha kuwa wanakamatwa na kufikishwa mahakamani. Ummy ameyasema hayo jana katika tamko maalumu alilolitoa kwa wanafunzi hao waliohitimu elimu ya msingi nchini kote. Alisema wazazi na walezi wanapaswa kutambua umuhimu wa mtoto wake kuendelea kielimu, na kukua kimwili na kiakili kabla ya kuingia katika ndoa kwani elimu ya watoto wa kike ni moja ya njia bora za kupunguza umaskini katika mataifa yanayostawi. “Natoa rai kwa wananchi wote kuendelea kutoa taarifa kw

PROFESA MARK MWANDOSYA AMTEMBELEA NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI.

Image
 Profesa Mark Mwandosya (kushoto) akielezea uzoefu wake alipokuwa Kamishna wa Kwanza wa Nishati na Maendeleo ya Petroli, Wizara ya Nishati na Madini mwaka 1985 mara alipomtembelea Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo. Kulia ni mwakilishi kutoka Kampuni ya Pan African Energy aliyeambatana na Profesa Mark Mwandosya, Jacqueline Kawishe.  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Juliana Pallangyo akielezea maendeleo ya  Idara ya Nishati katika kikao hicho. Kutoka kushoto, Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli Nchini kutoka  Wizara ya Nishati na Madini, James Andilile, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Juliana Pallangyo, Profesa Mark Mwandosya na mwakilishi kut

Rais Magufuli Ateua Makatibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa na Mara

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 09 Septemba, 2016 amemteua Bw. Ado Steven Mapunda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara. Bw. Ado Steven Mapunda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Benedict Richard Ole Kuyan ambaye amestaafu. Pia, Rais Magufuli amemteua Bw. Tixon Tuliangine Nzunda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa. Bw. Tixon Tuliangine Nzunda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Symthies Emmanuel Pangisa ambaye amestaafu. Tarehe ya kuapishwa kwa Makatibu Tawala wa Mikoa walioteuliwa itatangazwa baadaye. Gerson Msigwa Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU Dar es Salaam 09 Septemba, 2016

GIGY MONEY ACHEZEA KICHAPO,NI BAADA YA KUFUMANIWA NA MCHUMBA WA MTU

Image
Baada ya kurukaruka na wanaume tofauti, hatimaye msanii na Video Queen Bongo, Gift Stanford ‘Gigy Money’, amejikuta akichezea kichapobaada ya kufumaniwa akiwa na mchumba wa mtangazaji wa Choice FM aliyetajwa kwa jina moja la Mo, nyumbani kwake Kawe jijini Dar. Video Queen Bongo, Gift Stanford ‘Gigy Money akiwa katika mapozi tofauti. Kwa mujibu wa chanzo makini, Gigy amekuwa hatupii picha za aina yoyote kwenye ukurasa wake wa Instagram kwa sababu ya majeraha aliyopata baada ya msichana aliyefahamika kwa jina la Shov Mohamed kumfumania nyumbani hapo kwa Gigy. “Mnajua Gigy hivi karibuni alifumaniwa nyumbani kwake na mwanaume wa mtu akapata kipondo hevi mpaka hivi ninavyowaambia majeraha ndiyo kwanza yanaanza kupoa na mara nyingi amekuwa akificha majeraha ya usoni kwa kujipaka make up kwa wingi kama akitaka kutoka. “Shov alimfumania baada ya kwenda kwa Mo anayeishi jirani na Gigy, akagonga mlango bila kuitikiwa ndipo alikuja mtu akamtonya kuwa amemuona Mo anaingia ny

Tundu Lissu : Prof. Lipumba Hana Hoja, Anawavuruga CUF

Image
MBUNGE wa Singida Mashariki ambaye pia ni Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni,Tundu Lissu, amesema aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Iblahim Lipumba amekosa hoja ya kuzungumza na badala yake anawavuruga wanachama wa CUF. Lissu ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema amesema Lipumba hakuwahi kuwa na idadi kubwa ya wabunge kama walivyo sasa tangu alipoanza kugombea urais zaidi ya kupata viti viwili tu lakini walipoungana mwaka jana katika umoja wao wa Ukawa wakaibuka  na viti 10. Mbunge wa Singida Mashariki ambaye ni Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mwanasheia Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu akizungumza na wanahabari. (hawapo pichani). Kauli hiyo ameisema leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na wanahabari ambapo aliongeza kuwa Lipumba aache kukiandama Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa madai ya kuwa kinaivuruga CUF. Aliongeza kuwa Lipumba kuendelea kutoa matamshi hayo kwa wanac

PICHA TANO ZA MUONEKANO WA NDANI WA JENGO JIPYA LA J.K. NYERERE AIRPORT TERMINAL 3 JIJINI DAR

Image
Muonekano wa ndani wa jengo jipya la Abiria la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa J.K. Nyerere, jijini Dar es salaam ambalo bado linaendelea na Ujenzi. Mafundi wakiendelea na kazi ndani ya jengo (terminal 3).

Viongozi wa EAC Wagoma Kusaini Mkataba wa Ulaya eac

Image
JUMUIYA ya Afrika Mashariki (EAC), imeiomba Jumuiya ya Ulaya (EU), iipe muda wa miezi mitatu kujua hatima ya wao kusaini Mkataba wa Kiuchumi na Jumuia hiyo (EPA). Uamuzi huo ulifikiwa jana Ikulu Dar es Salaam na viongozi wa Jumuiya hiyo baada ya kikao cha 17 kilichodumu kwa takribani saa sita. Akizungumza baada ya kikao hicho, Mwenyekiti wa EAC, Rais John Magufuli alisema kikao hicho kilikuwa na ajenda nne, ila ya EPA ilikuwa ngumu kulingana na uzito wake. Alitaja ajenda hizo kuwa ni ripoti ya mgogoro wa Burundi, kuingizwa rasmi kwa Sudan Kusini kwene Jumuiya, kupitishwa kwa Naibu Katibu Mkuu wa EAC na EPA. Rais Magufuli alisema viongozi wote kwa pamoja walikubaliana kupewa muda wa miezi mitatu ili Sekretarieti ya EAC iangalie na kupitia masharti ya EPA kabla ya kusaini ili kila mmoja afaidike. Hata hivyo nchi ambazo zilishasaini makubaliano hayo kutoka Jumuiya hiyo ni Kenya. Alisema katika kikao hicho, walibaini mambo 10 ambayo yanapaswa kuangaliwa kabla ya

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI TAREHE 10.09.2016

Image

MAGAZETI YA MICHEZO NA BURUDANI

Image