Jamhuri Yajibu Kesi Ya Dada’ke Msuya
Awali, wakili wa washtakiwa, Peter Kibatala aliwasilisha maombi ya wateja wake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kile alichodai kuwa hati ya mashtaka ilikuwa ina mapungufu kwa kuwa haioneshi kama washitakiwa hao walikuwa wana nia ovu.
Akijibu hoja hiyo ya Kibatala mahakamani hapo, wakili wa serikali, Diana Lukundo alisema hoja zote walizoziwasilisha na upande wa washtakiwa haziko kisheria na kuna aina mbalimbali za kuwasilisha mashtaka.
Baada ya upande huo wa Jamhuri kujibu hoja hizo za upande wa washtakiwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkazi Mkuu, Magreth Bankika, mahakama hiyo inatarajia kutoa maamuzi ya hoja hiyo Septemba 27, mwaka huu.
Awali ilidaiwa mahakamani hapo
kuwa, mnamo Mei 25, mwaka huu maeneo ya Kibada Kigamboni jijini Dar es
Salaam, Miriam Mrita na Revocatus Muyela, walimuua kwa kumchinja dada wa
bilionea Msuya, Anathe Msuya.
Mtuhumiwa, Revocatus Muyela baada ya kutoka mahakamani.
NA DENIS MTIMA/GPL
Comments
Post a Comment