TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KAGERA LAPELEKEA SHULE ZA SEKONDARI ZA IHUNGO NA NYAKATO KAFUNGWA KWA MUDA
Shule ya
Sekondari Ihungo iliyoko mjini Bukoba huko Kagera yafungwa hadi Septemba
26 baada ya miundombinu kuharibiwa na tetemeko la ardhi, diwani wa kata
ya Nshambya Jimmy Karugendo athibitisha leo asubuhi.
Mwenyekiti
wa taifa wa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe
aliishauri serikali kuifunga shule ya sekondari ya Ihungo ambayo imepata
madhara makubwa kutokana na tetemeko la ardhi lilitokea mkoani Kagera
na kuunda kamati ya kitaifa ya maafa itakayoshughulikia madhara
yaliyotokana tetemeko hilo liliyoyakumba maeneo mbalimbali yaliyoko katika mkoa huo.
Alitoa
kauli hiyo baada ya kujionea madhara yaliyotokana na tetemeko hilo
katika shule hiyo hali inayowalazimu wanafunzi kulala kwenye uwanja na
madhara ya nyumba za makazi ambazo zimeharibika vibaya na nyingine
kuanguka kabisa, amesema madhara ya tetemeko hilo serikali inapaswa
kuyachukulia kama moja ya majanga la kitaifa.
Comments
Post a Comment