WABUNGE WATOA POSHO KUSAIDIA MAAFA KAGERA
Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,
(Tamisemi) George Simbachawene amesema madaktari bingwa zaidi ya 15
kutoka Mwanza wamepelekwa Kagera kwa ajili ya kuongeza huduma kwenye
hospitali.Kadhalika, wabunge wameunga mkono juhudi za serikali na wameridhia kukatwa posho ya siku moja ili kuchangia kusaidia maafa yao.
Hatua
hiyo inafuatia muongozo wa mbunge wa Mlalo CCM, Rashid Shangazi
aliyeomba kiti kutoa muongozo ili wabunge watoe fedha hizo kama sehemu
ya kuomboleza pamoja na waathirika.Hoja hiyo iliungwa mkono na wabunge wa pande zote bila kuangalia itikadi zao.
Hata
hivyo, Mbunge wa Tarime vijijini Chadema John Heche alisema chama chake
kilishatoa Sh 100,000 kila mbunge lakini kufuatia hoja hiyo na wao wapo
tayari kuchangia posho zao.
Comments
Post a Comment