MO Dewji aikabidhi Simba Mil. 100 za usajili, asema akiipata bajeti ya usajili itakuwa zaidi ya Bilioni
Hatimaye ahadi ya shabiki wa Simba, ambaye ni Mkurugenzi wa Makampuni ya Mohammed Enterprises (MeTL Group), Mohammed Dewji amekamilisha ahadi aliyoisema kabla ya mkutano mkuu wa Simba kwa kukabidhi Milioni 100 kwa uongozi wa Simba kwa ajili ya kufanya usajili. MO amekabidhi pesa hizo baada ya kueleza mipango yake kwa Simba ya kuwa kama wanachama wa Simba wataridhia kufanya mabadiliko basi atachangia pesa ya usajili jambo ambalo katika mkutano wake wa Jumatatu na waandishi wa habari kuwa ahadi yake ni kweli na ataikamilisha kabla ya dirisha la usajili kufungwa. Akizungumza baada ya kupokea cheki kutoka kwa MO, Rais wa Simba, Evans Aveva, amemshukuru MO kwa msaada huo na sasa wanasimba watatembea kwa kujiamini kwani wamepata pesa ya kufanya usajili. “Nakushukuru MO kwa msaada ambao umetupatia tunaamini ni mapenzi ambayo unayo kwa Simba ndiyo umefanya uwe tayari kutoa pesa hizi na sisi tunaamini zitaweza kutusaidia kupiga hatua na hata tuweze kutembea