Ndege asafiri kutoka Finland hadi Uganda
NDEGE mmoja ambaye inaaminika alitoka nchini Finland amepatikana katika uwanja wa ndege wa Entebbe nchini Uganda.
Ndege
huyo aina ya Osprey (mwewe) kwa sasa anatunzwa na maafisa wa kituo cha
kuwahudumia wanyama cha Uganda Wildlife Education Centre (UWEC).
Ndege huyo mkubwa, aligunduliwa na
maafisa wa uwanja wa ndege katika njia inayotumiwa na ndege kupaa na
kutua katika uwanja wa huo wa Entebbe.
Isaac
Mujaasi, afisa wa mauzo na mawasiliano katika UWEC, ameambia BBC kwamba
ndege huyo alikuwa ameumia katika mabawa yake baada ya kugongwa na
ndege iliyokuwa inapaa.
Alikuwa na pete yenye maelezo kumhusu
mguuni ambayo inaashiria kwamba alimilikiwa na makumbusho ya historia
asilia nchini Finland.
Bw Mujaasi anasema waliwasiliana na maafisa wa makumbusho hao ambao wamethibitisha kwamba ndege huyo ni wao.
Hili
lilituthibitishia kwamba ndege huyu alisafiri kutoka Helsinki,
Finland,” Bw Mujaasi amesema. “Tutamtibu ndege huyo na akipona
tutamwachilia na huenda akarejea kwao.”
Afisa huyo hata hivyo amesema ni kawaida
kwa ndege kuhama kutoka Ulaya, hasa wakati wa majira ya baridi na
kukimbilia maeneo yenye joto.
Comments
Post a Comment