WASANII, WATANGAZAJI NA WATU MAARUFU KUVUNA MAPESA KUPITIA MITANDAO YAO YA JAMII.
Katibu
Mkuu wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante
Ole Gabriel (katikati) akimsifia msanii Diamond Platinumz kwa jinsi
ambavyo amekuwa akiitanga Tanzania nje ya nchi kwa muziki wake.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Aggrey and Clifford, Rashid Tenga alielezea machache
mbele ya wageni na waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo juu ya
huduma mpya ya matangazo katika bara la Afrika utakaowanufaisha
watangazaji, wasanii na watu maarufu uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni Katibu Mkuu wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,
Profesa Elisante Ole Gabriel na Kulia ni Mkurugenzi wa Ukuzaji Biashara
wa Binary, Eni Kihedu.
PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG.
Katibu
Mkuu wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante
Ole Gabrielakimsifia Wema Sepetu jinsi ambavyo amekuwa akilitunza jina
lake.
Msanii Diamond Platinuz akitoa shukrani zake za pekee kwa niaba ya wasanii walihudhuria hafla hiyo.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Aggrey and Clifford, Rashid Tenga (kushoto) akizunguza na
Katibu Mkuu wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa
Elisante Ole Gabriel wakati wa uzinduzi wa huduma ya matangazo kutumia
teknolojia ya kidigitali ambayo itawezesha watangazaji wa biashara
kutangaza biashara zao kwa kuwatumia wasanii na watu maarufu katika
jamii iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Pembeni ni
Wageni waalikwa waliohudhuria shughuli hiyo.
Wasanii waliohudhuria shughuli hiyo.
Waandishi nao hawakuwa nyuma kufuatilia tukio.
Huduma ya matangazo kidigitali kwa kutumia wasanii na watu maarufu yaanzishwa nchini.
KAMPUNI
inaoongozwa kwa kutoa huduma ya matangazo ya biashara nchini ya Aggrey
& Clifford imezindua kitengo cha kutoa huduma ya matangazo kutumia
teknolojia ya kidigitali ambayo itawezesha watangazaji wa biashara
kutangaza biashara zao kwa kuwatumia wasanii na watu maarufu katika
jamii ambayo itanufaisha pande zote zitazoshiriki kutumia huduma hii .
Huduma
hii ya kisasa inayoendana na wakati wa sasa wa kizazi kipya inawezesha
matangazo kuwafikia walengwa wengi na kwa haraka inasimamiwa na kampuni
tanzu ya masuala ya huduma za matangazo ya biashara kwa kutumia
teknolojia ya kidigitali ya Aggrey&Clifford inayojulikana kama
Binary.
Uzinduzi
wa kitengo hiki cha matangazo kwa kutumia teknolojia ya kisasa
itakayoleta mapinduzi katika sekta ya matangazo ya biashara nchini
umefanyika jana katika hoteli ya Hyatt Regency ambapo mgeni rasmi
alikuwa ni Katibu Mkuu wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,
Profesa Elisante Ole Gabriel na ilihudhuriwa na wataalamu wa masoko
kutoka makampuni ya FMCG, huduma za mawasiliano,mabenki na taasisi
mbalimbali za biashara ikiwemo wasanii na wanamichezo.
Kampuni
ya Binary kwa kuanza tayari inashirikiana na wasanii na watu maarufu
Zaidi zaidi ya 40 ambao miongoni mwao wapo wasanii wa
filamu,wanamuziki,watangazaji maarufu wa redio na luninga. Kutokana na
ushirikiano huu Binary itawatumia katika huduma za matangazo za wateja
mbalimbali wanaotangaza huduma na bidhaa zao kidigitali ili kuwafikia
watumiaji wa huduma/bidhaa wengi na kwa urahisi.
Huduma
hii mpya ya matangazo katika bara la Afrika unanufaisha watangazaji kwa
huduma zao kuwafikia wananchi ama wateja wengi kutumia umaarufu wa
wasanii na watu maarufu ambao pia wananufaika kwa kupata mapato ya
uhakika kutokana na kutumiwa kwao katika huduma ya matangazo na pia ina
unafuu kulinganisha na njia nyingine za matangazo.
Profesa
Elisante Ole Gabriel alisema kuwa serikali inao dhamira ya kuwasaidia
wasanii wa tasnia mbalimbali na wanamichezo na alipongeza kuanzishwa kwa
huduma hii nchini ambao itaongeza ajira na vipato vya wasanii wakati
huohuo kunufaisha makampuni kwa njia ya matangazo ya biashara zao.
Naye
Mkurugenzi wa Ukuzaji Biashara wa Binary, Eni Kihedu amesema “Huduma hii
mpya ni jukwaa la aina yake lya matangazo ya baiashara kwa kuwa
inawezesha matangazo kuwafikia walengwa kwa asilimia 100% kwa
kulinganisha na kutangaza kwa kutumia magazeti na ama majarida na
inaleta unafuu kwa watangazaji ambao kwa kutumia mtandao wasanii zaidi
ya 40 ambao tunashirikiana nao kupitia akaunti zao za mitandao ya
kijamii matangazo yataweza kuwafikia watumiaji wa bidhaa na huduma zaidi
ya milioni 20 nchini na tunao uwezo wa kufikia watu wengi zaidi”.
Kuhusiana
na huduma hii mpya ya matangazo itakavyonufaisha wasanii Kihedu alisema
“Tunatumia fursa ya kutumia teknolojia ya digitali katika biashara
ambayo itaongeza vipato vyao wakati huohuo vipaji vyao kuendelea
kuonekana kwa watu wengi katika jamii na kuwawezesha kuwekeza zaidi
kwenye fani yao na tasnia yao”
Aliongeza
kuwa ushirikiano wa Binary na wasanii katika huduma za matangazo
utafanyika kwa uwazi na kunufaisha pande zote na kutafanyika makubaliano
maalumu ya malipo kutokana na viwango vinavyotozwa kwa kila tangazo
litakalowekwa kwenye akaunti za mitandao yao ya kijamii na kulingana na
wafuasi wanaotembelea akaunti zao.
“Viwango
vya matangazo viko wazi kwa watangazaji na wasanii hivyo tunaamini kila
upande utanufaika inavyostahili .Tunaamini njia hii ni jukwaa la aina
yake kwa watangazaji kufikisha matangazo yao kwa wateja wanaowalenga kwa
kuwa njia zilizokuwa zinatumika awali kutangaza hazina nafasi tena
kutokana na mabadiliko ya tekonolojia“.Alisema
Comments
Post a Comment