WASANII WAASWA KUZINGATIA MAADILI KATIKA UTENGENEZAJI WA KAZI ZAO.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akisalimiana na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi Joyce Fissoo wakati akiwasili katika hafla ya uzinduzi wa studio ya kisasa ya Wanene Entertainment Julai 29,2016 Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akisalimiana na mmoja wa wakurugenzi wa Wanene Entertainment Bw. Darish Pandit wakati akiwasili katika hafla ya uzinduzi wa studio ya kisasa ya Wanene Entertainment Julai 29, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura
(kushoto) akimsikiliza kwa makini mmoja wa wakurugenzi wa Wanene
Entertainment Bw. Bhadresh Pandit (kulia) wakati wa hafla uzinduzi wa
studio ya kisasa ya Wanene Entertainment Julai 29, 2016 Jijini Dar es
Salaam katikati ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi Joyce
Fissoo .
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (katikati) akizungumza jambo na wakurugenzi wa Wanene Entertainment Bw. Bhadresh Pandit (kushoto) na Bw. Darish Pandit(wa pili kushoto) wakati wa hafla uzinduzi wa studio ya kisasa ya Wanene Entertainment Julai 29, 2016 Jijini Dar es Salaam wa pili kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi Joyce Fissoo na kulia ni mtayarishaji wa video kutoka kampuni ya Wanene Entertainment Bw. Hanscana.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (wa pili kulia) akikata utepe kuzindua studio mpya ya kisasa ya Wanene Entertainment Julai 29, 2016 Jijini Dar es Salaam wa pili kushoto ni mmoja ya wakurugenzi wa Wanene Entertainment Bw. Darish Pandit.
Naibu
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (wa
pili kulia) akiangalia moja ya vyumba vya kurekodia na kutengengeneza
video vilivyopo ndani ya studio ya Wanene Entertainment mara baada ya
kuizindua studio hiyo Julai 29, 2016 Jijini Dar es Salaam kulia ni
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (kulia) akipata maelezo kutoka kwa mmoja ya wakurugenzi wa Wanene Entertainment Studio Bw. Darish Pandit(kushoto) kwa kuhusu maeneo mbalimbali ndani ya studio hiyo Julai 29, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Mtayarishaji
wa video kutoka kampuni ya Wanene Entertainment Studio Bw. Hanscana
akimuonesha Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.
Anastazia Wambura (aliyekaa) naamna kazi za video zinavyotengenezwa
mara baada ya kurekodiwa katika maeneo mbalimbali alipotembelea studio
hiyo mara baada ya kuizindua rasmi Julai 29, 2016 Jijini Dar es Salaam.
B
aadhi ya wadau waliohudhulia hafla ya uzinduzi wa studio ya kisasa ya Wanene Entertainment Julai 29, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura ( wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wakurugenzi wa studio za kisasa za Wanene Entertainment na wa tatu kushoto ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi Joyce Fissoo.
(Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM)
…………………………………………………………………………………………..
Na Raymond Mushumbusi WHUSM
Wasanii nchini wameaswa kuzingatia maaadili
katika utengenezaji wa kazi zao ili kuenzi na kulinda mila, desturi na
tamaduni za mtanzania .
Wito huo umetolewa jana na Naibu Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura wakati
akizindua studio ya kisasa ya kurekodi kazi za sanaa ya Wenene
Entertainment.
Mhe Anastazia Wambura amesema kuwa baadhi ya
wasanii wamekuwa hawafati maadili katika utengenezaji wa kazi zao na
kuvifanya vyombo vinavyosimamia kazi za sanaa nchini kama Baraza la
Sanaa la Taifa (BASATA) kutoa adhabu dhidi yao kutokana na ukiukwaji wa
maadili katika kazi zao.
“Ninaiomba kampuni ya Wanene Entertainment
kuisaidia Serikali kuwaelimisha wasanii watakaoleta kazi zao
kutengenezwa kwenu kuzingatia maadili badala ya kutengeneza kazi ambazo
haziendani na maadili ya nchi yetu” alisema Mhe Anastazia.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Bodi ya
Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo amehaidi kushirikiana na studio ya
Wanene Entertainment kuendeleza sanaa ya Tanzania kufikia katika viwango
vya kimataifa na kuongeza pato la wasanii na taifa kwa ujumla.
Naye Mkurugenzi wa kampuni ya Wanene
Entertainment Bw.Darsh Pandit amesema kuwa ufunguzi wa studio hiyo ni
muitikio wao kwa Serikali ya awamu ya tano katika suala la kutoa ajira
kwa vijana na kuwezesha vijana kujiajiri kwa kutumia vipaji vyao kupitia
kazi za sanaa.
“Studio hii ina lengo la kukuza na
kuendeleza sanaa ambayo imekuwa ajira kubwa kwa vijana wengi na
tunaahidi kuzingatia maadili katika utengenezaji wa kazi zetu na pia
tutazingatia ubora ili kuitangaza sanaa ya Tanzania kimataifa” alisema
Bw. Pandit.
Aidha mtayarishaji wa video katika kampuni
hiyo Bw. Hasacna amesema kuwa ni fursa sasa kwa watayarishaji wa video
wanaochipukia nchini kuonesha vipaji vyao kwa kuwa wabunifu katika
uandaaji na utengenezaji wa video za muziki na filamu kwa ujumla.
Comments
Post a Comment