Skip to main content

MO Dewji aikabidhi Simba Mil. 100 za usajili, asema akiipata bajeti ya usajili itakuwa zaidi ya Bilioni

Aveva-na-Mohammed-Dewji-MO-702x336
Hatimaye ahadi ya shabiki wa Simba, ambaye ni Mkurugenzi wa Makampuni ya Mohammed Enterprises (MeTL Group), Mohammed Dewji amekamilisha ahadi aliyoisema kabla ya mkutano mkuu wa Simba kwa kukabidhi Milioni 100 kwa uongozi wa Simba kwa ajili ya kufanya usajili.
MO amekabidhi pesa hizo baada ya kueleza mipango yake kwa Simba ya kuwa kama wanachama wa Simba wataridhia kufanya mabadiliko basi atachangia pesa ya usajili jambo ambalo katika mkutano wake wa Jumatatu na waandishi wa habari kuwa ahadi yake ni kweli na ataikamilisha kabla ya dirisha la usajili kufungwa.
Akizungumza baada ya kupokea cheki kutoka kwa MO, Rais wa Simba, Evans Aveva, amemshukuru MO kwa msaada huo na sasa wanasimba watatembea kwa kujiamini kwani wamepata pesa ya kufanya usajili.
“Nakushukuru MO kwa msaada ambao umetupatia tunaamini ni mapenzi ambayo unayo kwa Simba ndiyo umefanya uwe tayari kutoa pesa hizi na sisi tunaamini zitaweza kutusaidia kupiga hatua na hata tuweze kutembea kifua mbele,” alisema Aveva.
Aidha Aveva alisema kiasi hicho cha pesa bado hakijatosha kwa kufanya usajili ambao wamepanga kuufanya lakini kitawasaidia kupiga hatua ya kufanya usajili ambapo kwa msimu huu wamepanga bajeti ya Milioni 400 lakini pia kumtaja mchezaji wa Ivory Coast ambaye wanataka kumsajili ni Fredrick Blagnon.
Kwa uapnde wa MO alisema ametoa msaada huo kama sehemu ya ahadi aliyoitoa kabla ya mkutano mkuu na hakuna makubaliano yoyote lakini pia kuwapa ahadi mashabiki wa Simba kuwa kama akipata nafasi ataweka bajeti zaidi ya Bilioni 1 kwa mwaka kwa ajili ya usajili.

Comments

Popular posts from this blog