Vigogo wote Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Watumbuliwa MAJIPU
SERIKALI imemuondoa katika nafasi yake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), Gerald Kamwenda na wakurugenzi wenzake, katika jitihada za kufumua na kusuka upya shirika hilo. Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, ametangaza hatua hiyo ya serikali jana alipokutana na vyombo vya habari na kuongeza kuwa, watumishi wengine 41 wamehamishwa vituo vya kazi. Alifafanua kuwa hatua hizo ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, lililotaka kufumuliwa na kusukwa upya kwa TFS ili kuongeza ufanisi. Kutokana na hatua hiyo, Waziri Maghembe alisema Profesa Dos Santos Silayo ameteuliwa kuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa TFS, wakati Kamwenda anahamishiwa Chuo cha Viwanda vya Misitu kilichopo Moshi. Aidha, Mwanaidi Kijazi aliyekuwa Mkurugenzi wa Usimamizi wa Raslimali za Misitu na Nyuki, yeye amekwenda kuwa Mhifadhi Mkuu Amani Nature Reserve na nafasi yake inachukuliwa na Zawadi Mbwambo. Waziri Maghembe alisema