Posts

KIKWETE AONGOZA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CCM MJINI DODODMA LEO

Image
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete akifungua Mkutano wa Halmashauri Kuu ya taifa ya CCM mjini Dodoma Julai 21, 2016. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mtarajiwa, Rais John Pombe Magufuli na Wapili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dkt, Ali Mohamed Shein . Kulia ni Makamu Mwenye kiti wa CCM, Bara, Philip Mangula na wapili kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.   Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete akisisitiza jambo mbele ya Wajumbe wa Mutano wa Halmashauri Kuu ya taifa ya CCM mjini Dodoma Julai 21, 2016. Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha  Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete kufungua Mkutano wa Halmashauri Kuu ya taifa ya CCM mjini Dodomam leo Julai 21, 2016. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mtarajiwa, Rais John Pombe Magufuli na Wapili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dkt, Ali Mohamed Shein . Kulia ni Makamu Mwenye kiti wa CCM, Bara,

Mwanaheri: Umbo langu linanitesa

Image
Stori: Imelda Mtema MSANII anayekuja vizuri kwenye Tasnia ya Filamu Bongo, Mwanaheri Ahmed ametoa dukuduku lake la moyoni kuwa umbo lake limekuwa likimtesa sana na mara  nyingi amekuwa hawezi hata kukatiza sehemu waliokaa vijana wa kiume. Mwanaheri ambaye kwa sasa anajizolea mashabiki wengi mitandaoni kutokana na umbo lake, alisema anapata wakati mgumu sana na umbo lake hilo kwa sababu hawezi kusema akatize mitaa ‘korofi’ kama Manzese akiwa anatembea kwa miguu. “Umbo ni zuri na linanipendeza lakini kuna wakati mwingine linageuka kero kabisa maana huwezi kuwa huru useme unaweza kukatiza mitaani bila hofu, yaani ni lazima uchukue usafiri ili uweze kufika sehemu husika,” alisema Mwanaheri ambaye amefanya vizuri kwenye Filamu ya Mwanaheri.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi ya July 23

Image
Advertisement

Yanga yamuacha Kessy

Image
Mchezaji wa Yanga, Hassan Kessy. Wilbert Molandi, Dar es Salaam MSAFARA wa wachezaji 21 wa Yanga, asubuhi ya kesho Jumamosi utaondoka kuelekea nchini Ghana kwa ajili ya kukipiga na Medeama ya nchini humo huku wakiwaacha mabeki wao, Hassan Kessy na Mtogo, Vincent Bossou. Yanga itarudiana na Medeama katika mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika baada kutoka sare ya kufungana bao 1-1 mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Julai 16, mwaka huu. Chini ya Kocha Mholanzi, Hans van Der Pluijm, Yanga inatakiwa kushinda kwenye mchezo huo ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu kucheza Nusu Fainali ya michuano hiyo, kinyume na hapo hali ya mambo inaweza kuwa mbaya na yawezekana wakawa wamefuta ndoto za kusonga mbele. Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh, amesema msafara wao unatarajiwa kuwa na watu 30, kati ya hao, wachezaji ni 21 na viongozi tisa. Amesema msafara huo unatarajiwa kuondoka saa moja asubuhi kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JN

CHADEMA Wafungua kesi mahakama ya Afrika Mashariki dhidi ya Serikali

Image
 Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jana kimefungua rasmi kesi dhidi ya Serikali katika mahakama ya Afrika Mashariki kupinga zuio la kufanya mikutano ya hadhara ya kisiasa. Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Bara), John Mnyika aliwaambia waandishi wa habari kuwa wameamua kufungua kesi hiyo kwakuwa tamko hilo la Serikali ni kinyume cha katiba na mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na sheria ya vyama vya siasa. Mnyika ambaye aliambatana na mwanasheria wa chama hicho, John Mallya alisema kuwa wamekusanya ushahidi wa kutosha wa matamko ya katazo la kufanyika mikutano ya kisiasa na namna chama hicho kilivyozuiwa kufanya mikutano hiyo sehemu mbalimbali nchini. “Tumeleta vielelezo vya zuio lenyewe la polisi kama ushahidi wa kwamba ni kweli polisi wa Tanzania wametoa agizo kama hilo. Pili, tumeleta vielelezo vya mikutano iliyozuiwa… mikutano ya Kahama, Mahafali ya wanachuo wa Chadema kule Dodoma, Mahafali yaliyofanyika kule Moshi na mikutano mingine,”

Msiba: Tasnia ya Filamu Tanzania imepata msiba, R.I.P Mchekeshaji Kundambanda

Image
July 22 2016 ripoti zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kwa baadhi ya mastaa wa vichekesho nchini zikionyesha taarifa ya kufariki kwa mmoja kati ya wachekeshaji maarufu nchini Tanzania,   Ismail Issa Makombe  ‘ Baba Kundambanda’  kutoka kwenye maigizo ya Vituko Show. Taarifa za awali zinadai kuwa amefariki akiwa nyumbani kwao Masasi, Mtwara, endelea kuwa karibu na millardayo.com kwa taarifa zaidi.

Hii ndiyo hoteli mpya aliyofungua Chistiano Ronaldo

Image
FUNCHAL, Ureno M SHAMBULIAJI wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo hatimaye ameifungua hoteli yake ya nyota tano ambayo inaonekana kuwa na ubora wa kiwango cha juu hasa katika suala la ubunifu wa majengo. Ronaldo ambaye kwa sasa yupo katika mapumziko kwenye Fukwe za Ibiza, Hispania amekamilisha mradi huo wa hoteli ambayo ipo katika Mji wa Madeira ambako ndipo nyumbani kwao. Hoteli hiyo iliyopewa jina la The Pestana CR7 Hotel, ina vyumba 48 vya kulala, gym na bwawa la kuogelea ni moja ya hoteli nne ambazo mchezaji huyo amepanga kujenga. Kwenye korido za hoteli hiyo kuna nyasi za bandia pamoja na jezi ya Ronaldo ya timu ya taifa yenye namba saba ambayo ndiyo amekuwa akiitumia. Ndani ya vyumba kuna urembo tofauti kwa kila chumba ambapo pia kuna michezo ya kwenye runinga ‘Play Station’ huku baadhi ya vyumba vikiwa na bei tofauti. Gharama ya kulala katika hoteli hiyo kwa usiku mmoja ni pauni 180 (Sh laki 5), kuna huduma ya bure ya internet, pia kuna baadh

Kisa nguo na kofia… amuua mdogo wake!

Image
  Kakamega TUKIO la aina yake limefanywa kijana Andrew Muganda (26) aliyeripotiwa kumpigwa mdogo yake Wycliffe Shitanda (23) hadi kumuua, kisa kikidaiwa kuwa alivaa nguo na kofia ya kaka yake huyo bila idhini yake, tukio lililotokeas hivi karibuni katika Kijiji cha Shamberere, Malava, Kakamega nchini Kenya. Kutokana na tarifa iliyotolewa na mama yao mzazi, Violet Lagu, Muganda limuuliza mdogo wake kwa nini alivaa nguo zake bila idhini yake, alijibu kwa jeuri. “Nina taaifa zako kuwa umekuwa ukitafuta ugomvi na mimi,” Shitanda alimjibu kaka yake. Papo hapo wawili hao walianza kupigana jambo lililopelekea Muganda kumdhibiti mdogo wake Shitanda kwa kipigo kikali hadi kupoteza maisha yake.