Posts

Mzee Zahir Zorro alivyowakosha wakazi wa Mwanza

Image
Mwanamuziki wa siku nyingi nchini kwenye muziki wa dansi na rhumba, Zahir Ally Zoro (pichani) usiku wa kuamkia Jumamosi aliwaburudisha vilivyo wakazi wa Jiji la Mwanza baada ya kufanya shoo kali katika Ukumbi wa Kilimanjaro Hotel, Nyegezi. Ilikuwa ni shoo yake ya kwanza kwa mwaka huu 2016 ambapo wapenzi wa muziki wa dansi na rhumba walivutiwa na burudani iliyotolewa na Zorro hasa baada ya kuimba live wimbo uitwao “Beatrice” ambao ni wimbo uliofanya vizuri sana wakati anauachia akiwa na bendi yake ya Mass Media. Burudani kutoka kwa Zahir Ally Zorro ikiendelea. JJ Band kutoka Jijini Mwanza, pia walifanya shoo kali katika kumsindikiza Zahir Ally Zorro. Ilikuwa Shoo kali sana ikizingatiwa kwamba wakazi wa Jiji la Mwanza huwa wanaumiss muziki wa dansi/rhumba. Twiga Band kutoka Jijini Mwanza pia walimsindikiza Mzee Zahir Ally Zorro ambapo walifanya shoo nzuri na hivyo kuonyesha kwamba kwa siku za hivi karibuni Mwanza kutakuwa na bendi nzuri. Zahir ...

Maalim Seif atua Pemba, vurugu zaikutanisha CUF, SMZ

Image
Msafara wa Katibu CUF, Maalim Seif Sharif Hamad ukilakiwa na wakazi wa Kisiwani cha Pemba Zanzibar wakati katibu huyo alipowasili kisiwani humo kwa ziara ya kikazi. Picha ya Mtandao Habari Kwanza Maalim Seif aliwasili visiwani humo jana saa 4 asubuhi katika Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume na kulakiwa na mamia ya wafuasi wa chama hicho. Umati wa wananchi wakiongozwa na viongozi mbalimbali wa CUF akiwamo Naibu Katibu Mkuu, Nassor Ahmed Mazrui walijipanga kuanzia uwanjani hapo kuelekea Mji wa Chake Chake, Mkoa wa Kusini Pemba. Hali ilikuwa hivyo katika barabara zote za kisiwani humo mpaka katika Mji wa Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba ambako Maalim Seif alifikia, tofauti na alipokuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa SMZ alikuwa akifikia katika nyumba Serikali iliyopo Mkanjuni, Wilaya ya Chake Chake. Katika ziara hiyo ya kichama, kiongozi huyo anatarajiwa kuonana na viongozi wa wilaya nne za Pemba. Hiyo ni mara ya kwanza kwa kiongozi huyo kutembelea rasm...

NE-YO Kugonga Shoo na Nguli wa Bongo Fleva Wiki Ijayo Mwanza

Image
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu(Katikati)akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, (hawapo pichani) wakati wa kutangaza baadhi ya wanamuziki nchini ambao watatoa burudani pamoja na Mwanamuziki nguli kutoka Marekani NE-YO, katika Uwanja wa (CCM) Kirumba jijini Mwanza kwenye tamasha la Jembeka na Vodacom Festival 2016.Wengine katika picha kushoto ni Mwakilishi wa NE-YO,E.Jay Mathews na Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe ni Jembe ambao ndiyo waandaji wa tamasha hilo, Dkt. Sebastian Ndege. Mwakilishi wa Mwanamuzi nguli toka nchini Marekani NE-YO, E.Jay Mathews (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangazwa kwa wasanii watakaotoa burudani pamoja na mwanamuziki huyo katika tamasha la Jembeka na Vodacom festival 2016, litakalofanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, wapili (kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe ni Jembe ambao ndiyo waandaji wa tamasha hilo,Dkt. Sebastian Ndege, Mati...

MAJALIWA AZUNGUMZA NA WATANZANIA WAISHIO NCHINI UINGEREZA

Image
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza  uliopo London wakati alipowasili ubalozini hapo  kuzungumza na watanzania  waishio  nchini humo Mei  14, 2016.. Kushoto  ni  Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Msafiri Marwa.  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akitia saini kitabu cha wageni wakati alipowasili kwenye ubalozi wa Tanzania  nchini Uingereza uliopo London kuzungumza na Watanzania Mei 14, 2016. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki , kikanda na Kimataifa, Augustine Mahiga na kushoto ni Jaji Mkuu wa Tamzania, Mohamed Othman.  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watanzania Waishio  nchini Uingereza  kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo London Mei 14, 2014.   Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Kikanda na Kimataifa, Augustine Mahiga. Kushoto ni KaimuBal...

MASHINE ILIYOTUMBULIWA NA MAGUFULI UWANJA WA NDEGE, IMEANZA KUFANYA KAZI

Image
Hatimaye mashine iliyotembelewa na Rais JPM jana na kukutwa ikiwa mbovu au haifanyi kazi kwa ufanisi sasa inapiga mzigo kama kawaida na ikiwa chini ya uangalizi wa Maafisa Usalama wa Mamalaka ya Viwanja vya Ndege,Polisi na Afisa wa TRA. Mashine hiyo aina ya Rapscan inayotumika kukaguwa mizigo ya abiria wanaoingia Dsm kutoka Znz,na mikoa mingine ya Tanzania,mapori ya Utalii kama Selous,Mikumi,Sadani na Ruaha pamoja na wasafiri wa nje ya nchi.Ikumbukwe kuwa palikuwa na "uzembe" wa abiria wanaoingia nchini kupitia eneo la TB One,uwanja wa Terminal One una "Status" ya "General Aviation" kwa maana huruhusu kutua ndege za abiria,mizigo na kukodishwa,ambazo zinaweza kuwa za kutoka ndani ya nchi au nje ya nchi Kwa maana hiyo,Arrival ya Terminal One ni tofauti na ile ya Terminal Two,sababu ya Teeminal Two imegawanyika katika sehemu mbili ambazo ni "Domestic Arrival" na "International Arrival",hivyo ndeg...

KIWANDA CHA BIA SERENGETI CHAPIGWA FAINI

Image
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa raisi Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina akipata maelezo jinsi gani kiwanda hicho kinavyochuja maji kwa njia ya kisasa kabisa kwaajiri ya matumizi na uzalishaji kiwandani hapo. Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa raisi Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina wa kwanza kushoto,katikati aliyevaa kanzu ni mbunge wa Temeke(CUF)Mh.Abdallah Mtolea wakitembezwa sehemu mbalimbali za kiwandani hapo mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza. Naibu Waziri Wa nchi Ofisi ya Makamu wa raisi Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina(katikati) akipata maelezo kutoka kwa Afisa mazingira wa kiwanda cha serengeti Bw.Simon Peter mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kiwandani hapo. …………………………………………………………………………………………………. Na Mwandishi wetu-Dar es Salaam Kiwanda cha bia aina ya serengeti kilichopo chang’ombe wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam kimepigwa faini ya shillingi za kitanzania millioni kumi na sita(16)na Baraza la usimamizi wa...

YANGA YAKABIDHIWA UBINGWA WA LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA

Image
Waziri na Kilimo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba (kushoto) akimkabidhi Kombe la ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' jioni ya leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam baada ya mchezo dhidi ya Ndanda FC uliomalizika kwa sare ya 2-2 Wachezaji wa Yanga wakifurahia na Kombe lao jioni ya leo Uwanja wa Taifa

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZINDUA KITUO CHA KISASA CHA HUDUMA ZA MAGARI MKOANI ARUSHA

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro Mhe. Said Meck Saddik alipowasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu Mkoani Arusha, baada ya kukamilisha zira yake ya kikazi katika Mikoa ya Mwanza na Geita. Katikati Mkuu wa Mkoa Arusha Mhe. Daud Felix Ntibenda. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Viongozi na Makamanda wa Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa ya Kilimanjaro na Arusha alipowasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu Mkoani Arusha, baada ya kukamilisha zira yake ya kikazi katika Mikoa ya Mwanza na Geita. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia Vikundi vya Ngoma za aina mbalimbali alipowasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro kwa ajili ya kuanza zi...

Mkenya Adandia Helikopta na Kuning’inia, Apaa nayo Angani

Image
Mwanaume mmoja katika Mji wa Bungoma, Magharibi mwa Kenya ameshangaza ulimwengu baada ya kudandia helikopta ambayo ilipaa angani na kuondoka naye jana. Helikopta hiyo ilikuwa imesafirisha mwili wa mfanyabiashara mashuhuri nchini humo, Jacob Juma aliyeuawa kwa kupigwa risasi na kufariki dunia jijini Nairobi wiki iliyopita, vyombo vya habari nchini Kenya vinasema. Mfanyabiashara Jacob Juma, ambaye pia alikuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Erad  amekuwa akizua mjadala mitandaoni Kenya kutokana na ujumbe wake anaoandika hasa kwenye Twitter, aliuawa kwa kupigwa risasi jijini Nairobi wiki iliyopita. Video zinazosambaa mitandaoni zinaonesha helikopta hiyo ikipaa juu angani kutoka uwanja wa Posta, mwanamume huyo akiwa amejishikilia kwenye vyuma vya helikopta hiyo. Taarifa zinasema baadaye ndege ilitua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa Bungoma na mwanamume huyo kupelekwa hospitali. Wengi wameeleza kushangazwa kwao na tukio hilo la aina yake huku wengine baad...

Nadia Buhari ateswa na aibu

Image
Nadia Buhari Mrembo anayeuza nyago kwenye filamu za Ghallywood, Nadia Buhari amefunguka kuwa tabia yake ya aibu inamtesa sana kiasi kwamba watu wengi wamekuwa wakimchukulia tofauti kuwa anaringa na kujisikia jambo ambalo halina ukweli wowote. Nadia alisema; “Kiukweli aibu inanitesa. Ila watu wanatakiwa kuelewa kuwa nimezaliwa nikiwa na aibu na watu wasinichukulie tofauti, kila mtu anaasili yake.”