KIWANDA CHA BIA SERENGETI CHAPIGWA FAINI
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa raisi Muungano na Mazingira Mh.Luhaga
Mpina akipata maelezo jinsi gani kiwanda hicho kinavyochuja maji kwa
njia ya kisasa kabisa kwaajiri ya matumizi na uzalishaji kiwandani hapo.
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa raisi Muungano na Mazingira Mh.Luhaga
Mpina wa kwanza kushoto,katikati aliyevaa kanzu ni mbunge wa
Temeke(CUF)Mh.Abdallah Mtolea wakitembezwa sehemu mbalimbali za
kiwandani hapo mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza.
Naibu
Waziri Wa nchi Ofisi ya Makamu wa raisi Muungano na Mazingira Mh.Luhaga
Mpina(katikati) akipata maelezo kutoka kwa Afisa mazingira wa kiwanda
cha serengeti Bw.Simon Peter mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza
kiwandani hapo.
………………………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi wetu-Dar es Salaam
Kiwanda
cha bia aina ya serengeti kilichopo chang’ombe wilaya ya Temeke jijini
Dar es salaam kimepigwa faini ya shillingi za kitanzania millioni kumi
na sita(16)na Baraza la usimamizi wa mazingira Nchini(NEMC)baada ya
kutokutimiza masharti ya sheria ya mazingira ya mwaka(2004)na kanuni
zake.
Uamuzi
huo umefikiwa baada ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa raisi
Muungano na mazingira Mh.Luhaga Mpina kupata malalamiko kutoka kwa
wanainchi wanaozunguka maeneo ya kiwanda hicho na kuainisha uchafuzi wa
mazingira yanayowazunguka wananchi hao na kuhatarisha usalama wa afya
zao,ambapo ilimlazimu naibu waziri kufanya ziara ya kushtukiza
kiwandani hapo,huku akiambatana na Wakurugenzi kutoka Baraza la
usimamizi wa mazingira nchini(NEMC)na kujionea uharibifu huo.
Mh.Mpina
ameagiza kiwanda hicho kulipa faini hiyo na kurekebisha miundo mbinu
hiyo ndani ya siku arobaini na tano kusiwepo tena na utiririshaji maji
machafu na yenye kemikali kali za sumu ambayo yanatoa harufu mbaya
inayohatarisha afya za wakazi wa chang’ombe wilaya ya temeke.
Pia
mkurugenzi wa mazingira Bw. Boniventure Baya ametoa siku saba kwa
kiwanda hicho kiwe kimelipa faini hiyo vinginevyo hatua kali za kisheria
zitachukuliwa kutokana na kwamba wamekua wakikaidi maagizo yanayotolewa
na Baraza hilo la mazingira nchini(NEMC)na kuwataka kufanya hivyo
haraka iwezekanavyo baada ya kukiuka sheria ya utunzaji mazingira ya
mwaka(2004) na kutokutimiza masharti waliyopewa takribani miaka miwili
iliyopita.
Naye
mbunge wa Temeke(CUF) Mh.Abdallah Mtolea alisema kiwanda hicho kimekua
na mahusiano mabaya na wananchi wanaozunguka maeneo jirani na kiwanda
hicho hivyo kupelekea kuwa na mgogoro wa muda mrefu na uongozi
kiwandani hapo na kumuomba Naibu waziri kutatua tatizo hilo ambalo
limekua likifanywa kwa makusudi na na uongozi wa kiwanda hicho ilihali
wanajua madhara ya wanayoyapata wananchi.
Aidha
kwa upande wake afisa mazingira wa kiwanda hicho Bw.Simon Peter
alipinga vikali tuhuma hizo ambazo zimeelekezwa katika kiwanda hicho na
kusema uongozi wa kiwanda hicho unafanya kila jitihada ili kuweza
kutatua kero hiyo na si kweli kwamba hawashughulikii tatizo hilo la
mazingira jirani na wakazi hao.
Kwa
upande wao wananchi kupitia kwa Bi.Emanuela Peter,walisema hiyo ni kero
kubwa sana kwao ambapo imekuwa ikiwalazimu kuyahama makazi yao hasa
wakati wa kipindi cha masika ambapo maji ya mvua na yale ya kiwanda
huchanganyikana na kujaza uchafu wote majumbani mwao kutoka kiwandani na
kuhatarisha afya zao hivyo kuhamia kwenye nyumba za kulala wageni kwa
muda,hivyo wameiomba serikali kuangalia kwa makini na kuweza kulipatia
ufumbuzi.
Vilevile
Mh.Luhaga alifanya ziara ya kushtukiza katika kiwanda cha Cement Wazo
kilichopo Tegeta wilaya ya kinondoni jijini Dar es salaam,hata hivyo
hakuweza kukutana na kiongozi yeyote wa kiwanda hicho kwa madai kua
walikua nje ya mkoa wa Dar es salaam,aidha Mh.Mpina alitoa tamko la
serikali kuwa,serikali ya awamu ya tano haina uadui na wafanyabiashara
pamoja na wawekezaji kama inavyozaniwa na watu wengine,bali inachotaka
ni kufuatwa kwa Sheria,taratibu na kanuni kama inavyostahili
Comments
Post a Comment