Mkenya Adandia Helikopta na Kuning’inia, Apaa nayo Angani

160513144717_bungoma_helicopter_man_640x360_courtesytwitter
Mwanaume mmoja katika Mji wa Bungoma, Magharibi mwa Kenya ameshangaza ulimwengu baada ya kudandia helikopta ambayo ilipaa angani na kuondoka naye jana.
Helikopta hiyo ilikuwa imesafirisha mwili wa mfanyabiashara mashuhuri nchini humo, Jacob Juma aliyeuawa kwa kupigwa risasi na kufariki dunia jijini Nairobi wiki iliyopita, vyombo vya habari nchini Kenya vinasema.
160513145050_bungomaman2Mfanyabiashara Jacob Juma, ambaye pia alikuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Erad  amekuwa akizua mjadala mitandaoni Kenya kutokana na ujumbe wake anaoandika hasa kwenye Twitter, aliuawa kwa kupigwa risasi jijini Nairobi wiki iliyopita.
Video zinazosambaa mitandaoni zinaonesha helikopta hiyo ikipaa juu angani kutoka uwanja wa Posta, mwanamume huyo akiwa amejishikilia kwenye vyuma vya helikopta hiyo.
Taarifa zinasema baadaye ndege ilitua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa Bungoma na mwanamume huyo kupelekwa hospitali.
Wengi wameeleza kushangazwa kwao na tukio hilo la aina yake huku wengine baadhi ya Wakenya waliokuwepo kwenye tukio hilo, kwa imani zao wakidai kuwa mwanamume huyo alisahau kama jana ilikuwa Ijumaa tarehe 13, ambayo huwa ni siku yenye matukio mabaya.
Wengine wanatumia majina ya filamu na hata nyimbo. Mfano wimbo wa ‘I Believe I Can Fly’, wake R Kelly na filamu ya Mission: Impossible ambayo mwigizaji nyota wake ni Tom Cruise.




Comments

Popular posts from this blog