Mzee Zahir Zorro alivyowakosha wakazi wa Mwanza
Mwanamuziki wa siku nyingi nchini
kwenye muziki wa dansi na rhumba, Zahir Ally Zoro (pichani) usiku wa
kuamkia Jumamosi aliwaburudisha vilivyo wakazi wa Jiji la Mwanza baada
ya kufanya shoo kali katika Ukumbi wa Kilimanjaro Hotel, Nyegezi.
Ilikuwa ni shoo yake ya kwanza kwa mwaka
huu 2016 ambapo wapenzi wa muziki wa dansi na rhumba walivutiwa na
burudani iliyotolewa na Zorro hasa baada ya kuimba live wimbo uitwao
“Beatrice” ambao ni wimbo uliofanya vizuri sana wakati anauachia akiwa
na bendi yake ya Mass Media.
Burudani kutoka kwa Zahir Ally Zorro ikiendelea.
JJ Band kutoka Jijini Mwanza, pia walifanya shoo kali katika kumsindikiza Zahir Ally Zorro.
Ilikuwa Shoo kali sana ikizingatiwa kwamba wakazi wa Jiji la Mwanza huwa wanaumiss muziki wa dansi/rhumba.
Twiga Band kutoka Jijini Mwanza pia
walimsindikiza Mzee Zahir Ally Zorro ambapo walifanya shoo nzuri na
hivyo kuonyesha kwamba kwa siku za hivi karibuni Mwanza kutakuwa na
bendi nzuri.
Zahir Ally Zorro (kushoto) akiwa katika
mahojiano baada ya shoo. Anasema alifarijika sana baada ya wakazi wa
Jiji la Mwanza kufurahia burudani yake jukwaani ambapo alisisitiza zaidi
media za Mwanza kusupport muziki wa dansi ili kuurudisha kwenye chat.
Zahir Ally Zorro (kushoto) akizungumza na Slyvester Joseph kutoka BMG na Afya Radio ya Jijini Mwanza.
Zahir Ally Zorro akiwa na bango la 102.5 Lake Fm Mwanza.
Mkurugenzi wa Kilimanjaro Hotel, Joseph
Chuwa, akizungumzia shoo ya Zahir Ally Zorro ambapo anasema Mwanza huwa
wanamiss muziki wa dansi hivyo atahakikisha mara kwa mara anawaletea
wanamuziki hao ili kuwaburudisha wana Mwanza na kuongeza kwamba pia leo
Jumapili kutakuwa na Family Bonanza ambapo JJ Band, Twiga Band pamoja na
Zahir Ally Zoro watatoa burudani.
Slyvester Joseph kutoka BMG & Afya
Radio (kushoto) akifanya mahojiano na Alphonce Tonny Kapela (kulia)
kutoka Metro Fm Mwanza kuhusiana na muziki wa dansi pamoja na shoo ya
Zahir Ally Zorro.
Credit:Slyvester Joseph @BMG
Comments
Post a Comment