MASHINE ILIYOTUMBULIWA NA MAGUFULI UWANJA WA NDEGE, IMEANZA KUFANYA KAZI
Hatimaye
mashine iliyotembelewa na Rais JPM jana na kukutwa ikiwa mbovu au
haifanyi kazi kwa ufanisi sasa inapiga mzigo kama kawaida na ikiwa chini
ya uangalizi wa Maafisa Usalama wa Mamalaka ya Viwanja vya Ndege,Polisi
na Afisa wa TRA.
Mashine hiyo aina ya Rapscan
inayotumika kukaguwa mizigo ya abiria wanaoingia Dsm kutoka Znz,na mikoa
mingine ya Tanzania,mapori ya Utalii kama Selous,Mikumi,Sadani na Ruaha
pamoja na wasafiri wa nje ya nchi.Ikumbukwe kuwa palikuwa na "uzembe"
wa abiria wanaoingia nchini kupitia eneo la TB One,uwanja wa Terminal
One una "Status" ya "General Aviation" kwa maana huruhusu kutua ndege za
abiria,mizigo na kukodishwa,ambazo zinaweza kuwa za kutoka ndani ya
nchi au nje ya nchi
Kwa maana hiyo,Arrival ya Terminal
One ni tofauti na ile ya Terminal Two,sababu ya Teeminal Two
imegawanyika katika sehemu mbili ambazo ni "Domestic Arrival" na
"International Arrival",hivyo ndege nyingi za domestic katika Terminal
Two mizigo ya abiria haina haja kukaguliwa sababu watu wanatoka mkoa
mmoja ndani ya nchi kwenda mkoa mwingine,na wale wanaotoka nje ya nchi
hawachanganyikani na wa ndani ya nchi
Uwanja wa Terminal One "Arrival"
hiyo hiyo moja hutumika na abiria wa kutoka Zanzibar,Mikoani,Mbuga za
Wanyama(Porini) na nje ya nchi.Hivyo kuwa na Mashine mbovu eneo la
Arrival ambayo inahudumia watu wanaopita toka Zanzibar(Wakiwa na mizigo
ya kibiashara kwa nia ya kukwepa ushuru) na nje ya nchi ni "kosa"
kiutendaji.Wapo watu kama Pasco wa JF wanaodhani JPM kakurupuka,wasijuwe
kuwa "status" ya Terminal One Arrival sio kama ile ya "Domestic
Terminal Two"
Vijana wa JPM,hatumpi vitu vya
kukurupuka,anapewa data zilizoshiba,ndio maana akifika anaenda moja kwa
moja.Jana baada ya kuongea tu kufika saa kumi mashine zikawa
zimetengenezwa na mizigo inakaguliwa kwa ufanisi mkubwa.Simu nyingi
zilizokuwa zinapitishwa kinyemela toka Dubai via Zanzibar kuja Dsm
zimeanza kunaswa,mali pori zisizo na vibari zinaonekana na hivyo kuwa na
uhakika wa kutambua nini na nini kinaingia nchini.
Kwa taarifa tu ni kuwa Wamiliki
wengi wa ndege Terminal One ni wafanyabiashara wa uwindaji na
utalii,matengenezo ya ndege zao hufanyika nje ya nchi,hivyo hufanya
udanganyifu wa kwenda porini na kubeba mali pori,kurudi Dsm bila
kuushusha mzigo,na baadae kusafiri kwenda nje ya nchi na mzigo
"kimyakimya",na wakati ndege zikirudi toka nje huja na bidhaa ambazo ni
"dutable",na baadae kuingia nchini bila kutozwa kodi
Ujanja mwingine uliokuwa unatumika
na wafanyabiashara wengi ni kushusha mzigo Zanzibar na baadae kuuleta
Dsm na ndege za Charter na hivyo kukwepa kosi,Ndege ya Qatar na Oman Air
hutua Zanzibar,hivyo wafanyabiashara wengi huja na bidhaa na kuzishusha
Znz na baadae wanakuja kama abiria kupitia Terminal One na hivyo
kuingiza nchini bidhaa nyingi bila kulipa kodi,kwa mashine ile
kutokutumika vizuri basi Taifa limepoteza mapato mengi kwa muda mrefu
JPM kwenda pale jana
hajakurupuka,ni matokeo ya jitihada za kumuonyesha sehemu ambapo kuna
mianya ya ukwepaji kodi.., Twende JPM ipo siku watakuelewa,hasa
utakapoanza kuiachia hela unayoikusanya sasa,wacha tule ugali dagaa kwa
muda..Msosi wa uhakika mezani unakuja
By Barafu
Comments
Post a Comment