Posts

BREAKING NEWZ:JPM Avunja Bodi ya TCRA, Amsimamisha Kazi Mkurugenzi Mkuu

Image
Rais Magufuli alipofanya Mkutano na Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameivunja Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Dkt. Ally Yahaya Simba kutokana na kutosimamia ipasavyo Mkataba wa utekelezaji wa mfumo wa usimamizi wa mawasiliano ya simu (TTMS), na kusababisha nchi kupoteza mapato ya takriban shilingi bilioni 400 kwa mwaka. Rais Magufuli amechukua hatua hiyo leo tarehe 26 Aprili, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam baada ya kufanya kikao cha kazi kati yake na viongozi na wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Wizara ya fedha na Mipango na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU). Tarehe 22 Machi, 2013 Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) iliingia mkataba na kampuni ya SGS juu ya uwekaji, uendeshaji na uhamishaji wa mapato ya simu ambapo kampuni hiyo ilipaswa kutekeleza vipengele vitano l

Mbunge Nusura… Akamatwe na ‘unga’ Dar

Image
Kamanda wa Kitengo cha Kupambana na Kudhibiti Madawa ya Kulevya, ACP Mihayo Msikhela Na Makongoro Oging’, UWAZI Dar es Salaam: Jeshi la Polisi Kitengo cha Kupambana na Kudhibiti Madawa ya Kulevya, wiki iliyopita nusura limnase mbunge mmoja kutoka jimbo moja lililopo katika moja ya mikoa ya pwani (jina linahifadhiwa) baada ya kumuwekea mtego kutokana na madai kwamba alikuwa akisafirisha madawa ya kulevya ‘unga’ kutoka kwenye ufukwe mmoja wilayani Bagamoyo kuelekea jijini Dar. Taarifa zilizopatikana kutoka kwa vyanzo vyetu ndani ya jeshi hilo zinadai kuwa, msamaria mwema mmoja alivujisha siri kwa jeshi hilo kwamba, mbunge huyo amebeba unga kwenye gari lake dogo akielekea Dar ambapo bila kupoteza muda, polisi walimuwekea mtego kabambe kwenye njia ambazo alitarajiwa kupita ambapo hata hivyo, aliukwepa baada ya kubadilisha njia. Taarifa zaidi zinaeleza kuwa, mbunge huyo alikuwa akipita usiku wa saa mbili na mzigo huo lakini inadaiwa kuwa alishtukia kwamba amewekew

BREAKING NEWZ:Mke wa Mwai Kibaki Afariki Dunia.

Image
NAIROBI, KENYA Mke wa rais wa zamani nchini Kenya, Mwai Kibaki, Mama Lucy Kibaki amefariki dunia leo asubuhi, Jumanne, Aprili 26, 2016 akiwa kwenye matibabu mjini London Uingereza. Taarifa iliyotolewa na rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta imesema, Mama Lucy Kibaki amefariki akiwa katika hospitali ya Bupa Cromwell mjini London Uingereza alikokuwa akitibiwa. Mwezi mmoja uliopita, Mama Lucy alipewa rufaa ya kwenda Nairobi Hospital akitokea hospitali ya Gertrudeiliyopo Muthaiga, baada ya hali yake kutokuimarika wiki iliyopita alisafrishwa hadi mjini Landon kwa matibabu ambako ndiko mauti yamemkuta. Akithibitisha kifo hicho, rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa kenya imesikitishwa na kifo cha mama Lucy mke wa aliyekuwa rais wa Kenya Mwai Kibaki. Katika taarifa iliotumwa katika vyombo vya habari Uhuru amesema Mama Lucy amekuwa mgonjwa kwa kipindi cha mwezi mmoja. Amesema kuwa Kenya imempoteza mwanamke aliyechangia mengi katika maendeleo ya taifa la Kenya hus

PICHA ZA MAJIVU YA MWILI WA PRINCE YAKIINGIZWA KWENYE GARI ZAONEKANA

Image
Majivu ya mwili wa mwanamuziki nyota Prince ulichukuliwa ukiwa umebebwa kwenye chombo kilichofunikwa na koti jeusi na kuingizwa kweye gari punde tu baada ya kuchomwa moto. Prince ambaye ni muumini wa dhehebu la dini ya Mashahidi wa Yehova aliacha wosia mwili wake kuchomwa na kufanyiwa maziko ya siri na ya kawaida yaliyogharimu dola 1,600.   Majivu ya Mwili wa Prince yakiingizwa kwenye gari huku dada wa marehemu  Tyka Nelson akishuhudia          Dada wa marehemu  Prince, Tyka Nelson, akiwa na majonzi mazito Posted by JAFE MALIBENEKE at Tuesday, April 26, 2016 Email This BlogThis! Share to Twitter Share to Facebook Share to Pinterest

Maajabu Mazishi ya Liyumba

Image
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Joachim Liyumba enzi za uhai wake. Stori: Dustan Shekidele, Wikienda MAHENGE, Morogoro: Rest in peace! Mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Joachim Liyumba (68), aliyefariki Aprili 18 na kuzikwa wikiendi iliyopita kijijini kwao, Kwiro, Mahenge Wilaya ya Ulanga mkoani hapa huku mambo manne yakiwastaabisha waliojitokeza kwenye mazishi hayo. Mwili wapokelewa kwa ngoma ya baba yake Liyumba, ni ngoma aina ya Sangora. Ngoma yakesha Wombolezaji wakiwasili kanisani kwa ajili ya maombezi ya ibada ya kuuaga mwili wa marehemu Liyumba. Wakiwa njiani kuelekea kanisani…. Mwili wa Liyumba wabadilishwa kutoka gari la kwanza na kuwekwa kwenye gari la wagonjwa kisha kuelekea katika Kanisa la Parokia ya Kwiro, Jimbo la Mahenge. Padri Filbert Mhasi akiendesha ibada Mazishi yake yahudhuriwa na watu wachache. Chanzo chabainika kwa nini

JPM Ateua Makatibu Tawala wa Mikoa 26

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 25 Aprili, 2016 amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara. Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa kati ya Makatibu tawala hao 10 ni wapya, 2 wamebadilishiwa vituo vya kazi na 13 wamebakisha katika vituo vyao vya sasa. Makatibu Tawala wapya walioteuliwa ni kama ifuatavyo;     1. Arusha –    Richard Kwitega     2. Geita –      Selestine Muhochi Gesimba     3. Kagera –     Armatus C. Msole     4. Kilimanjaro –    Eng. Aisha Amour     5. Pwani –      Zuberi Mhina Samataba     6. Shinyanga –   Albert Gabriel Msovela     7. Singida –     Dr. Angelina Mageni Lutambi     8. Simiyu –    Jumanne Abdallah Sagini     9. Tabora –   Dkt. Thea Medard Ntara    10. Tanga –    Eng. Zena Said Makatibu Tawala waliobadilishwa vituo vya kazi ni kama ifuata

BREAKING NEWS : CAG ATAJA MAJIPU SUGU KWA TAIFA

Image
========= UPDATES: ========= => Ulaji na uzembe vinatajwa kubeba sehemu kubwa ya ripoti hii. => Misamaha ya kodi 2014/15 ni asilimia 2 ya pato la taifa kinyume cha asilimia 1 => Halmashauri 40 hivi ndo zenye hati safi kati ya halmashauri zaidi ya 160 => Bidhaa a bilioni 9 za kupelekwa nje ziliuzwa hapa hapa nchini. Upigaji huo wa ukwepaji kodi. => Bidhaa za bilioni 89 za nje hakuna ushahidi kama zilienda Rwanda, Burundi na Uganda. => Rufaa za kodi nyingi mno zimedoda mahakamani na hivyo kuikosesha serikali kodi => Deni la Taifa hadi Juni 2015 lilifikia trilioni 33.5. Ndani ya mwaka mmoja lilikua kwa trilioni 7! => Malipo kwa deni kwa mwaka ni trilioni 4. => Deni na mishahara inamaliza mapato yote ya taifa. CAG anahoji, tutapata wapi pesa za maendeleo? => CAG Anataka maduka ya fedha za kigeni yadhibitiwe => Vyama vya siasa, kimoja tu kimewasilisha hesabu. Vyama 21 bado, Msajili afiatilie. Hajakitaja chama kilichowasilisha => Mishahara hewa ka

RC Mwanza Atoa Saa 24 Kompyuta iliyoibwa ipatikane Ukerewe

Image
Mkuu wa mkoa wa mwanza John Mongella. Mkuu wa mkoa wa MWANZA John Mongella  ametoa saa 24 kwa kamanda wa Polisi Wilaya ya Ukerewe Ally Mkaripa, kuhakikisha wanaitafuta hadi kuipata komputa iliyoibwa usiku wa kuamkia April 22, 2016 kwenye chumba kinachotumika na mifumo ya ukusanyaji mapato  na uaandaji wa malipo ya Halmashauri (EPICOR) Mhe. Mongella ametoa agizo hilo wakati  akizungumza kwenye kikao cha kujitambulisha kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri,ambapo taarifa za awali zilionesha kutokea kwa wizi wa komputa moja iliyofungwa kwenye chumba cha mifumo ya komputa ambayo ndio hutumika kuandaa malipo mbali mbali ya halmashauri. “OCD kesho nitakwenda kanisani asubuhi, ikifika saa 8.00 mchana nataka taarifa niikute mezani kwangu, vinginevyo hatutaelewana”, amesema Mongella na kuongeza sisi tunajua nini chakufanya kama kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa lakini na wewe tumia mbinu zako kuweza kubaini wapi ilipo kompyuta hiyo. Akizungumza kando ya ukum

Serikali Yapangua Hoja Moja ya UKAWA

Image
SIKU moja baada ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kususa kuchangia hotuba za bajeti, Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Florence Mwanri, amesema serikali haikukosea kuipa Wizara ya Ujenzi fedha zaidi ya zilizokuwa zimeidhinishwa na Bunge. Hoja hiyo ni moja kati ya tatu ambazo juzi ziliibuliwa bungeni na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe. Badala ya kuwasilisha Mpango Mbadala wa Maendeleo wa Taifa na maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu mpango wa serikali pamoja na maoni ya kambi hiyo kuhusu hotuba ya Waziri Mkuu, juzi Mbowe alisema wabunge wa upinzani watakuwa wanaingia kwenye Ukumbi wa Bunge lakini hawatachangia hotuba ya bajeti mpaka pale hoja zao zitakapojibiwa. Mbowe alidai kuwa uamuzi wao huo umetokana na Serikali kufanya kazi bila kuwa na mwongozo wa utendaji kazi kwa wizara mbalimbali, kuvunjwa kwa Katiba na sheria za nchi na kupokwa uhuru na madaraka ya muhimili wa Bunge. Mwenyekiti huyo wa Chadema na Mbunge wa Hai

NAPE AZINDUA TAMASHA LA KIMATAIFA LA FILAMU MJINI ARUSHA

Image
Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akifunua pazia kuashiria uzinduzi wa Tamasha la kimataifa la filamu la Tanzanite mjini Arusha. Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (mwenye kaunda suti ya kijivu) akiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Ndugu Felix Ntibenda kwenye picha ya pamoja na viongozi pamoja na wadhamini kwenye uzinduzi wa Tamasha la Kimataifa la Filamu la Tanzanite. Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza wakati wa uzinduzi wa tamasha la Kimataifa la Filamu la Tanzanite mkoani Arusha . Waziri Nape aliwaambia wadau na waigizaji wa Filamu waliohudhuria uzinduzi wa Tamasha hilo kuwa hii ni moja ya hatua kubwa kwenye historia ya filamu nchini na kuahidi Wizara yake itaendelea kutoa ushirikiano mkubwa na kuhakikisha haki za wasanii hazipotei wala haziliwi na wajanja. Mkurugenzi wa Tanzanite One ambao ndio wadhamini wakuu wa Tamasha, Ndugu Faisal Juma akiz

Binti anayefanya kazi Mochwari atinga Global TV

Image
Sabrina Gharib (19) anayefanya kazi kwa vitendo kimasomo  kwenye Mochwari  ya Hospitali ya Rufaa ya Tumbi Kibaha mkoani Pwani, leo ametembelea Global Publishers na kufanyiwa mahojiano na Global TV Online. Sabrina Gharib (kulia) akiwa na mama yake Asha Ramadhani wakiendelea kufanya mahojiano. Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa,  Oscar Ndauka akiongea nao jambo. Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (kushoto) pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Global wakizungumza jambo na wageni hao. Sabrina Gharib akiwa katika mapozi tofauti na wafanyakazi wa Global Publishers. BINTI mwenye miaka 19, Sabrina Gharib, anayefanya kazi kwa vitendo kimasomo  kwenye Mochwari  ya Hospitali ya Rufaa ya Tumbi Kibaha mkoani Pwani, amekuwa gumzo kwa watu wanaokwenda kuchukua miili ya wapendwa wao hospitalini hapo, leo ametinga ndani ya mjengo wa Global Publishers na kufanyiwa mahojiano na Global TV Online. Akifanyiwa mahojiano katika kipindi cha Exclusive, Sab

UGANDA IMETANGAZA RASMI KUTUMIA BANDARI YA TANGA NCHINI TANZANIA KUSAFIRISHIA MAFUTA GHAFI YAKE.

Image
Hatimaye Serikali ya Jamhuri ya Uganda imetangaza rasmi uamuzi wake wa kutumia Bandari ya Tanga nchini Tanzania kusafirishia mafuta ghafi yake.  Uamuzi huo umetangazwa na Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Jamhuri ya Uganda wakati wa Mkutano Mkuu wa 13 wa Ushoroba wa Kaskazini uliomalizika Jijini Kampala Uganda.  Ujumbe wa Tanzania ulio kamilisha mazungumzo hayo na hatimaye kushuhudia utangazwaji wa hatua hiyo uliongozwa na Mhe. Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa . Jopo la wataalamu kutoka Tanzania lililoongozwa na Mhe. Prof. Sospeter Muhongo bado wako jijini Kampala kukamilisha mpango huo wa Bomba la Mafuta Ghafi ambapo pia nchi nyingine za Afrika Mashariki na Kati zinatarajia kunufaika. Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dar es Salaam 23 Aprili, 2015

MWANAMUZIKI NGULI WA CONGO PAPA WEMBA AFARIKI DUNIA

Image
Mwanamuziki Papa Wemba enzi za Uhai wake. Mwanamuziki nguli wa Congo Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba maarufu kama Papa Wemba amefariki dunia huko Abidjan, Ivory Coast, usiku wa kuamkia leo. Habari zilizotufikia hivi punde zinasema marehemu Papa Wemba amefia hospitali alikokimbizwa mara baada ya kuanguka na kupoteza fahamu wakati akiwa katika onesho jukwaani. Papa Wemba alizaliwa June 14, 1949 huko Lubefu katika wilaya ya Sankuru nchini Congo. Alijipatia umaarufu sana kwa sauti nyororo na midundo ya Soukous ulimwenguni kote, ikiwamo Tanzania ambako amezuru mara kadhaa na kujizolea mashabiki wengi.  Papa Wemba akiwa jukwaani kwa mara ya mwisho jijini Abidjan, Ivory Coast, usiku wa kuamkia  Papa Wemba aanguka na kupoteza fahamu katikati ya onesho Wafanyakazi wa huduma ya kwanza wamepanda jukwaani. Hali ilizidi kuwa mbaya wakamkibiza hospitali ambako alikata roho

RAIS MSTAAFU, MHE. DKT JAKAYA MRISHO KIKWETE AKUTANA NA WANAFUNZI NA WANACHAMA WA CCM WAISHIO JIJINI BEIJING - CHINA.

Image
Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete, akijiandaa kuzungumza na Wanafunzi na wanachama wa CCM waishio Mji wa Beijing nchini China.  Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete, akizungumza na wanafunzi na Wanachama wa CCM, waishio nchini China, wakati alipokutana nao akiwa katika ziara yake nchini humo. ************************************** Na Mwandishi Wetu, Beijing China Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi {CCM} na Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo tarehe 20th April 2016 amekutana na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wa Tawi la Beijing ambao ni Wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya elimu ya juu, katika Ukumbi wa Grand uliopo katika Makazi ya Viongozi ya Diaoyutai State Guesthouse jijini Beijin, nchini China. Wakisoma risala yao, Wanafunzi hao kutoka vyuo mbalimbali vilivyopo Beijin na miji ya karibu kama vile Tianjin walimuhakikishia Mheshimiwa Dkt. Kikwete kuwa wao ni waaminifu na wazal