Posts

KIPA WA SIMBA AFUNGIWA MIAKA 10, GEITA GOLD NA POLISI ZASHUSHWA DARAJA

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),  chini ya Makamu Mwenyekiti wake, Wakil Jerome Msemwa leo imetoa maamuzi ya shauri la upangaji matokeo kwa mechi za Kundi C Ligi Daraja la Kwanza. Akisoma hukumu hiyo baada ya kumaliza kuwahoji viongozi wa klabu na Wenyeviti wa vya vyama vya mikoa husika jana, Wakili Msemwa amesema adhabu hizo zimetolewa kwa kufuata Kanuni za Nidhamu za TFF, na nafasi ya kukata rufaa kwa wahusika juu ya maaamuzi hayo ziko wazi. Klabu za Geita Gold (Geita), JKT Oljoro (Arusha) na Polisi Tabora (Tabora) zimekutwa na hatia ya upangaji wa matokeo na kupewa adhabu ya kushushwa daraja mpaka ligi daraja la pili (SDL) msimu ujao. Upande wa klabu ya JKT Kanembwa FC ya mkoani Kigoma, imeshushwa daraja mpaka kwenye ngazi ya ligi ya mkoa (RCL), baada ya kushika nafasi ya mwisho katika msimamo wa kundi lake, Kundi C. Kamati ya Nidhamu imewafungia maisha kutojihusisha na mpira wa miguu mwamuzi wa mchezo k

BARAKA DA PRINCE NA NAJ WAONYESHEANA MAHABA HADHARANI, CHEKI PICHA HIZI

Image
Couple ambayo inazungumziwa sana kwa sasa kwenye mitandao ya kijamii na hata kwenye media ni ya Baraka Da Prince na Naj, Na hii ni baada ya tetesi kuwa Baraka amekuwa na tabia ya kuwapitia wasanii kimapenzi hadi kutungiwa jina la Zipu Mbovu. Baraka na Naj baada ya kutoka kwenye show ya Friday Night Live ya EATV na EA Radio walienda kujimwaga kwenye kumbi mbali mbali za starehee na ndipo picha hii ikanaswa. Unadhani Baraka na Naj watadumu kwenye mapenzi kutokana na jina walilonalo kwenye tasnia ya muziki?

RAIS DKT. MAGUFULI NA RAILA ODINGA WASHIRIKI IBADA YA JUMAPILI YA PILI YA PASAKA CHATO MKOANI GEITA.

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri mkuu mstaafu wa Kenya Raila Odinga wakisali katika kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita. Rais Dkt. Magufuli amesali ibada ya jumapili ya pili ya Pasaka tangu kuchaguliwa kuwa Rais. Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Raila Odinga pamoja na Mke wa Raila Bi. Ida Odinga wakifatilia kwa makini mahubiri ya Paroko Padre Henry Mulinganisa katika ibada ya pili ya pasaka Chato Mkoani Geita. Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisali katika kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita. Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisali katika kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita. Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Mke wa Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya, Bi. Ida Odinga, Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya Raila Odinga pamoja na Rais Dkt. John Magufuli wakifatilia kwa makini mahubiri yaliyokuwa yakitolewa katika kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita. Rai

ZIFAHAMU FAIDA KUMI ZA MMEA WA ALOE VERA KWA BINADAMU...

Image
                                                                  mmea wa aloe vera ni mmoja ya mimea ambayo imejizoelea umaarufu miaka hii ya karibuni  baada ya kuonyesha kutibu na kuzuia aina mbalimbali za magonjwa, lakini pia kurefusha maisha na kupunguza makali ya magonjwa yasiyopona kama kisukari, presha, magonjwa ya moyo, pumu, kifafa, ukimwi na mengine mengi, lakini mmea huu ulikua ukitumika tangu miaka ya zamani sana na watu waliishi miaka mingi wakiwa na nguvu na akili kupitia mmea huu. kwa faida za mmea huu ni bora kumiliki hata bidhaa moja tu ambayo utakua unaitumia siku zote za maisha yako ili kupunguza uwezekano wa kupatwa na magonjwa hatarishi..kwa sasa kampuni ya forever living product ndio inaongoza kwa mauzo hayo duniani, ikiwa imetapakaa zaidi ya nchi 150.hapa tanzania ikiwa  imeuaza zaidi ya bilioni ishirini kwa mwaka jana tu  na kulipa kodi serikali zaidi ya bilioni tano za kitanzania, hii inaonyesha watanzania wameamka na wanatumia sana bidhaa

Mwanamuziki Lady Jaydee Azungumzia Msanii wa Kiume Anaemfikiria Sasa Kushirikiana Naye

Image
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Lady Jaydee ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake wa 'Ndi ndi ndi' amefunguka na kuweka wazi wazi msanii wa kiume ambaye kwa sasa anamfikiria katika kufanya nae kazi. Kupitia Accout yake ya twitter ambapo alitoa nafasi ya maswali kutoka kwa mashabiki zake Lady Jaydee aliulizwa swali kama ataweza kufanya remix ya wimbo wake mpya na kama atafanya hivyo anadhani ni msanii gani wa kiume ambaye ataweza kufanya nae kazi hiyo. Ndipo hapo aliposema kwa sasa anamfikiri sana Mr Blue. "Kiukweli mtu niliemfikiria hapo ni Mr Blue, naona ndio ata fit vizuri zaidi, Msanii wa Tanzania alieko akilini kwangu hivi sasa ni Mr Blue" alisisitiza Lady Jaydee Mbali na hilo msanii huyo aliweka wazi sababu za ukimya wake kwenye muziki kabla ya kuja na wimbo huo mpya na kusema kuwa huo ndio utaratibu wake toka amenza muziki na toka anatoka na Album ya kwanza mwaka 2001 yeye si mtu ambaye anatoka ngoma mara kwa mara bali huwa

Shamsa: Nusura niharibike ubongo kwa kipigo

Image
Staa wa filamu Bongo, Shamsa Ford. Stori: Imelda Mtema Staa wa filamu Bongo, Shamsa Ford amefunguka kuwa amekutana na kipigo cha mara kwa mara kipindi anaishi na baba mtoto wake Dickson Matok ‘Dick’ kiasi ambacho alikuwa akikaribia kupata athari kwenye ubongo. Akizungumza na mwandishi wa habari hii hivi karibuni, Shamsa alisema kuwa amenusurika kumpoteza mtoto wake akiwa tumboni kutokana na mitama aliyokuwa akipigwa na mpenzi wake huyo lakini kwa sababu alikuwa anampenda alikuwa habanduki. “Jamani napinga vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake wenzangu kwani ilibaki kidogo niharibike ubongo kwa kipigo cha mwanaume huku nikiamini napendwa kumbe ni ujinga mtupu,” alisema Shamsa

Fina Mango na Masoud Kipanya waongezeka katika timu ya Power Breakfast ya Clouds Fm

Image
Siku kadhaa zilizopita katika mitandao ya kijamii zilisambaa habari za kuwa watangazaji wa kipindi cha Power Breakfast ya Clouds Fm, Gerrard Hando na Paul James (PJ) wameondoka katika redio hiyo. Katika kipindi hicho cha Power Breakfast leo Ijumaa, Aprili 1 zimesikika sauti mpya katika kipindi hicho ambapo ni Fina Mango na Masoud Kipanya ambao wamesikika katika kipengele cha kuperuzi na kudadisi ambacho kinahusika na kupitia magazeti ya siku husika. Baada ya kuongezeka kwa watangazaji hao, inaonyesha dhahiri kuwa Gerrard Hando na PJ watakuwa wameondoka katika kituo hicho baada ya kudumu kwa kipindi kirefu ambapo mikataba yao ilimalizika jana Machi, 31.

MAKONDA AWAGEUKIA BODABODA WA DSM.AWAAHIDI PIKPIK KWA SH.3,500 KWA SIKU,KUINGIA POSTA.

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekutana na waendesha pikipiki za kubeba abiria maarufu kama Bodaboda mkoani humo na kuwapa ahadi nono za kuwainua kimaisha kupitia biashara hiyo. Pamoja na mambo mengine, Makonda ameahidi kuwapa pikipiki bodaboda hao kwa marejesho ya shilingi 25,000 kwa wiki (sawa na shilingi 3,500) kwa siku na baadae kuwaachia wazimiliki wao. Mwendesha bodaboda akiwa amepakia abiria watatu kwenye chombo hicho cha usafiri, jambo ambalo ni hatari kwa usalama wao, kama walivyokutwa eneo la Mwembeyanga, jijini Dar es Salaam juzi. Picha na Joseph Zablon (Maktaba) Katika hatua nyingine, Makonda ameahidi kuwatengenezea mpango mzuri wa utakaowawezesha bodaboda hao kuingia katikati ya Jiji, tofauti na ilivyo sasa. Ahadi ya Makonda kuwaruhusu Bodaboda kuingia Jijini ni ukamilifu wa ahadi ya Rais John Magufuli wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana. Juzi, Meya mpya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita (Chadema) pia

SAKATA LA WASTARA MAPYA YAIBUKA,MBUNGE ASEMA AMELOGWA NA WASTARA,AJIBU MAPIGO,AELEZA MAZITO

Image
  Makubwa! Aliyekuwa mume wa nyota wa Filamu za Bongo, Wastara Juma ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Donge (CCM), Zanzibar, Sadifa Juma ameibua jambo zito miongoni mwa jamii akidai kuwa, mtalaka wake, Wastara Juma amekuwa akimroga, twende na Risasi Jumamosi. Madai hayo aliyatoa Alhamisi iliyopita baada ya gazeti hili kumuuliza habari zilizoenea kwamba, amemuangukia Wastara akitaka warudiane kwani yaliyopita si ndwele. Sadifa alisema kuwa, aligundua hilo la kurogwa baada ya Wastara kuondoka nyumbani kwake na kutangaza kwenye vyombo vya habari kuwa, amepewa talaka mbili. Akizungumza kwa dakika 25, Sadifa alikwenda mbele zaidi kwa kusema: “Ukimwangalia Wastara harakaharaka unaweza kusema ni mwema sana lakini hana wema wowote. Hivi Wastara ni wa kuniroga mimi kweli?” ILIKUWA HIVI Risasi Jumamosi: (baada ya kujitambulisha na salamu) “mheshimiwa tunataka kujua nini kinaendelea kati yako na mkeo Wastara?” Mume: “Kuhusu nini?” Risasi Jumamosi: “Kuna madai kwamba, umea

NAIBU WAZIRI MAMBO YA NDANI YA NCHI ATEMBELEA GEREZA LA BANGWE AFANYA MAZUNGUMZO NA WATUMISHI WA WIZARA MKOANI KIGOMA

Image
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(katikati), akiongozana na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kigoma, SACP Sabas Matolo(kushoto) na Mkuu wa Gereza la Bangwe,SSP Raphael Mwanyingile(kulia), alipofika kutembelea gereza hilo katika ziara ya kikazi mkoani Kigoma tarehe 31/3/2016. Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, akisaini kitabu cha wageni katika Gereza la Bangwe mkoani Kigoma, ambapo baadae alisikiliza risala iliyohusu  mambo mbalimbali,  iliyoandaliwa na wafungwa na mahabusu walioko katika gereza hilo na kuahidi kushughulika changamoto zao. Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kigoma, SACP Sabas Matolo, akisoma taarifa ya hali ya magereza mkoani Kigoma mbele ya Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni.Naibu Waziri yuko mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi. Mmoja wa Askari Magereza mkoa wa Kigoma, akizungumza wakati wa kipindi cha maswali kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nch

Tuhuma za Rushwa: Mbunge Ndassa Naye Afikishwa Kortini

Image
Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa. MBUNGE wa Sumve, Richard Ndassa amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar, leo akituhumiwa kuomba rushwa ya Shilingi  milioni 30  akiwa kwenye Kamati za Bunge. Ndasaa  anakuwa  mbunge  wa  nne  wa  CCM kupandishwa  mahakamani  kwa  tuhuma  za  rushwa  baada  jana wabunge Mh.Kangi Lugola wa jimbo la Mwibala, Mh.Sadiq Murad wa jimbo la Mvomero na Mh.Victor Mwambalaswa wa jimbo la Lupa kupandishwa  mahakamani kwa tuhuma za kuomba rushwa ya milioni 30 toka kwa mkurugenzi wa Wilaya ya Gairo  ili taarifa yake ipitishwe bila kujadiliwa.

SERIKALI KUPITIA UPYA MIKATABA YA TRL

Image
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (katikati) akimsikiliza mmoja wa abiria anayetumia usafiri wa reli ya kati mkoani Kigoma. Kushoto ni Mbunge wa Kigoma Mjini, Mhe. Zitto Kabwe na Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Saveli Maketta. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza na wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), mkoani Kigoma. Muonekano wa mabehewa ya treni yakiwa mwisho wa reli ya kati, mkoani Kigoma. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Kapteni wa Meli ya MV Liemba ya namna inavyoendeshwa, mkoani Kigoma. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa tatu kulia), akipata ufafanuzi wa namna ya injini za Meli ya MV Liemba zinavyofanya kazi wakati alipotembelea Meli hiyo mkoani Kigoma. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (mwenye kizibao cha njano), akimsikiliza Kapt