MAKONDA AWAGEUKIA BODABODA WA DSM.AWAAHIDI PIKPIK KWA SH.3,500 KWA SIKU,KUINGIA POSTA.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekutana na waendesha
pikipiki za kubeba abiria maarufu kama Bodaboda mkoani humo na kuwapa
ahadi nono za kuwainua kimaisha kupitia biashara hiyo.
Pamoja na mambo mengine, Makonda ameahidi kuwapa pikipiki bodaboda hao kwa marejesho ya shilingi 25,000 kwa wiki (sawa na shilingi 3,500) kwa siku na baadae kuwaachia wazimiliki wao.
Katika hatua nyingine, Makonda ameahidi kuwatengenezea mpango mzuri wa utakaowawezesha bodaboda hao kuingia katikati ya Jiji, tofauti na ilivyo sasa.
Ahadi ya Makonda kuwaruhusu Bodaboda kuingia Jijini ni ukamilifu wa ahadi ya Rais John Magufuli wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana.
Juzi, Meya mpya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita (Chadema) pia aliahidi kuhakikisha Bodaboda wanaweza kuingia mjini kwa utaratibu maalum.

Comments
Post a Comment