SERIKALI KUPITIA UPYA MIKATABA YA TRL
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (katikati)
akimsikiliza mmoja wa abiria anayetumia usafiri wa reli ya kati mkoani
Kigoma. Kushoto ni Mbunge wa Kigoma Mjini, Mhe. Zitto Kabwe na Kulia ni
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Saveli Maketta.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza
na wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), mkoani Kigoma.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili
kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Kapteni wa Meli ya MV Liemba ya
namna inavyoendeshwa, mkoani Kigoma.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa tatu
kulia), akipata ufafanuzi wa namna ya injini za Meli ya MV Liemba
zinavyofanya kazi wakati alipotembelea Meli hiyo mkoani Kigoma.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (mwenye
kizibao cha njano), akimsikiliza Kapteni Winton Mwassa (wa kwanza
kulia), kutoka Kampuni ya huduma za meli mkoani Kigoma mara baada ya
kutembelea na kuona hali ya MV Liemba.
……………………………………………………………………
Serikali
imeliagiza Shirika la Reli Tanzania (TRL), kupitia upya mikataba ya
ununuzi wa vichwa vya treni na mabehewa ili kubaini kasoro
zilizojitokeza na kuchukua hatua stahiki kabla ya maboresho ya reli ya
Tanga-Moshi-Arusha.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ametoa agizo
hilo mkoani Kigoma wakati akikagua miundombinu ya reli na kusissitiza
nia ya serikali kufufua reli ya kanda ya kaskazini ili kuimarisha huduma
ya uchukuzi katika mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha.
“Kama
Serikali tumewekeza vya kutosha katika TRL, hivyo tunawataka mfanye
biashara itakayolipa nasi tutahakikisha popote reli ilipo inatoa huduma
iliyokusudiwa na kuchangia kukuza uchumi wa nchi”, amesema Prof.
Mbarawa.
Prof.
Mbarawa amewataka wafanyakazi wa TRL kufanya kazi kwa bidii na uadilifu
ili kupata bidhaa na abiria wengi wa kuwasafirisha nchini kote.
Amesema
Serikali imedhamiria kuliongezea nguvu TRL ambapo baadhi ya mitambo
kutoka Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) itakabidhiwa kwa
shirika hilo hivyo kulitaka kuwa na mpango madhubuti wa kufanya biashara
na kurudisha hadhi ya usafiri wa reli hapa nchini.
“Fanyeni
bidii ili mpate mzigo wa kusafirisha kutoka Tanga kwenda Moshi na
Arusha ili kufikia lengo la kubeba mzigo wa tani milioni moja kwa
mwaka”, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.
Amezungumzia
umuhimu wa TRL kuafanya kazi kwa karibu na Mamlaka ya Usimamizi wa
Bandari nchini (TPA), ili kuongeza kasi ya huduma za uchukuzi nchini,
kuongeza fursa za ajira na kukuza pato la shirika na taifa.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TRL, Bw. Masanja Kadogosa amesema TRL
imejipanga kutafuta masoko ndani na nje ya nchi ili kuboresha huduma za
uchukuzi na kukuza pato lake.
Katika
hatua nyingine Prof. Mbarawa amekagua Meli ya MV Liemba na kuitaka
Mamlaka ya Usimamizi wa usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA),
kuhakikisha meli za MV Liemba na MV Mwongozo zinakaguliwa na kufanya
kazi inavyostahili katika Ziwa la Tanganyika.
“Tumieni
fursa ya kuwa karibu na nchi za maziwa makuu kufanya biashara ili meli
zetu zipate mzigo wa kutosha na kuongeza mapato kwa taifa”, amesisitiza
Prof. Mbarawa.
Prof.
Mbarawa ambaye yupo katika ziara mkoani Kigoma amewataka viongozi na
wafanyakazi wa taasisi zilizo chini ya wizara yake kufanya kazi kwa
kushirikiana ili kuibua fursa za kiuchumi katika ukanda wa magharibi na
hivyo kufufua miundombinu itakayochochea uchumi wa mikoa ya magharibi
mwa Tanzania yenye fursa nyingi za kibiashara.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Comments
Post a Comment