NAIBU WAZIRI MAMBO YA NDANI YA NCHI ATEMBELEA GEREZA LA BANGWE AFANYA MAZUNGUMZO NA WATUMISHI WA WIZARA MKOANI KIGOMA
Naibu
Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad
Masauni(katikati), akiongozana na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kigoma, SACP
Sabas Matolo(kushoto) na Mkuu wa Gereza la Bangwe,SSP Raphael
Mwanyingile(kulia), alipofika kutembelea gereza hilo katika ziara ya
kikazi mkoani Kigoma tarehe 31/3/2016.
Naibu
Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni,
akisaini kitabu cha wageni katika Gereza la Bangwe mkoani Kigoma, ambapo
baadae alisikiliza risala iliyohusu mambo mbalimbali, iliyoandaliwa
na wafungwa na mahabusu walioko katika gereza hilo na kuahidi
kushughulika changamoto zao.
Mkuu
wa Magereza Mkoa wa Kigoma, SACP Sabas Matolo, akisoma taarifa ya hali
ya magereza mkoani Kigoma mbele ya Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni.Naibu Waziri yuko mkoani Kigoma kwa
ziara ya kikazi.
Mmoja
wa Askari Magereza mkoa wa Kigoma, akizungumza wakati wa kipindi cha
maswali kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi
Hamad Masauni(hayupo pichani).Naibu Waziri alifanya mkutano na watumishi
wa Idara zote zilizopo chini ya Wizara, mkutano huo ulifanyika katika
ukumbi wa mikutano wa Shirika la Hifadhi ya Jamii(NSSF),mkoani Kigoma.
Watumishi
wa Idara zilizopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo
pichani), wakati wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Shirika la
Taifa la Hifadhi ya Jamii(NSSF), mjini Kigoma.
(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Comments
Post a Comment