Posts

Maskini Millen Magese..Ugonjwa Wake Waendelea Kumsumbua Afanyiwa Operation Mara 13...Ashindwa Kufanya Show Afrika Kusini

Image
Akiwa kitandani, Millen Magese anaongea kwa tabu baada ya kuzidiwa katikati ya onesho la Mercedes Benz Fashion Week, jijini Johannesburg, Afrika Kusini. Anawatoa hofu mashabiki wake kwasababu kilichotokea kiliwashtua. Akiwa kwenye kitanda cha hospitali, mwanamitindo huyo aliyewahi kuwa Miss Tanzania, anasema kiwango cha sukari kilikuwa kimeshuka kwa kiasi kikubwa kutokana na kupata maumivu makali na kutokwa damu nyingi kwa siku nane mfululizo. Millen akipewa huduma ya kwanza baada ya kuzidiwa Kutokana na tukio hilo, Millen ameshindwa kuendelea kushiriki kwenye show hiyo kubwa ya fashion. Maumivu anayoyazungumzia Millen si maumivu ya kawaida, ni maumivu makali. Mrembo huyo yupo kwenye vita vigumu na virefu dhidi ya ugonjwa uitwao Endometriosis. Ni ugonjwa ambao huhusisha seli zinazofaa kuwa ndani ya mji wa uzazi kuwa nje ya mji huo. Millen na wanawake wengine wanaosumbuliwa na ugonjwa huo hukabiliana na maumivu makali kila nyakati za siku zao za hedhi. N

Mike Tyson auza mjengo wake wa Las Vegas

Image
Mike Tyson. -UNGEPENDA kuishi kistaa na una kiasi cha Dola za Marekani Usd milioni 1.5 sawa na shilingi bilioni 3.3? Kama hivyo ndivyo, basi unaweza kununua mjengo wa kifahari wa mwanamasumbwi wa zamani wa Marekani, Mike Tyson. Staa huyo ameishi katika mjengo huo wenye futi za mraba 5,800 tangu mwaka 2008 ila sasa ameamua kuhamia kwenye mjengo mpya wenye vyumba vitano vya kulala na mabafu sita. Mbali na kuhama, mjengo huo bado hauko vibaya maana una sehemu tatu za kupashia moto nyumba (fireplaces), chumba cha kukutana na wahabari, sehemu ya kunywea mvinyo, eneo la kuchezea pool na maporomoko yaliyo sehemu ya kuingilia jumba hilo. Wakala wa Tyson, Ken Lowman, ameeleza kuwa eneo hilo lote limefanyiwa maboresho mapema mwaka huu na lipo katika muonekano mzuri japo linakosa kitu kimoja ambacho ni sehemu ya kufugia chui.

Mke, mume wazua timbwili studio za radio

Image
Wakiwa studio. Stori:  Dustan Shekidele, Wikienda Morogoro: Kioja! Mwanamke Betina Kimbe (25) na mumewe, Emmanuel Peter (30), wamezua timbwili ‘hevi’ ndani ya Studio za Radio Planet FM ya mjini hapa baada ya mke kukimbilia redioni akiomba achangiwe nauli ya kurudi kwao mkoani lringa akitaka kumtoroka muwewe kwa sababu alimweka ‘bondi’ wakati wa Mechi ya Simba na Mbeya City iliyochezwa jijini Dar wiki iliyopita. Betina alitinga na mwanaye wa mwaka mmoja ndani ya studio hizo akitokea nyumbani kwa baba mtoto wake huko Dumila kwa madai ya kuchoshwa na mumewe huyo huku akimshushia tuhuma lukuki. MKE ‘AMTUMBUA JIPU’ MUMEWE Akihojiwa na Mtangazaji Warda Makongwa wa Kipindi cha Mcharuko wa Pwani cha Radio Planet FM, Betina alisema aliamua ‘kumtumbua jipu’ mumewe huyo kufuatia mateso aliyokuwa akiyapata kila kukicha. “Nilipojifungua mtoto huyu, mume wangu alishinda klabuni, aliporudi nyumbani alikuja na mwanamke na kulala naye chumbani kwetu huku mimi akinilaza chini. “Nilip

BREAKING NEWS : ZITTO KABWE AFUNGUKA KUHUSU UTEUZI WA MAKONDA MTAKA NA SHIGELA

Image

MAGAZETI YA LEO JUMATATU TAREHE 14.03.2016

Image

BASI LA LEINA TOURS LA KAHAMA- DAR LAPATA AJALI,LATUMBUKIA MTARONI

Image
Basi la Leina Tours lililokuwa likitokea Kahama kwenda Dar es Salaam, limeacha njia na kutumbukia katika mtaro eneo la Kimara Bucha usiku wa kuamkia leo Idadi ya waliofariki haijafahamika ila waliojeruhiwa ni zaidi ya 30 na walikimbizwa Haospitali ya Mwananyamala na Muhimbili.

SAFARI ZA TRENI RELI YA KATI ZAANZA RASMI

Image
Huduma  ya usafiri  wa reli ya Kati iliyokuwa imesimama kwa takribani miezi miwili sasa imerejea kufuatia  kukamilika kwa ukarabati wa reli  hiyo katika eneo la kidete wilayani kilosa, mkoani Morogoro. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa  amesema  hayo baada ya kukagua na kuridhika na ukarabati uliofanywa katika maeneo ya Magulu, Munisagara, Mzaganza na kidete Wilayani Kilosa. “Hakikisheni mnailinda reli hii kwa manufaa yenu na ya Taifa, leo hii reli iko vizuri na treni ya kwanza kutoka Dar Es Salam  kwenda bara itapita na kumaliza changamoto ya usafiri iliyokuwa inawakabili wananchi wanaotumiia reli hii”.Amesema Profesa Mbarawa. Profesa Mbarawa amewataka wananchi wa maeneo ya Kilosa, Magulu, Munisagara, Mzaganza, Kidete, Godegodena Gulwe ambao maeneo yao yanakabiliwa na mafuriko ya mto Mkondoa kuacha Kilimo cha kuelekeza Maji kwenye reli bali washirikiane na Serikali kudhibiti maji hayo kwenda kwenye  hifadhi ya reli. Ames

WAZIRI MKUU MAJALIWA AZUNGUMZA NA WATUMISHI WA SERIKALI,VIONGOZI WA DINI NA WADAU WA MAENDELEO WA MKOA WA KAGERA

Image
 Baadhi ya watumishi wa serikali, viongozi wa dini na wadau wa maendeleo wa mkoa wa Kagera wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa ELCT mjini Bukoba akiwa katika ziara ya mkoa wa Kagera Machi 13, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watumishi wa serikali, Viongoze wa dini na wadau wa maendeleo wa mkoa wa Kagera kwenye  ukumbi wa ELCT mjini Bukoba Machi 13, 2016. Alikuwa katika siku ya kwanza ya ziara ya mkoa wa Kagera.

MBARAWA AFUNGUA RASMI SAFARI ZA TRENI RELI YA KATI

Image
Muonekano wa Sehemu ya Reli katika eneo la Kidete, Wilayani Kilosa, mara baada ya ukarabati kufuatia mvua kubwa zilizonyesha katika mikoa ya Iringa na Dodoma na kukata Mawasiliano kati ya Mkoa wa Morogoro na Dodoma. Kazi za ukarabati wa mwisho zikiendelea katika eneo la Kidete, Wilayani Kilosa, mara baada ya ukarabati kufuatia mvua kubwa zilizonyesha katika mikoa ya Iringa na Dodoma na kukata Mawasiliano kati ya Mkoa wa Morogoro na Dodoma. Treni ya Mizigo ikiwa tayari kuanza safari katika eneo la Kidete Wilayani Kilosa, kufuatia kukamilika kwa ukarabati wa eneo hilo, uliodumu kwa takriban miezi miwili na hivyo kurudisha mawasiliano ya reli kati ya Mkoa wa Morogoro na Dodoma. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Mhandisi wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO), Mhandisi Felix Nlalio, kuhusu namna ya kudhibiti mkondo wa maji katika mto mkondoa yasiathiri hifadhi ya reli. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na

JPM awathibitisha watendaji wakuu TRA, TAKUKURU

Image
Kamishna Mkuu wa TRA, Bw. Alphayo Kidata. Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Valentino Mlowola.

Mambo 5 yanayoleta uadui kwa wapenzi!

Image
Ni matumaini yangu kuwa msomaji wangu umzima wa afya njema na unaendelea na majukumu yako ya kujitafutia mkate wa kila siku. Namshukuru Mungu kwa kunijalia afya njema na kunipa tena nafasi ya kubadilishana mawazo kuhusu mambo yanayohusu uhusiano wa kimapenzi. Rafiki, bila shaka ipo wazi kwamba kila mmoja anapenda kuwa na mpenzi ambaye mbali na kumpenda kwa moyo wake wote, atapenda kumfanya awe kama ndugu, rafiki au zaidi ya hapo. Atakayekuwa tulizo la moyo, kivuli kwenye jua kali, maji jangwani na tiba kwenye maradhi. Hakuna anayeweza kuukabidhi moyo wake kwa mtu ambaye anajua fika kwamba atamtesa, atamnyanyasa, kumsababishia maumivu ya moyo, kuwa kero kwenye maisha yake na ‘kum-treat’ kama adui yake. Mapenzi ni sanaa kama zilivyo sanaa nyingine. Kwa mfano, ili kumudu kupiga gitaa au kinanda na kupata muziki mzuri, ni lazima ujifunze. Kwenye mapenzi ni hivyohivyo, ili kuishi vizuri na mpenzi wako ni lazima ujifunze. Usichoke kujifunza kila kukicha ili kuwa na u

Mjue Katibu Mkuu mpya wa Chadema!

Image
Katibu Mkuu mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Vicent Mashinji, akizungumza na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama hicho, usiku wa kuamkia leo mara baada ya kuchaguliwa, kwenye Mkutano Mkuu uliokuwa ukifanyika Jijini Mwanza. Dkt. Mashinji anaziba nafasi iliyoachwa wazi na Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dkt. Willbload Slaa. Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe, Makamu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar, Mh. Said Issa Mohamed pamoja na Mjumbe wa Mkutano Mkuu, Mh. Edward Lowassa wakifarilia kwa makini hotuba ya Katibu Mkuu mpya wa Chama hicho, Dkt. Vicent Mashinji (hayupo pichani). Sehemu ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CHADEMA wakishangilia baada ya kupatikana bila kwa Katibu Mkuu mpya, Dkt. Vicent Mashinji. WASIFU WA DK. VECENT MASHINJI Dk. Mashinji aliyezaliwa katika Wilaya ya Sengerema, alianza elimu ya msingi katika Shule ya Iligamba Januari 1981 hadi Oktoba 1987 na kisha kue

RAIS DKT MAGUFULI ATEUA WAKUU WA MIKOA LEO MACHI 13 2016

Image

Mastaa watumika kukamata vigogo wa unga!

Image
Video Queen, Agness Gerald ‘Masogange’ Stori: Sifael Paul, Ijumaa Dar es Salaam: Mjini hakukaliki! Mkakati wa Rais Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’ wa kupambana na biashara haramu ya dawa za kulevya ‘unga’ hapa nchini, umeiva ambapo uchunguzi wa gazeti hili umebaini kwamba unawatumia baadhi ya mastaa Bongo kuwakamata vigogo wanaojihusisha na biashara hiyo. WAANZIA KWA ‘MATEJA’ Uchunguzi huo wa wiki kadhaa jijini Dar ulibaini kwamba mara tu baada ya Rais Magufuli kutangaza kupambana na mfumo wa wauza unga, kikosi maalum cha Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Maofisa wa Uhamiaji waliingia kazini ‘fasta’ ambapo walianza kwa kuwatumia watu wa chini kabisa, kuanzia kwa watumiaji wa unga (mateja) ili kupata mwanga wa wapi wanapopata dawa hizo. Kupanta undani wa stori hii, nunua Gazeti la Ijumaa kwa Tsh. 500/=

Rais wa Vietnam atembelea Kampuni ya Simu ya Halotel jijini Dar es salaam

Image
Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tang San akizungumza na viongozi wa Kampuni ya Simu za mikononi kutoka nchini Vietnam ya Halotel inayofanya kazi hapa nchini Tanzania. Kampuni hiyo inatoa huduma ya simu Vijijini kwa gharama nafuu. Rais Truong Tang San anatarajiwa kumaliza ziara yake ya siku nne hapo kesho na kuelekea nchini Msumbiji kwa ajili ya ziara nchini humo. Viongozi mbalimbali walioambatana na Rais Truong Tang San, wakiwa pamoja na Balozi wa Vietnam, Mhe. Vothanh Nam (katikati) wakisikiliza kwa makini mazungumzo aliyokuwa yakiendelea kati ya Rais Tang San (hayupo pichani) na viongozi wa Kampuni ya simu ya Halotel Rais Truong Tang San akizindua Sanamu ya kiongozi wa zamani wa Vietnam iliyopo kwenye Kampuni ya Simu ya Halotel. Viongozi wa Halotel na Viongozi walioambatana na Rais Tang San (hayupo pichani) wakishangilia wakati uzinduzi ukiendelea  Rais Truong Tang San akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kampuni ya simu ya Halotel.Picha na R

Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe Keshawasili Jijini Mwanza Kwa Ajili ya Kikao cha Kumpata Mrithi wa Dr. Slaa

Image
Mwenyekiti wa chama cha Demokrsaia na Maendeleo (CHADEMA) akiwasili uwanja wa ndege jijini Mwanza.kwaajili ya mkutano wa  baraza kuu CHADEMA  ambao utamtangaza  Katibu  mkuu wa chama hicho kuchukua mikoba ya Dr. Slaa Mwenyekiti Freeman Mbowe akisalimiana na viongozi mbalimbali wa CHADEMA mkoa wa Mwanza waliofika kumlaki uwanja wa ndege Mwenyekiti wa baraza la wazee akiwasili uwanja wa ndege mwanza Mwenyekiti wa chadema akiwasili hotel ya Gold Crest ambako mkutano wa baraza kuu chadema utafanyika.Kulia ni afisa habari wa chadema Tumaini Makene Makamu katibu chadema Mh Salum Mwalimu akimpokea mwenyekiti   Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo akijadili jambo na makamu katibu Makamu katibu Mh Salum Mwalimu akimlaki kwa bashasha kubwa Makamu Mwenyekiti CHADEMA,Tanzania visiwani Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe Keshawasili Jijini Mwanza Kwa Ajili ya Kikao cha Kumpata Mrithi wa Dr. Slaa The Choice 2 hrs ago