Mambo 5 yanayoleta uadui kwa wapenzi!
Ni matumaini yangu kuwa msomaji wangu
umzima wa afya njema na unaendelea na majukumu yako ya kujitafutia mkate
wa kila siku. Namshukuru Mungu kwa kunijalia afya njema na kunipa tena
nafasi ya kubadilishana mawazo kuhusu mambo yanayohusu uhusiano wa
kimapenzi.
Rafiki, bila shaka ipo wazi kwamba kila
mmoja anapenda kuwa na mpenzi ambaye mbali na kumpenda kwa moyo wake
wote, atapenda kumfanya awe kama ndugu, rafiki au zaidi ya hapo.
Atakayekuwa tulizo la moyo, kivuli kwenye jua kali, maji jangwani na
tiba kwenye maradhi.
Hakuna anayeweza kuukabidhi moyo wake
kwa mtu ambaye anajua fika kwamba atamtesa, atamnyanyasa, kumsababishia
maumivu ya moyo, kuwa kero kwenye maisha yake na ‘kum-treat’ kama adui
yake.
Mapenzi ni sanaa kama zilivyo sanaa
nyingine. Kwa mfano, ili kumudu kupiga gitaa au kinanda na kupata muziki
mzuri, ni lazima ujifunze. Kwenye mapenzi ni hivyohivyo, ili kuishi
vizuri na mpenzi wako ni lazima ujifunze. Usichoke kujifunza kila
kukicha ili kuwa na uhusiano imara na ndoa inayoweza kudumu, jifunze
kupenda na kumuenzi umpendaye kwa moyo wako wote.
Labda nikuulize rafiki yangu, wewe
ulijifunzia wapi mapenzi? Shuleni, nyumbani, chuoni, mitaani au
mtandaoni? Yawezekana ukatafsiri mapenzi kwa maana ya tendo la ndoa
lakini hapa simaanishi hivyo, nazungumzia sanaa nzima ya mapenzi katika
tafsiri pana.
Ukweli ambao unashangaza, watu wengi
wana uelewa mdogo juu ya suala zima la maisha ya kimapenzi, jambo ambalo
linasababisha waishi kimazoea na kushindwa kufuata misingi halisi ya
jambo hilo nyeti katika maisha.
Matokeo yake, watu ambao awali wakati
wanaanzisha uhusiano wa kimapenzi walikuwa wanapendana na kugandana kama
ruba, huishia kuwa maadui na kuvunja uhusiano wao kwa majuto mengi.
Yaani mtu ambaye awali alikuwa kipenzi cha roho yako, anabadilika na
kuwa mwiba mkali maishani mwako.
NINI HUMFANYA MPENZI AWE ADUI?
Kwa kawaida, mnapoanzisha uhusiano wa kimapenzi kila mmoja humueleza au kumuonesha mwenzake nini anapenda na kipi hakimfurahishi. Kwa kuwa mapenzi ni suala la hiyari, mwenzio anapokukabidhi moyo wake anategemea kuwa utayafanya yale yanayomfurahisha na kuepuka yale yanayomuudhi kwa kadiri uwezavyo. Wataalam wa mapenzi wana msemo mmoja kwamba ‘penzi la kweli humsukuma mtu kumfurahisha mpenzi wake kwa kadiri ya uwezo wake na kamwe halitafuti visingizio’.

Usitafute visingizio linapokuja suala la
kumfurahisha mwenzio. Yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo yanaweza
kumgeuza mpenzi wako akawa adui yako.
1.UKISHINDWA KUMSIKILIZA
Mapenzi ni kusikilizana kwa kila jambo, hakuna nguzo muhimu kama kukubali kuupokea udhaifu wa mwenzako. Jenga mazoea ya kumsikiliza mpenzi wako kwa staha! Hata kama amekukwaza (lazima itatokea tu kwani yeye siyo malaika), tafuta namna nzuri ya kufikisha hisia zako kwake.

Kabla ya kumsikiliza usikimbilie
kumhukumu, kumsimanga, kumvunja moyo au kutoa kashfa ambazo zitamfanya
asononeke ndani ya moyo wake kwani vitu hivyo vikizidi, hupunguza hisia
za upendo na chuki huanza kujengeka taratibu.
Comments
Post a Comment