SAFARI ZA TRENI RELI YA KATI ZAANZA RASMI
Huduma
ya usafiri wa reli ya Kati iliyokuwa imesimama kwa takribani miezi
miwili sasa imerejea kufuatia kukamilika kwa ukarabati wa reli hiyo
katika eneo la kidete wilayani kilosa, mkoani Morogoro.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema
hayo baada ya kukagua na kuridhika na ukarabati uliofanywa katika
maeneo ya Magulu, Munisagara, Mzaganza na kidete Wilayani Kilosa.
“Hakikisheni
mnailinda reli hii kwa manufaa yenu na ya Taifa, leo hii reli iko
vizuri na treni ya kwanza kutoka Dar Es Salam kwenda bara itapita na
kumaliza changamoto ya usafiri iliyokuwa inawakabili wananchi
wanaotumiia reli hii”.Amesema Profesa Mbarawa.
Profesa
Mbarawa amewataka wananchi wa maeneo ya Kilosa, Magulu, Munisagara,
Mzaganza, Kidete, Godegodena Gulwe ambao maeneo yao yanakabiliwa na
mafuriko ya mto Mkondoa kuacha Kilimo cha kuelekeza Maji kwenye reli
bali washirikiane na Serikali kudhibiti maji hayo kwenda kwenye hifadhi
ya reli.
Amesema
Shirika la Reli Tanzania ( TRL) linaendelea kuhakikisha kuwa treni
inayopita kwenye reli ya Kati inapata mzigo mwingi wa kusafirisha
kutoka bandarini za Tanga na Dar Es Salaam kuelekea mikoa ya Mwanza,
Kigoma na Mpanda, hivyo wafanyabiashara watumie fursa hiyo ili kupunguza
mzigo unaosafirishwa kwa Nadia ya barabara.
Waziri
Profesa Mbarawa ameteembelea bwawa la Kidete linaloelezwa kuwa chanzo
cha mafuriko pindi linapojaa wakati wa mvua za Vuli na Masika katika
mikoa ya Dodoma na Iringa.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa John Henjewele amemhakikishia Waziri Profesa
Mbarawa kuwa ofisi yake itafuatilia kwa karibu malalamiko ya wananchi
wanaoishi karibu na reli ya Kati ili kuyapatia ufumbuzi na kuwataka
wananchi hao kuitumia fursa ya kuwa karibu na reli kunufaika kiuchumi.
Takribani
Shilingi millions 926 zimetumika katika ukarabati wa reli hiyo kufuatia
uharibifu uliotokea mwezi Januari na kukata Mawasiliano ya reli Kati
ya mikoa ya Dodoma na Morogoro na kusababisha Safari za treni kutoka
bara kuishia Dodoma.
Imetolewa na kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi,, Uchukuzi na Mawasiliano Serikalini.
Comments
Post a Comment