Maskini Millen Magese..Ugonjwa Wake Waendelea Kumsumbua Afanyiwa Operation Mara 13...Ashindwa Kufanya Show Afrika Kusini


Akiwa kitandani, Millen Magese anaongea kwa tabu baada ya kuzidiwa katikati ya onesho la Mercedes Benz Fashion Week, jijini Johannesburg, Afrika Kusini.


Anawatoa hofu mashabiki wake kwasababu kilichotokea kiliwashtua. Akiwa kwenye kitanda cha hospitali, mwanamitindo huyo aliyewahi kuwa Miss Tanzania, anasema kiwango cha sukari kilikuwa kimeshuka kwa kiasi kikubwa kutokana na kupata maumivu makali na kutokwa damu nyingi kwa siku nane mfululizo.

Millen akipewa huduma ya kwanza baada ya kuzidiwa

Kutokana na tukio hilo, Millen ameshindwa kuendelea kushiriki kwenye show hiyo kubwa ya fashion. Maumivu anayoyazungumzia Millen si maumivu ya kawaida, ni maumivu makali. Mrembo huyo yupo kwenye vita vigumu na virefu dhidi ya ugonjwa uitwao Endometriosis. Ni ugonjwa ambao huhusisha seli zinazofaa kuwa ndani ya mji wa uzazi kuwa nje ya mji huo.

Millen na wanawake wengine wanaosumbuliwa na ugonjwa huo hukabiliana na maumivu makali kila nyakati za siku zao za hedhi. Ni maumivu yasiyovumilika ambayo mara nyingi huishia kulazwa. Ugonjwa huo umemfanya afanyiwe upasuaji mara 13 hadi sasa. Kwa mwanamke mwingine, ugonjwa huo ni sababu tosha ya kuyakatia tamaa maisha, lakini si kwa Millen.

Mlimbwende huyu amekataa kukata tamaa. Ameamua kujitolea kuwa sauti ya wanawake wengine barani Afrika wanaosumbuliwa na ugonjwa huo. Amejitokeza bila kujali maumivu ya kimwili na moyo yanayotokana na ugonjwa huo uliomfanya akose fursa ya kupata mtoto na kuwa mama kama wanawake wengine. Millen anapigana vita ngumu na haoneshi kuweka silaha chini. Anapigana kutafuta tiba ya ugonjwa huu ambao unamuathiri kihisia na sasa kiuchumi pia.


Hapo mwanzo, aliweza kufanya show kuanzia 28-38 kwenye fashion weeks kubwa lakini leo huweza kufanya 4 tu. Ugonjwa huo umemnyong’onyeza kimwili lakini haimaanishi kuwa umemuondolea nia ya kuendelea kupambana kutafuta suluhu.

Ndio maana amezindua kampeni mpya aliyoipa jina #13IsEnoughIspeakOut #FindACure4Endo.

“Today is the 13th of March . We are officially kicking of the “13Is Enough ,I speak Out “Campaign for Many Faces Of Endo. 13 Is Enough campaign is our many faces of Endo massage this year, where I decided to use my Endo story and experience from the multiple surgeries I have gone through, to create more attention but more action towards finding a cure for Endometriosis,” ameandika kwenye Instagram.

“There other women who have gone through more surgeries than me because it’s true Cure for endometriosis is yet to be found . I /we can’t continue going through this pain. It’s a nightmare. I /we can’t do this alone . So I personally as Millen Magese asking all of you to help participate on this Endo challenge (info to follow) and nominate 3 people, ask your friends too. I believe #cureIsPossible help me to repost and tag your friends . Thank you all for your support.”

Ni kweli, operesheni 13 zimetosha. Tumpe moyo na kumuombea Millen ili apate nguvu ya kupambana kwenye vita hii ngumu. Tiba ya Endometriosis ipatikane sasa, imetosha.
HATUNABUDI KUUNGANA NA KUZIDI KUMUOMBEA NDUGU YETU NA DADA YETU AREJEE KATIKA HALI YAKE YA KAWAIDA.

Comments

Popular posts from this blog