MBARAWA AFUNGUA RASMI SAFARI ZA TRENI RELI YA KATI
Muonekano
wa Sehemu ya Reli katika eneo la Kidete, Wilayani Kilosa, mara baada ya
ukarabati kufuatia mvua kubwa zilizonyesha katika mikoa ya Iringa na
Dodoma na kukata Mawasiliano kati ya Mkoa wa Morogoro na Dodoma.
Kazi
za ukarabati wa mwisho zikiendelea katika eneo la Kidete, Wilayani
Kilosa, mara baada ya ukarabati kufuatia mvua kubwa zilizonyesha katika
mikoa ya Iringa na Dodoma na kukata Mawasiliano kati ya Mkoa wa Morogoro
na Dodoma.
Treni
ya Mizigo ikiwa tayari kuanza safari katika eneo la Kidete Wilayani
Kilosa, kufuatia kukamilika kwa ukarabati wa eneo hilo, uliodumu kwa
takriban miezi miwili na hivyo kurudisha mawasiliano ya reli kati ya
Mkoa wa Morogoro na Dodoma.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akitoa
maelekezo kwa Mhandisi wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO),
Mhandisi Felix Nlalio, kuhusu namna ya kudhibiti mkondo wa maji katika
mto mkondoa yasiathiri hifadhi ya reli.
Comments
Post a Comment