Posts

SERIKALI YAMKABIDHI CHEKA CHETI CHA PONGEZI KUTOKANA NA USHINDI WAKE.

Image
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye(kulia) akiwa ameambatana na Bondia Francis Cheka (wapili kulia) alipotembelea Wizarani leo jijini Dar es Salaam na Serikali imemkabidhi  Cheti cha pongezi. Kushoto ni Rais wa Chama cha ngumi Tanzania (TPBO) Yassin Adballah (Ustadh). Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye(katikati) akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa zoezi la kumkabidhi Cheti cha pongezi kutokana na ushindi Bondia Francis Cheka (kushoto) leo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Makoye Alex Nkenyenge. Bondia Francis Cheka akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)  wakati wa zoezi la kupokea Cheti cha pongezi kutoka kwa Serikali leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye,Rais wa Chama cha ngumi Tanzania (TPBO) Yassin Adballah (Ustadh) na Meneja wa Bondia huyo Chifu Ndambi

Walimu 8 Mbaroni Mwanza kwa Kujihusisha na Mapenzi na Wanafunzi

Image
Walimu hao wakipandishwa kwenye gari la polisi ili kupelekwa kituoni. WALIMU wanane wa Shule ya Sekondari Mihama, Kata ya Kitangili, Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza, wamesimamishwa kazi, watano kati yao wakishikiliwa na polisi kwa tuhuma za kufanya mapenzi na wanafunzi. Pia, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo aliyetembelea shule hiyo jana, amevunja bodi ya shule hiyo baada ya kubainika kutofanya kikao hata kimoja tangu ilipoteuliwa Aprili 24, 2013. Wakitiwa pingu. Pamoja na Mkuu wa Shule, Joseph Malifedha, walimu wengine waliotiwa mbaroni jana ni Rodrick Uroki, Denis Sanga, Edmund Boaz, Steven Samuel. Walimu watatu waliokuwa wakifundisha shuleni hapo, lakini wakahamishwa na hivi sasa wanasakwa na polisi kwa tuhuma hizo ni Joseph Lamongi na Joeza Mzava waliohamia Sekondari ya Sangabuye pamoja na Abdallah Mtelwe aliyehamia Tanga. Malifedha anadaiwa kuwachangisha fedha wanafunzi wa kidato cha kwanza na cha tatu kwa ajili ya picha za kuweka kwenye vitambuli

Jide ndoa tena

Image
  Mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ au Jide. Na Mwandishi Wetu,  Risasi Jumamosi Dar es Salaam: Siku chache baada ya kupewa talaka na aliyekuwa mumewe, mtangazaji Gardner G. Habash ‘Captain’, mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva anayekuja na ujio mpya alioubatiza jina la Naamka Tena, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ au Jide amedaiwa kupata mwanaume mwingine ambaye yupo kwenye mikakati kabambe ya kumuoa, Risasi Jumamosi lina ubuyu kamili. Jide ambaye amekuwa kimya kimuziki kwa zaidi ya miaka miwili, Februari mwaka huu alipewa talaka katika Mahakama ya Manzese-Sinza jijini Dar baada ya mvutano uliodumu kwa muda mrefu tangu wawili hao washindwe kuishi pamoja. Kwa mujibu wa chanzo makini, Jide alimpata mwenza muda mrefu tangu walipomwagana na Gardner lakini mipango ya ndoa ikashindwa kwenda haraka kwa sababu hakuwa amepewa talaka hiyo aliyoidai mahakamani. “Mbona Jide kitambo tu alishapata mtu sema alikuwa hawezi kufanya mambo ya ndoa kwani

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFANYA ZIARA ITILIMA MKOANI SIMIYU

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akikagua ujenzi wa Maabara katika shule ya Sekondari ya Budalabugija wilayani Itilima akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu Machi 4, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu Machi 4, 2016. (P:icha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua bwawa la umwagiliaji na maji ya kunywa la kijiji cha Mkoma na Mwalushu wilayani Itilima akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu, Machi 4, 2016. (Picha na ofisi ya  Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwsalimia wananchi  baada ya kukagua bwawa la maji ya kunywa na umwagiliaji la vijiji vya Mkomana Mwalushu wilayani Itilima Machi 4, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwsalimia wananchi  baada ya kukagua bwawa la maji ya kunywa na umwagiliaji la vijiji vya Mkomana Mwalushu wilayani Itilima Machi 4, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri M

Waziri wa zamani Rwegasira afariki dunia

Image
Waziri zamani wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Joseph Rwegasira. Taarifa iliyotolewa jana na Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa ilisema Balozi Rwegasira alifariki jana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Taarifa hiyo ilieleza mwili wa marehemu Rwegasira utaagwa leo katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Peter, Oysterbay saa 8.00 mchana kabla ya kusafirishwa keshokutwa kwenda Bukoba, Kagera kwa mazishi. Rwegasira aliyezaliwa Machi 21, 1935, aliwahi kuwa mwenyekiti wa jumuiya ya vyama vya wafanyakazi (Juwata), Mkuu wa Mkoa wa kwanza wa Pwani na baadaye Balozi wa Tanzania nchini Zambia. Pia, aliwahi kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara na baadaye Waziri wa Kazi kabla ya kuhitimisha kwa uwaziri wa mambo ya nje kati ya mwaka 1993 hadi 1995 chini ya Rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi.

HATARI SANA! Hili Ndio Dau la Kupata Huduma ya Mrembo Huyu Mwenye Shepu Ya Maana!

Image
Gift Stanford ‘Gigy Money’. M UUZA nyago kwenye video mbalimbali za Kibongo, Gift Stanford ‘Gigy Money’ kwa mara ya kwanza amefungukia ishu yake ya malipo kupitia video za Bongo Fleva anazofanya kama ‘Video Queen’ kuwa kwa sasa bila shilingi milioni moja humpati. Akichonga na   Showbiz   Gigy alisema kuwa, kwa sasa Muziki wa Bongo Fleva umebadilika na hata video zake zina viwango vikubwa tofauti na kipindi cha nyuma ambapo hata makampuni ya video yalikuwa machache hivyo kwa wale mastaa yupo tayari kuwafanyia kuanzia laki tano lakini kwa wale ambao hawana majina sana ‘chipukizi’ bila milioni moja hawampati. “Kwa kawaida video nyingi huwa naanzia laki tano lakini kuna video ambazo kiukweli kabisa bila milioni moja siwezi kufanya,” alisema Gigy. Gigy ametokelezea kwenye video kibao za Bongo Fleva ambazo ni Siachani Nawe ya Barakah Da Prince, Get High ya Godzilla, Shika Adabu Yako ya Nay wa Mitego na nyingine nyingi.

MKUU WA MAJESHI AONGOZA KUWAAGA MAOFISA MAJENERALI 16 WA JWTZ WALIOSTAAFU

Image
Mnadhimu Mkuu mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Samuel Ndomba (kwenye gari kushoto) na Mkuu wa Vikosi vya Kulinda Amani Umoja wa Mataifa, Luteni Jenerali mstaafu, Paul Ignas Meela wakitoa heshima katika hafla ya kuagwa iliyofanyika Viwanja vya Twalipo Mgulani Dar es Salaam leo mchana. Maofisa Majenerali 16 waliostaafu Utumishi Jeshini waliagwa. Mkuu wa Majeshi, Jenerali, Davis Mwamunyange (kushoto), akisalimiana na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi hilo mstaafu, Luteni Jenerali, Samuel Ndomba. Mkuu wa Majeshi, Jenerali, Davis Mwamunyange (kushoto), akisalimiana na kumpongeza Mkuu wa Vikosi vya Kulinda Amani Umoja wa Mataifa, Luteni Jenerali mstaafu, Paul Ignas Meela katika hafla hiyo. Brigedia Jenerali mstaafu, Msangi (kulia mbele), akikagua gwaride maalumu waliloandaliwa maofisa hao wastafu wakati wakiagwa rasmi baada ya kumaliza utumishi wao jeshini. Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), mstaafu Meja Jenerali, Raphael Muhuga, a

MADHARA YA MATUMIZI YA MIRUNGI KIAFYA

Image
   Mtumiaji wa mirungi yupo katika hatari ya kupata vidonda vya tumbo. - Kupungukiwa msukumo wa kufanya tendo la ndoa (low sex drive) na pia kuwahi kumaliza haraka na kutoweza kudumu kwenye tendo la ndoa kwa muda mrefu. 2. Ukosefu wa haja kubwa (constipation) 3. Utumiaji wa muda mrefu husababisha ini kushindwa kufanya kazi, pia meno kubadilika rangi, kudhoofika, fizi kuuma na harufu mbaya mdomoni. 4. Upungufu wa usingizi. 5. Humpelekea mlaji kutawaliwa nayo. (addiction) 6. Madhara ambayo bado kinamama walaji Mirungi hawajagundua ni kwamba mtoto anayezaliwa na mama mlaji Mirungi mara nyingi hukataa kunyonya titi la mama yake kwa sababu ladha ya maziwa inabadilika kwa ajili ya utumiaji wa madawa (pesticides) unaotumiwa na wakulima wa Mirungi kama inavyoeleza utafiti uliofanyika na Chuo Kikuu Cha Aden (Aden University). 7. Utafiti mwengine kule Ethiopia unatueleza ya kuwa mtoto wa mama mwenye kula Mirungi kwa wingi huwa hana uzito wa kawaida wakati wa kuz

Rais Magufuli, Kenyatta waweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya Arusha

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa Tengeru nje kidogo ya Jiji la Arusha mara baada ya kuwasili kwa ajili ya Uzinduzi rasmi wa Barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji la Arusha. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kabla ya uzinduzi rasmi wa Barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji la Arusha. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kabla ya uzinduzi rasmi wa Barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji la Arusha. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais wa Uganda Yoweri Museveni kabla ya uzinduzi rasmi wa Barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 uliofanyika Tengeru nje kidogo ya jiji la A