SERIKALI YAMKABIDHI CHEKA CHETI CHA PONGEZI KUTOKANA NA USHINDI WAKE.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye(kulia)
akiwa ameambatana na Bondia Francis Cheka (wapili kulia) alipotembelea
Wizarani leo jijini Dar es Salaam na Serikali imemkabidhi Cheti cha
pongezi. Kushoto ni Rais wa Chama cha ngumi Tanzania (TPBO) Yassin
Adballah (Ustadh).
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye(katikati)
akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa zoezi la kumkabidhi Cheti
cha pongezi kutokana na ushindi Bondia Francis Cheka (kushoto) leo
jijini Dar es Salaam.Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo
Makoye Alex Nkenyenge.
Bondia
Francis Cheka akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)
wakati wa zoezi la kupokea Cheti cha pongezi kutoka kwa Serikali leo
jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye,Rais wa Chama cha ngumi Tanzania
(TPBO) Yassin Adballah (Ustadh) na Meneja wa Bondia huyo Chifu Ndambile
Juma Ntinginya.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (wapili
kushoto) akimsikiliza kwa makini Katibu Mtendaji wa BMT Mohamed Kiganja
(aliyesimama) akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa zoezi la
kumkabidhi Cheti cha pongezi Bondia Francis Cheka (kushoto) kutokana na
ushindi wa Mkanda wa Uzito wa Super Middle wa Mabara wa WBF leo jijini
Dar es Salaam. Wapili kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Makoye
Alex Nkenyenge
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia)
akimkabidhi Cheti cha pongezi Bondia Francis Cheka kutokana na ushindi
alioupata katika pambano baina yake na Bondia Mserbia anayeishi
Uingereza Geard Ajetovic (hayupo pichani) leo jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia)
na Bondi Francis Cheka wakiwaonyesha waandishi wa Habari Mkanda wa uzito
wa Super Middle wa Mabara ambao Cheka ameunyakuwa baada ya kushinda
pambano la tarehe 27 Februari baina yake na Bondia Mserbia anayeishi
Uingereza Geard Ajetovic (hayupo pichani) leo jijini Dar es
Salaam.Kushoto ni Meneja wa Bondia huyo Chifu Ndambile Juma Ntinginya.
Picha na Frank Shija, WHUSM
Comments
Post a Comment