Walimu 8 Mbaroni Mwanza kwa Kujihusisha na Mapenzi na Wanafunzi
WALIMU wanane wa Shule ya
Sekondari Mihama, Kata ya Kitangili, Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza,
wamesimamishwa kazi, watano kati yao wakishikiliwa na polisi kwa tuhuma
za kufanya mapenzi na wanafunzi.
Pia, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa
Mulongo aliyetembelea shule hiyo jana, amevunja bodi ya shule hiyo baada
ya kubainika kutofanya kikao hata kimoja tangu ilipoteuliwa Aprili 24,
2013.
Pamoja na Mkuu wa Shule, Joseph
Malifedha, walimu wengine waliotiwa mbaroni jana ni Rodrick Uroki, Denis
Sanga, Edmund Boaz, Steven Samuel.
Walimu watatu waliokuwa wakifundisha
shuleni hapo, lakini wakahamishwa na hivi sasa wanasakwa na polisi kwa
tuhuma hizo ni Joseph Lamongi na Joeza Mzava waliohamia Sekondari ya
Sangabuye pamoja na Abdallah Mtelwe aliyehamia Tanga.
Malifedha anadaiwa kuwachangisha fedha
wanafunzi wa kidato cha kwanza na cha tatu kwa ajili ya picha za kuweka
kwenye vitambulisho (passport size).
Akitangaza uamuzi huo, Mulongo alisema
tume maalumu ya uchunguzi iliyoundwa Januari 27, kuchunguza tuhuma
dhidi ya walimu hao kujihusisha na mapenzi na wanafunzi imebaini ukweli
baada ya kuwahoji wanafunzi kadhaa.
“Ni fedheha na haivumiliki kuona
walimu wakifanya mapenzi na wanafunzi wao. OCD wakamate walimu wote na
uanze uchunguzi mara moja na kukusanya ushahidi utakaowezesha wahusika
kufikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake,” aliagiza Mulongo.
Amri hiyo ilitekelezwa mara moja kwa walimu hao kuwekwa chini ya ulinzi.
Pia, alimwagiza Ofisa Elimu Mkoa wa
Mwanza, Khamisi Maulid kuangalia uwezekano wa kuwahamishia shule
nyingine wanafunzi waliodhulumiwa kingono na walimu wao ili kuwaepusha
na matatizo ya kisaikolojia.
Maulidi alisema wanafunzi walioathirika zaidi ni wale wa kidato cha nne.
Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania
(CWT), Mkoa wa Mwanza, Said Mselem alisema kitendo hicho kimeifedhehesha
taaluma ya ualimu na kuahidi kuwa ofisi yake itatanua wigo wa uchunguzi
hadi kwenye shule nyingine
Comments
Post a Comment