Waziri wa zamani Rwegasira afariki dunia

Waziri
Waziri zamani wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Joseph Rwegasira.
Taarifa iliyotolewa jana na Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa ilisema Balozi Rwegasira alifariki jana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Taarifa hiyo ilieleza mwili wa marehemu Rwegasira utaagwa leo katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Peter, Oysterbay saa 8.00 mchana kabla ya kusafirishwa keshokutwa kwenda Bukoba, Kagera kwa mazishi.
Rwegasira aliyezaliwa Machi 21, 1935, aliwahi kuwa mwenyekiti wa jumuiya ya vyama vya wafanyakazi (Juwata), Mkuu wa Mkoa wa kwanza wa Pwani na baadaye Balozi wa Tanzania nchini Zambia.
Pia, aliwahi kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara na baadaye Waziri wa Kazi kabla ya kuhitimisha kwa uwaziri wa mambo ya nje kati ya mwaka 1993 hadi 1995 chini ya Rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi.

Comments

Popular posts from this blog