UN Yalaani Korea Kaskazini Kurusha Kombora la Masafa Marefu
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limelaani hatua ya Korea Kaskazini kulipua Kombora la masafa marefu. Katika taarifa iliyotolewa baada kikao cha dharura mjini New York imesema baraza limekubaliana kuiwekea nchini hiyo vikwazo vya kiuchumi mapema iwezekanavyo,lakini pia baraza hilo limeilaumu Korea Kaskazini kwa kukiuka maazimio ikiwa ni pamoja na hatua yake ya kulipua bomu la nyuklia mwezi January. Kauli hizo za kuilaani hatua hiyo Korea Kaskazini zimetowa maeneo mbali mbali duniani pamoja na kulaumiwa na dunia Korea Kaskani yenyewe imesema imelipua kombora hilo ili kutuma mitambo ya satellite angani,jambo linalopingwa na mahasimu wake kuwa hiyo ni danganya toto kwani ina nia ya kujaribu kombora angani. Akitoa taarifa ya kulaani hatua hiyo Rais wa Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa ambaye pia ni Balozi wa Venezuela Rafael Ramirez Carreno amesema wanachama wamekubaliana kulaani kile alichosema ukiukwaji Korea Kaskazini wa azimio la Umoja wa Mataifa. Rafael Ra