Posts

MTOTO WA MIAKA 9 ATAKA KUWEKA REKODI YA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO KWA KUTUMIA NJIA NGUMU

Image
Mzazi wa mtoto Idda Baitwa,Bw Respcius Baitwa akifanya maandalizi na mwanae ya kuanza safari  ya kuweka rekodi ya kupanda Mlima Kilimanjaro Mtoto Idda Baitwa akiwa na baba yake mzazi Bw Respcius Baitwa pamoja na ndugu zake wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi kabla ya kuanza safari  ya kuweka rekodi ya kupanda Mlima Kilimanjaro. Mtoto Idda Baitwa akijiandikisha katika lango la Umbwe la kupanda mlima Kilimanjaro kabla ya kuanza safari ya kupanda mlima huo.nyuma yake ni Bw Respicius Baitwa akshuhudia. Safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa mtoto Idda Baitwa ikaanza. Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini. MTOTO wa miaka tisa(9) Idda Baitwa ameanza safari  ya kuweka rekodi ya kupanda Mlima Kilimanjaro akiwa na umri mdogo zaidi huku akitumia njia ya Umbwe ambayo inaaminika kuwa ngumu zaidi kwa watalii wakati wa kupanda mlima huo. Msichana huyo mwanafunzi wa darasa la nne, katika shule ya msingi Mnazi iliyoko M...

Mkuu wa Majeshi ya ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange katika sherehe za miaka 10 ya chuo cha JKT mapinga

Image
  Mkuu wa Majeshi ya ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange akiwa anakata utepe kuashiria uzinduzi rasimi wa uwanja  uliopewa jina la Jenerali Davisi Mwamunyange  ambao utatumika kwa shughuli mabalimbali ikiwemo gwaride kulia ni Mkuu wa JKT Meja Jenerali Raphael Muhuga na kushoto ni Mkuu wa chuo cha JKT Mapinga Meja Aristides Rutta sherehe hizo ziliambatana na kutimiza miaka kumi ya kuanzishwa kwa chuo cha JKT Mapinga  kilichopo jijini Dar es salaam  Mkuu wa majeshi ya ulinzi Jenerali Devisi Mwamunyange akikagua gwaride h lililo andaliwa wakati wa sherehe za kutimiza miaka kumi ya kuanzishwa chuo cha jkt Mapinga kilichopo jijini Dar es salaam   Mkuu wa majeshi ya ulinzi Jenerali  Devisi Mwamunyange akiwa anangalia bwawa lakufugia samaki ambalo limejengwa na chuo cha jkt mapinga jenerali Mwamunyange alikuwa mgeni rasimi katika kuadhimisha miaka kumi ya kuanzishwa kwa chuo cha jkt mapinga  Jengo la utawala l...

ANGALIA PICHA SAFARI YA MWISHO YA MWANAFUNZI DANIEL LEMA ALIYECHOMWA MOTO KWA KUTUMIWA KUWA MWIZI

Image
Mwili wa Daniel Lema ukiagwa na baadhi ya wanachuo pamoja na raia waliojitokeza kuhudhuria ibada ya kuuaga mwili wa marehemu mapema asubuhi ya leo katika hospitali ya rufaa mkoani iringa. Mwanafunzi (LEMA) aliyejeruhiwa kwa moto   Baadhi ya raia walijitokeza kumuaga Lema katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya rufaa mkoani Iringa. LEMA Aliyekua akisoma mwaka wa 4 kozi ya sheria katika chuo kikuu kishiriki cha Mt.Augustino Tawi la Iringa (Ruaha University College-RUCO), mwanzoni mwa wiki hii ameshambuliwa kwa kuunguzwa na moto akidhaniwa ni mwizi. Mnamo tarehe 24.06.2014 mwanafunzi huyo alikua ametoka kuangalia michuano ya kombe la dunia na akiwa amelewa akawa anatafuta chakula cha jioni na ilikua majira ya saa 5 Usiku, Mwanafunzi huyo aliingia kwenye mgahawa ambao biashara ilikua imefungwa kwa muda huo lakini ndani kulikuwapo na binti ambaye alianza kupiga kelele kwa kudhani alikua mwizi. Na kw...

ANGALIA PICHA APIGWA NYUNDO YA KICHWA NA MKEWE

Image
Faustina Selali,akiwa katika maumivu makali baada ya kushambuliwa na mumewe. Inasikitisha sana jamani. Faustina Selali, 38, mkazi wa Mgeta, Mvomero mkoani hapa, yupo kwenye mateso makali akijiuguza kutokana na kipigo alichopata kutoka kwa mumewe wa ndoa aliyemtaja kwa jina la Lugasiani John Miasiku, kisa kikiwa ni mumewe huyo kutaka kuoa mke wa pili. Mwanamke huyo amelazwa katika wodi nambi 3 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, ambapo amesimulia kisa chote mbele ya kamera ya Uwazi. KISA CHENYEWE Akizungumza kwa tabu, Faustina alisema tukio hilo lililobadilisha historia ya maisha yake na kumwachia machungu moyoni mwake, lilitokea Juni 25, mwaka huu majira ya saa nne usiku ndani ya nyumba yao. “Mimi na mume wangu tumeishi kwenye ndoa kwa muda wa miaka 20 na kufanikiwa kupata watoto watano. Kwa kipindi kirefu nilihisi ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamke mwingine, wakati naendelea kumchunguza, mume wangu akaniambia anataka kuoa mke wa pili,” ...

ANGALIA PICHA MTOTO MWINGINE AFANYIWA UKATILI WA KUTISHA NA MAMA YAKE MKUBWA MORO

Image
                           M toto Mwajuma Athuman[6] aliyeokotwa na wanajeshi kambi baada ya kukimbia mateso ukatili anaodai kufanyiwa na mama yake mkubwa Bi,Ashura Omar amefichua siri nzito mbele ya Afisa mtendaji wa kata ya Kingolwira                                                    Mwenyekiti wa Mtaa Tank la Maji  ka ta ya  Kingolwira Bw Mohamed Said akiwa na mtoto huyo Mtoto huyo akiwa na Makovu aliyodai yametokana na kipigo toka kwa mama yake mkubwa Mtoto huyo hawezi kutembea baada ya mguu wa kushoto uliokuwa na kidonda kuvimba,akidai kidonda hicho pia kimetokana na kichapo toka kwa mama yake huyo. Mwenyeki  akimbeba mtoto huyo kueleka ofisi ya Afisa Mtendaji Mama mkubwa wa mtoto huyo baada ya kuona kamera za Mtandao huu zikimmulika alifich...

AVEVA NDIYE RAIS MPYA SIMBA SC...ASHINDA KWA KISHINDO KIKUBWA

Image
Amin Bakhresa  akitangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Simba SC. Evance Aveva akishukuru baada ya kutangazwa kuwa Rais mpya wa klabu ya Simba na kuchukua mikoba ya Ismail Aden Rage, aliyemaliza muda wake wa miaka minne. Rais mpya wa Simba, Aveva akipongeza Bakhresa kwa kazi nzuri ya kusimamia shughuli nzima ya uchaguzi, ambao ulifanyika pasipo bugudha yoyote ile katika Bwalo la Polisi Oysterbay jana  MIKAKATI IMEANZA! Rais mpya wa Simba Aveva (mwenye suti, kushoto), akisalimiana na Katibu Mkuu wa klabu hiyo Ezekiel Kamwaga huku Makamu Katibu Mkuu Phillip Stanley (mwenye shati jekundu) akiwasikiliza mipango yao.   Rais Aveva, akifurahia jambo na Makamu Mwenyekiti uongozi uliomaliza muda wake, Joseph Itang'are 'Mzee Kines' baada ya shughuli nzima ya uchaguzi kumalizika kwenye Ukumbi wa Bwalo la Polisi Oysterbay. (PICHA NA RICHARD BUKOS/GPL)

ANGALIA PICHA ALICHOFANYIWA BABA MWENYE NYUMBA HATOSAHAU MAISHANI.

Image
  Jamaa aliyetajwa kwa jina moja la Lugali  akihusishwa  kuchepuka na mke wa mpangaji wake, akiwa amenaswa kwenye gesti moja maeneo ya Buguruni, Dar. Vunja jungu! Saa kadhaa kabla ya kuanza kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, jamaa aliyetajwa kwa jina moja la Lugali ameibua sekeseke kwenye nyumba ya kulala wageni (gesti), kisa kikidaiwa ni mchepuko akihusishwa na mke wa mpangaji wake, Ijumaa Wikienda lina kisa na mkasa. Wakati ikirandaranda mitaani kutega mingo, Timu ya Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers ilipokea mchongo kuwa kuna timbwili kwenye gesti moja maeneo ya Buguruni, Dar ambapo walifika eneo la tukio na kushuhudia kasheshe hilo la aina yake. Ndugu wa mume waliyefumania wakimdhibiti baba mwenye nyumba huyo.  OFM ilimshuhudia mzee huyo akichomolewa kutoka chumbani huku damu zikimvuja baada ya kula kichapo kutoka kwa jamaa na ndugu wa mwanaume aliyedai kuwa jamaa huyo alikuwa anamsumbua mkewe. ...

Dk Salim afichua siri ya JK na Tume ya Warioba

Image
Dar es Salaam. Waziri Mkuu Mstaafu, Dk Salim Ahmed Salim amesema hakutarajia kusikia kauli za Rais Jakaya Kikwete alizozitoa bungeni kukosoa Rasimu Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa sababu walikuwa wanampa taarifa kwa kila hatua waliyokuwa wanafikia kabla ya kutoa rasimu hiyo.                Dk Salim alitoa kauli hiyo katika mahojiano maalumu na gazeti hili nyumbani kwake Masaki, Dar es Salaam wiki iliyopita. “Hatukutarajia kama hali ingefikia hatua iliyofikia,” alisema Dk Salim na kuongeza: “Lakini Rais ana uamuzi wake na anazingatia mambo mengine mengi.” Akilihutubia Bunge maalumu la Katiba Machi 21, mwaka huu Rais Kikwete aligusia mambo saba ya msingi yaliyomo katika Rasimu ya Katiba na kutaka yatazamwe kwa kina, huku akibainisha kuwa mengine hayawezekani kutekelezeka. Miongoni mwa mambo hayo ni muundo wa Serikali. Alipinga waziwazi pendekezo la serikali tatu lililopendekezwa na Tume na ...

RED CARPET YA TUZO ZA BET 2014

Image
Diamond Platnumz akihojiwa na Karrueche Tran ambaye ni mpenzi wa Chris Brown kwenye Red Carpet. Amber Rose. T.I. Gabrielle Union. Ne-Yo akipozi kwenye Red Carpet. Ashanti. Nelly. Claudia Jordan. John Legend. Eva Marcille. Lionel Richie. Jennifer Freeman