ANGALIA PICHA APIGWA NYUNDO YA KICHWA NA MKEWE
Faustina Selali,akiwa katika maumivu makali baada ya kushambuliwa na mumewe.
Inasikitisha sana jamani. Faustina Selali, 38, mkazi wa Mgeta, Mvomero mkoani hapa, yupo kwenye mateso makali akijiuguza kutokana na kipigo alichopata kutoka kwa mumewe wa ndoa aliyemtaja kwa jina la Lugasiani John Miasiku, kisa kikiwa ni mumewe huyo kutaka kuoa mke wa pili.
Mwanamke
huyo amelazwa katika wodi nambi 3 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Morogoro, ambapo amesimulia kisa chote mbele ya kamera ya Uwazi.
KISA CHENYEWE
Akizungumza
kwa tabu, Faustina alisema tukio hilo lililobadilisha historia ya
maisha yake na kumwachia machungu moyoni mwake, lilitokea Juni 25, mwaka
huu majira ya saa nne usiku ndani ya nyumba yao.
“Mimi
na mume wangu tumeishi kwenye ndoa kwa muda wa miaka 20 na kufanikiwa
kupata watoto watano. Kwa kipindi kirefu nilihisi ana uhusiano wa
kimapenzi na mwanamke mwingine, wakati naendelea kumchunguza, mume wangu
akaniambia anataka kuoa mke wa pili,” alisema Faustina kwa uchungu na
kuongeza:“Nikamhoji
mume wangu, dini yetu hairuhusu jambo hilo na zaidi ya yote
anachotafuta kwa huyo mke wa pili ni kitu gani wakati tayari mimi
nimeshamzalia watoto watano na bado naendelea kuzaa?
“Hakuwa
na jibu la maana, akaendelea kushikilia msimamo wake. Mwisho nikaona
nisimlazimishe sana, nikamwambia kama hivyo ndivyo basi tugawane mali
ili mimi niondoke aje huyo mwenzangu kwani sitakuwa tayari kuishi maisha
ya uke wenza. Kwa kweli hakuwa na jibu la maana.”
Akionyesha sehemu ya jeraha.
HARUFU YA KIFO
“Ugomvi
huo ulitokea Jumanne, kesho yake yaani Jumatano (siku ya tukio) mume
wangu alivyorudi shamba nilimtengea ugali kama kawaida. Alikula vizuri
tu... tukapanda kitandani kulala, kama unavyojua tena wanandoa muda wao
wa kuzungumza kwa utulivu ni usiku, nikaamua kuutumia muda huo kumwuliza
mwenzangu.
“Nikamwambia
kama bado ana msimamo wake uleule, anipe sehemu yangu niondoke zangu.
Hapo nikawa nimechokoza moto. Ilikuwa ghafla tu, aliamka kitandani na
kuchukua nyundo kisha akaileta kichwani na kunipiga nayo, baadaye
akanipiga mdomoni na kuning’oa meno mawili ya mbele kwa kutumia ile
nyundo.
“Hakuishia
hapo, akanitoa panga kisha akanicharanga mikono yote, palepale damu
zikaruka kama kachinja ng’ombe. Nilihisi maumivu makali sana, sikuwahi
kupata maumivu makali kama yale. Kusema ukweli nilichanganyikiwa kabisa
na kile kipigo.”
ATUMIA UJANJA KUJIOKOA
“Wakati
akiendelea kunipiga bila huruma, alikuwa akisema dawa yangu mimi ni
kufa ili aweze kumchukua huyo mwanamke wake bila usumbufu. Nilivyosikia
hivyo ikabidi nitumie akili; nikajiangusha chini na kujifanya nimekata
kauli ili nisiendelee kuumia.
“Alipoona
hivyo kweli akaniacha. Akavaa nguo zake na kukimbia. Mwanangu mdogo
Nesto akanisaidia kunikongoja hadi kwa jirani yetu Mzee Chota ambaye
naye aliita majirani haraka, ilikuwa ni saa sita usiku, wakanikimbiza
hadi Zahanati ya Mlali lakini nikapewa rufaa ya kuletwa hapa kutokana na
hali yangu kuwa mbaya.”
Kwa
mujibu wa Bi. Faustina, licha ya mume wake kumfanyia ukatili huo, ndugu
wanaofika hospitalini hapo kumjulia hali, wanasema mumewe bado
hajakamatwa na amekuwa akiendelea kutoa vitisho dhidi yake.
Uwazi
lilifunga safari hadi kijijini Mgeta kwa lengo la kuhojiana na
mtuhumiwa huyo na kufanikiwa kumkuta lakini alipomuona mwandishi wetu,
Miasiku alitimua mbio akidhani alifuatwa na askari.
Comments
Post a Comment