ANGALIA PICHA ALICHOFANYIWA BABA MWENYE NYUMBA HATOSAHAU MAISHANI.
Jamaa
aliyetajwa kwa jina moja la Lugali akihusishwa kuchepuka na mke wa
mpangaji wake, akiwa amenaswa kwenye gesti moja maeneo ya Buguruni, Dar.
Vunja
jungu! Saa kadhaa kabla ya kuanza kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, jamaa
aliyetajwa kwa jina moja la Lugali ameibua sekeseke kwenye nyumba ya
kulala wageni (gesti), kisa kikidaiwa ni mchepuko akihusishwa na mke wa
mpangaji wake, Ijumaa Wikienda lina kisa na mkasa.Wakati
ikirandaranda mitaani kutega mingo, Timu ya Oparesheni Fichua Maovu
(OFM) ya Global Publishers ilipokea mchongo kuwa kuna timbwili kwenye
gesti moja maeneo ya Buguruni, Dar ambapo walifika eneo la tukio na
kushuhudia kasheshe hilo la aina yake.
Ndugu wa mume waliyefumania wakimdhibiti baba mwenye nyumba huyo.
OFM
ilimshuhudia mzee huyo akichomolewa kutoka chumbani huku damu zikimvuja
baada ya kula kichapo kutoka kwa jamaa na ndugu wa mwanaume aliyedai
kuwa jamaa huyo alikuwa anamsumbua mkewe.
Mke aliyekuwa akisumbuliwa, na ndugu wa mume wenye hasira wakizidi kumuadabisha mtuhumiwa.
Kwa
mujibu wa mashuhuda, kabla ya jamaa hao kuingia chumbani humo kwanza
walivunja mlango wa chumba hicho baada ya kupata idhini kutoka kwa
msimamizi wa gesti hiyo kufuatia baba mwenye nyumba huyo kukahidi
kuwafungulia mlango ili wamchukue mke wa ndugu yao aliyedaiwa kuwa ndani
na mzee huyo.
Baba mwenye nyumba akizidi kuchezea kichapo.
Walidai
kwamba mzee huyo ambaye ni baba mwenye nyumba, alikuwa akimtolea udenda
mke huyo wa mpangaji wake ambaye ni jirani yake huku akimsumbua mara
kwa mara kwa simu na ujumbe mfupi wa SMS.
Ilidaiwa
kwamba kufuatia usumbufu huo, mke huyo alimweleza mumewe lakini mumewe
hakuamini kama kweli baba mwenye nyumba alikuwa akimtaka mke wake
kimapenzi.
Ilisemekana
kuwa mume huyo alimweleza mkewe ili aamini kweli baba mwenye nyumba
alipania kumtaka basi amkubali ili amkute naye gesti amkomeshe kwa tabia
hiyo ya baadhi ya wenye nyumba ambao huwataka wake wa wapangaji wake.
“Nilimwambia
mke wangu amkubali kwa sababu nilikuwa na nia ya kukomesha tabia yake
ya kutongoza wake wa wapangaji wake, akamwita Buguruni ndipo nikawapigia
ninyi waandishi wa habari ili mje mchukue ushahidi,” alisema mume
huyo.
Baada
ya kukutwa gesti humo, mzee huyo aliomba msamaha kwa mpangaji wake huyo
na kuahidi kulipa fidia ambapo aliwaandikia cheki feki kisha
akakimbilia Kituo cha Polisi cha Buguruni na kufungua shauri kuwa
alitekwa, akapigwa kisha akapelekwa gesti.
Shauri
hilo ambalo liliandikishwa kwa jalada namba BUG/RB 6182/2014- utekaji.
Mzee huyo alidai kutekwa na mpangaji wake huyo na kumpeleka nje ya mji
kisha kumpiga ili kuua soo.
Hadi gazeti hili linaanua jamvi kituoni hapo, polisi walikuwa wakichunguza ili ukweli ujulikane
Comments
Post a Comment