ANGALIA PICHA SAFARI YA MWISHO YA MWANAFUNZI DANIEL LEMA ALIYECHOMWA MOTO KWA KUTUMIWA KUWA MWIZI
Mwili
wa Daniel Lema ukiagwa na baadhi ya wanachuo pamoja na raia
waliojitokeza kuhudhuria ibada ya kuuaga mwili wa marehemu mapema
asubuhi ya leo katika hospitali ya rufaa mkoani iringa.
Mwanafunzi (LEMA) aliyejeruhiwa kwa moto |
Baadhi ya raia walijitokeza kumuaga Lema katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya rufaa mkoani Iringa.
LEMA
Aliyekua akisoma mwaka wa 4 kozi ya sheria katika chuo kikuu kishiriki
cha Mt.Augustino Tawi la Iringa (Ruaha University College-RUCO),
mwanzoni mwa wiki hii ameshambuliwa kwa kuunguzwa na moto akidhaniwa ni
mwizi.
Mnamo tarehe 24.06.2014 mwanafunzi
huyo alikua ametoka kuangalia michuano ya kombe la dunia na akiwa
amelewa akawa anatafuta chakula cha jioni na ilikua majira ya saa 5
Usiku, Mwanafunzi huyo aliingia kwenye mgahawa ambao biashara ilikua
imefungwa kwa muda huo lakini ndani kulikuwapo na binti ambaye alianza
kupiga kelele kwa kudhani alikua mwizi.
Na kwakua eneo hilo kulikuwa na mlinzi(Mmasai) ndiye aliyeanza kumshambulia mwanafunzi huyo.
Baada ya tukio hilo wakatokea watu
(2) waliojitambulisha kuwa ni askari wakaamuru mwanafunzi huyo asipigwe
kwa madai ya kumfikisha kituoni.
Lakini baada ya mwendo mfupi
kuelekea kituoni mwananchi mmoja alimchukua kijana huyo kinguvu kisha
kumwagia mafuta na kisha kumuwasha moto, ambao ulizimwa na madereva
bodabora walio kuwa eneo hilo na kisha kumkumbiza kijana huyo hospitali.
Mpaka sasa Kijana huyo amelazwa
katika wodi ya watu mahututi (ICU) katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa
Iringa ambapo mama yake mzazi pamoja na kaka yake ndio wanaomsaidia
kumuhudumia.
Mwili wake umeagwa mapema leo
katika hospitali ya rufaa mkoani Iringa tayari kwa safari ya kuelekea
mkoani Kilimanjaro kwaajili ya mazishi yatakayofanyika siku ya juma
tano.
Lema alizaliwa mnamo tarehe 05/06/1989 na kufariki tarehe 30/06/2014 Mungu na ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi!!!
Comments
Post a Comment