Posts

PICHA ZINATISHA..UKATILI MKUBWA..BABA AMCHARANGA MAPANGA MWANAE..KISA..KUANGUSHA TREI ZA MAYAI..!

Image
Tukio hili lilitokea eneo la Kitunda Dar es salaam pale mtoto huyu alipoangusha  baiskeli iliyokua na trei 25 za mayai. Ni ngumu kuamini kama Baba mzazi  wa mtoto ndiye aliyetenda kitendo hiki. credit:kandili yetu

TAZAMA BIBI WA MIAKA 100 ALIYEMALIZA SHULE YA MSINGI NA ANALENGO LA KUENDELEA KUSOMA ELIMU YA SEKONDARI..!!

Image
Bibi mmoja nchini Mexico amefanikiwa kuhitimu elimu ya shule ya msingi akiwa na umri wa miaka 100. Bibi huyo Manuela Hernandez (pichani) ambaye alizaliwa katika jimbo la Oaxaca mnamo mwezi Juni 1913, aliacha shule ya msingi baada ya kusoma kwa mwaka mmoja tu na kurejea kuisaidia familia yake masikini kufanya kazi za nyumbani. Hata hivyo alirejea shule kuendelea na masomo mwezi Oktoba mwaka uliopita akiwa na miaka 99 kufuatia kushauriwa na mmoja wa wajukuu zake. Manuela Hernandez akiwa ameshikilia cheti chake cha kuhitimu elimu ya msingi. Hivi sasa tayari amekabidhiwa diploma yake ya elimu ya msingi katika sherehe iliyofanyika katika jimbo Mexico Kusini. Bibi Hernandez amesema sasa ataendelea na masomo ya elimu ya sekondari. Zaidi ya nusu ya wakazi wa jimbo la Oaxaca wenye umri wa zaidi ya miaka 15 hawajamaliza elimu ya msingi

MAMAA MAJANGA AWAPA MAKAVU LIVE WANAWAKE WEZI WA WAUME ZA WATU....!!!SHUKA NAYO HAPA...

Image
  Mamaa  Majanga, Snura Mushi. MAMAA  Majanga, Snura Mushi amefunguka kuwa kinachowaponza wanawake wengi wanaoiba wanaume za watu ni kupenda kujitangaza.   Akizungumza kupitia  Global Online TV  (itaruka leo mtandaoni), Snura alisema kwa kulitambua hilo ndiyo maana aliwatonya kuwa ukiiba mume wa mtu fanya siri katika wimbo wa Nimevurugwa. “We ni mwizi halafu unatangaza kila sehemu unatafuta nini kama siyo matatizo na mwenye mali…,” alisema Snura. Ili kutazama mahojiano kamili na jinsi Snura alivyofunguka mambo mengi, fuatilia Global Online TV badae ili upate uhondo kamili.

SHEREHE YA KUTIMIZA MIAKA 3 YA BONGO MOVIE YAFANYA KATIKA UKUMBI WA EAST 24 MWISHONI MWA WIKI

Image
 Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steve Mengele (Nyerere) akihojiwa na waandishi wa habari wakati wa sherehe ya Kutimiza miaka 3 ya Klabu ya Bongo Movie, sherehe iliyofanyika katika Ukumbi wa East 24 uliopo Katika Jengo la Arcade Mikocheni, Mwishoni mwa Wiki Warembo wakiwa wamebeba Chupa za Windhoek zinazosambazwa na kuuzwa na Kampuni ya Mabibo Beer ambao ndio walikuwa wadhamini wakuu wa Sherehe ya Kutimiza Miaka 3 ya Klabu ya Bongo inayoongozwa na Steve Nyerere. Mwenyekiti wa Makampuni yaliyo chini ya Proin Group Of Companies, Bw Johnson Lukaza akipokea cheti cha kuthaminiwa kutoka kwa Mwenyekiti wa Bongo Movie kama mmoja wa wamiliki wa kampuni ya usambazaji wa kazi za filamu nchini  iitwayo Proin Promotions Limited.  Burudani pia zilikuwepo  Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabibo Beer, Mama Benadetha Rugemalila akiongea na waandishi wa habari wakati wa sherehe hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa East 24 uliopo Mikocheni katika jengo la Arcad

JIDE: MIMI NA GARDNER TUNAISHI KAMA KAKA NA DADA...!

Image
Super woman katika Afro-Pop, Judith Wambura a.k.a Lady Jaydeee au Jide katika  pozi na mume wake   Gardner Habash ‘Kapteini’ . Kumbe! Super woman katika Afro-Pop, Judith Wambura a.k.a Lady Jaydeee au Jide amefunguka kuwa yeye na mumewe, Gardner Habash ‘Kapteini’ kwa sasa wanaishi kama kaka na dada hivyo kuibua swali kivipi? Akizungumza na Ijumaa Wikienda katika mahojiano maalum yaliyofanyika kwenye  mgahawa wa staa huyo wa Nyumbani Lounge uliopo Ada Estate, Kinondoni jijini Dar mwishoni mwa wiki iliyopita, Jide alisema kuwa yeye na Gardner wamefikia hatua  ya kuishi katika staili  hiyo kutokana na mapenzi yao yaliyopitiliza. “Gardner ananipenda sana na mimi pia vilevile nampenda sana mume wangu. Mapenzi  yetu yamepitiliza hadi tunajiona kama vile tumezaliwa tumbo moja na ndiyo maana  nawaambia kuwa mimi na yeye tunaishi kama kaka na dada,” alifunguka Jide. Akiendelea kuzungumza kwa kujiamini, Jide alisema kuwa hadi simu ya mkononi  wanatumia moja

AJALI YAUA 22 KIBITI PWANI, YAHUSISHA MAGARI MATANO

Image
Watu 22 wamefariki duniani papo hapo katika ajali ya gari iliyotokea katika kijiji cha Mkupuka tarafa ya Kibiti iliyohusisha magari matano. Ajali hiyo imetokea jana usiku wa saa mbili kufuatia Hiace iliyokuwa ikijaribu kulipita gari lingine aina ya Tata lenye namba za usajili T 132 AFJ lililokuwa limesimama baada ya kugongana uso kwa uso na gari aina ya Kenta lenye namba za usajili T.774. Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa wa Pwani, Hajjat Mwantum Mahiza, wengi waliokufa ni vijana waliokuwa wanatoka Ikwiriri kwenda Kibiti wakiwa na lori aina ya Fuso na bidhaa zao kwa ajili ya mnada leo.

MAGAZETI YA MICHEZO NA BURUDANI

Image
MAGAZETI YA UDAKU LEO

MEZA YETU YA MAGAZETI YA LEO JUMATATU TAREHE 31.03.2014.

Image

ANGALIA NAFASI MPYA YA KAZI KUTOKA TPDC

Image
TANZANIA PETROLEUM DEVELOPMENT CORPORATION CAREER OPPORTUNITY MANAGING DIRECTOR Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC) is a National Institution established in 1969 with a mandate to undertake petroleum development.  TPDC has its headquarters in Dar es salaam and carries its operations in selected petroleum potential areas throughout the country, including the continental shelf of Tanzania.  The Corporation is currently operating in partnership with international oil companies under Production Sharing Agreements (PSA). Using this arrangement in recent years, major discoveries of natural gas have been made, both onshore and offshore. These discoveries provide TPDC with significant growth potential, with corresponding increased managerial and operational challenges across the petroleum value chain ranging from upstream, midstream to downstream.  To cope with such dynamic managerial and operational challenges, TPDC is looking for an expe

HEIFER INTERNATIONAL TANZANIA YAZINDUA MRADI MKUBWA WA KUENDELEZA SEKTA YA MAZIWA KWA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI

Image
Naibu waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi ambae pia alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Mh Kaika Telele akiongea na wageni waalikwa na wadau wa sekta ya Maziwa Afrika Mashariki uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwl Nyerere Mwishoni mwa Wiki.  Mkurugenzi Mkuu wa Heifer International Tanzania, Dk Henry Njakoi akiongea na wageni waalikwa na wadau wa sekta ya maziwa nchini na wa kimataifa waliofika katika uzinduzi wa Mradi wa Uendelezaji Sekta ya Maziwa Afrika Mashariki uliodhaminiwa na Mfuko wa Bill na Melinda, Mradi huo mkumbwa ulizinduliwa ijumaa iliyopita katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwl Nyerere uliopo Jijini Dar Es Salaam  Mkurugenzi Mkuu wa East Africa Dairy Development (EADD), Mh Rakesh Kapoor akichangia mada kwenye uzinduzi wa Mradi wa Kuendeleza sekta ya Maziwa kwa Nchi za Afrika Mashariki mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwl Nyerere, jijini Dar Es Salaam. Mradi huo mkubwa kutoka Heifer I