TAZAMA BIBI WA MIAKA 100 ALIYEMALIZA SHULE YA MSINGI NA ANALENGO LA KUENDELEA KUSOMA ELIMU YA SEKONDARI..!!


Bibi mmoja nchini Mexico amefanikiwa kuhitimu elimu ya shule ya msingi akiwa na umri wa miaka 100. Bibi huyo Manuela Hernandez (pichani) ambaye alizaliwa katika jimbo la Oaxaca mnamo mwezi Juni 1913, aliacha shule ya msingi baada ya kusoma kwa mwaka mmoja tu na kurejea kuisaidia familia yake masikini kufanya kazi za nyumbani. Hata hivyo alirejea shule kuendelea na masomo mwezi Oktoba mwaka uliopita akiwa na miaka 99 kufuatia kushauriwa na mmoja wa wajukuu zake.
Manuela Hernandez akiwa ameshikilia cheti chake cha kuhitimu elimu ya msingi. Hivi sasa tayari amekabidhiwa diploma yake ya elimu ya msingi katika sherehe iliyofanyika katika jimbo Mexico Kusini. Bibi Hernandez amesema sasa ataendelea na masomo ya elimu ya sekondari. Zaidi ya nusu ya wakazi wa jimbo la Oaxaca wenye umri wa zaidi ya miaka 15 hawajamaliza elimu ya msingi

Comments

Popular posts from this blog