Posts

JIDE: MIMI NA GARDNER TUNAISHI KAMA KAKA NA DADA...!

Image
Super woman katika Afro-Pop, Judith Wambura a.k.a Lady Jaydeee au Jide katika  pozi na mume wake   Gardner Habash ‘Kapteini’ . Kumbe! Super woman katika Afro-Pop, Judith Wambura a.k.a Lady Jaydeee au Jide amefunguka kuwa yeye na mumewe, Gardner Habash ‘Kapteini’ kwa sasa wanaishi kama kaka na dada hivyo kuibua swali kivipi? Akizungumza na Ijumaa Wikienda katika mahojiano maalum yaliyofanyika kwenye  mgahawa wa staa huyo wa Nyumbani Lounge uliopo Ada Estate, Kinondoni jijini Dar mwishoni mwa wiki iliyopita, Jide alisema kuwa yeye na Gardner wamefikia hatua  ya kuishi katika staili  hiyo kutokana na mapenzi yao yaliyopitiliza. “Gardner ananipenda sana na mimi pia vilevile nampenda sana mume wangu. Mapenzi  yetu yamepitiliza hadi tunajiona kama vile tumezaliwa tumbo moja na ndiyo maana  nawaambia kuwa mimi na yeye tunaishi kama kaka na dada,” alifunguka Jide. Akiendelea kuzungumza kwa kujiamini, Jide alisema kuwa hadi simu ya mkononi  wanatumia moja

AJALI YAUA 22 KIBITI PWANI, YAHUSISHA MAGARI MATANO

Image
Watu 22 wamefariki duniani papo hapo katika ajali ya gari iliyotokea katika kijiji cha Mkupuka tarafa ya Kibiti iliyohusisha magari matano. Ajali hiyo imetokea jana usiku wa saa mbili kufuatia Hiace iliyokuwa ikijaribu kulipita gari lingine aina ya Tata lenye namba za usajili T 132 AFJ lililokuwa limesimama baada ya kugongana uso kwa uso na gari aina ya Kenta lenye namba za usajili T.774. Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa wa Pwani, Hajjat Mwantum Mahiza, wengi waliokufa ni vijana waliokuwa wanatoka Ikwiriri kwenda Kibiti wakiwa na lori aina ya Fuso na bidhaa zao kwa ajili ya mnada leo.

MAGAZETI YA MICHEZO NA BURUDANI

Image
MAGAZETI YA UDAKU LEO

MEZA YETU YA MAGAZETI YA LEO JUMATATU TAREHE 31.03.2014.

Image

ANGALIA NAFASI MPYA YA KAZI KUTOKA TPDC

Image
TANZANIA PETROLEUM DEVELOPMENT CORPORATION CAREER OPPORTUNITY MANAGING DIRECTOR Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC) is a National Institution established in 1969 with a mandate to undertake petroleum development.  TPDC has its headquarters in Dar es salaam and carries its operations in selected petroleum potential areas throughout the country, including the continental shelf of Tanzania.  The Corporation is currently operating in partnership with international oil companies under Production Sharing Agreements (PSA). Using this arrangement in recent years, major discoveries of natural gas have been made, both onshore and offshore. These discoveries provide TPDC with significant growth potential, with corresponding increased managerial and operational challenges across the petroleum value chain ranging from upstream, midstream to downstream.  To cope with such dynamic managerial and operational challenges, TPDC is looking for an expe

HEIFER INTERNATIONAL TANZANIA YAZINDUA MRADI MKUBWA WA KUENDELEZA SEKTA YA MAZIWA KWA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI

Image
Naibu waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi ambae pia alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Mh Kaika Telele akiongea na wageni waalikwa na wadau wa sekta ya Maziwa Afrika Mashariki uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwl Nyerere Mwishoni mwa Wiki.  Mkurugenzi Mkuu wa Heifer International Tanzania, Dk Henry Njakoi akiongea na wageni waalikwa na wadau wa sekta ya maziwa nchini na wa kimataifa waliofika katika uzinduzi wa Mradi wa Uendelezaji Sekta ya Maziwa Afrika Mashariki uliodhaminiwa na Mfuko wa Bill na Melinda, Mradi huo mkumbwa ulizinduliwa ijumaa iliyopita katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwl Nyerere uliopo Jijini Dar Es Salaam  Mkurugenzi Mkuu wa East Africa Dairy Development (EADD), Mh Rakesh Kapoor akichangia mada kwenye uzinduzi wa Mradi wa Kuendeleza sekta ya Maziwa kwa Nchi za Afrika Mashariki mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwl Nyerere, jijini Dar Es Salaam. Mradi huo mkubwa kutoka Heifer I

DK. MARIA KAMM AIBUKA KIDEDEA TUZO YA MWANAMKE BORA

Image
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewataka wanawake walioteuliwa kwenye Tuzo ya Mwanamke Bora wa mwaka 2013/2014 wasibweteke bali waendeleze juhudi zao na wazidi kung’ara zaidi. Ametoa wito huo jana usiku (Jumamosi, Machi 29, 2014) kwenye hafla ya kumtuza mwanamke bora wa mwaka 2013/2014 iliyofanyika kwenye ukumbi wa African Dream nje kidogo ya mji Dodoma. “Lazima muendelee kuonekana mnazidi kung’ara. Tuzo ni njema kwa upande mmoja lakini pia ina changamoto zake kubwa ikiwa ni ya kuendelea kubaki mnang’ara hadi waliowapigia kura wakawaona mnafaa,” alisema Waziri Mkuu. Utoaji wa tuzo hiyo uliwapambanisha Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka; Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Asha-Rose Migiro; Mwalimu Mkuu Mstaafu na Mbunge Mstaafu, Dk. Maria Kamm pamoja na Mbunge wa Same Mashariki, Bi. Anne Kilango Malecela. Kila mmoja alikabidihiwa Tuzo ya Mwanamke Bora na Waziri Mkuu Pinda lakini Dk. Maria Kamm ndiye aliyeibuka mshindi wa jumla kwa kukabidhiwa

Mbeya City yainyuka Prisons, Mtibwa, JKT Ruvu kidedea

Image
Mbeya City Mtibwa Sugar iliyoitungua Coastal kwa mabao 3-1 BAO pekee lililofungwa katika dakika ya pili ya mchezo na Paul Nonga, lilitosha kuipa ushindi muhimu Mbeya City dhidi ya mahasimu wao Prisons na kuipumulia Yanga kisogoni kwenye mbio za kuwania nafasi mbili za juu za Ligi Kuu Tanzania bara msimu huu. Pambano hilo lililochezwakwenye uwanja wa Sokoine lilikuwa la vuta nikuvute, lakini ni Mbeya waliondeleza ubabe kwa wajelajela hao kwa kuwalaza kwa mara nyingine katika msimu wao wa kwanza wa ligi hiyo baada ya mchezo wa kwanza kuwanyuka 2-0. Kwa ushindi huo Mbeya City imefikisha pointi 45 moja pungufu na Yanga waliolala 2-1 Mkwakwani Tanga dhidi ya Mgambo JKT. Katika mechi nyingine ya ligi hiyo iliyochezwa uwanja wa Manungu, Mtibwa Sugar ilipata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya wageni wao Coastal Union. Mabao ya washindi katika mchezo huo yalifungwa na Jamal Mnyate dakika ya 14 kabla ya Coastal kusawazisha kupitia kwa Mbwana Hamis na Mussa Hassan kuipa uo

LIGI KUU TANZANIA BARA :SIMBA YANGA ZACHAPWA

Image
Yanga yafa Mkwakwani, Azam yanusa ubingwa Yanga Azam KLABU Ya Azam imejiweka katika mazingira mazuri ya kutwaa taji la Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara ya kwanza baada ya jioni hii kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Simba, huku Yanga ikifa Mkwakwani. Yanga ilikumbana na kipigo cha mabao 2-1 toka kwa Mgambo JKT na kutoa nafasi kubwa kwa Azam kunyakua taji hilo kama itashinda mechi mbili kati ya tatu ilizosalia katika ligi kabla ya msimu kuisha. Mabao ya Mcha Khamis 'Vialli' na John Bocco 'Adebayor' kwa kila kipindi yalitosha kuiwezesha Azam kuendeleza rekodi ya kutopoteza mechi kwa msimu huu na kufikisha pointi 53. Bao la Simba lililokuwa la kusawazisha lilifungwa kwa kichwa na beki wake wa kati, Joseph Owino dakika chache kabla ya mapumziko. Nako jijini Tanga bao la mapema la mshambuliaji mkali, Fully Maganga na jingine la mkwaju wa penati wa Malimi Basungu lililotosha kuizamisha Yanga kwenye uwanja wa Mkwakwani, bila kutarajiw

AJALI MBAYA YAUA WANAWAKE 12 MKOANI KILIMANJARO WALIOKUWA WAKIENDA MSIBANI....MAJINA YAO YATAJWA, SABA WAJERUHIWA

Image
Waombolezaji 12 waliokuwa njiani kuhani msiba wa mtoto aliyepoteza maisha baada ya kusombwa na mafuriko, wamefariki dunia na wengine saba wamejeruhiwa, baada ya gari lao kugongwa na malori mawili kwa wakati mmoja. Abiria hao walikuwa wanasafiri na gari dogo aina ya Toyota Pick Up namba T 170 AKZ kwenda kuhani msiba uliotokea katika kijiji cha Kongei kilichoko Hedaru mkoani Kilimanjaro. Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro , Robert Boaz waliofariki ni Stella John (45), Salma Kizoka (33), Marry Senzige (49), Neema Daniel (52), Rehema George, (29), Sophia Mbike (51), Ritta Kallani (55) na Kallan Stephano (55), Kolina Mmasa (55) na Bahati Daudi (25), Wengine ni Farida Kiondo (24) na Maria John (33) wote wakazi wa Kongei na kwamba miili yao imehifadhiwa katika hospitali ya Wilaya ya Same. Boaz aliwataja majeruhi kuwa ni Zubeda Mrindoko (42),Mipa Chediel (29) na Zubeda Mlita (32) ambao wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya KCMC kutokana na

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA AWASILI MKOANI RUKWA LEO TAYARI KWA KUANZA ZIARA YAKE YA SIKU 21

Image
 Baadhi ya Wananchi na wanachama mbalimbali wakisubiri kumpokea katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana kabla ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege mjini Sumbawanga mkoani Rukwa mapema leo asubuhi.   Ndege iliyombeba Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana ikiwasili katika uwanja wa ndege mjini Sumbawanga,mkoani Rukwa mchana huu.   Ndugu Kinana akishuka kwenye ndege mara baada ya kuwasili mchana huu Sumbawanga mkoani Rukwa,tayari kwa kuanza ziara yake rasmi mkoni humu,ambapo ziara yake rasmi inaanzia Wilaya ya Nkasi,mkoani Rukwa.  Ndugu Kinana akipokelewa na viongozi mbalimbali wa CCM mkoa Rukwa mara baada ya kuwasili mapema leo mchana.  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akivalishwa skafu na vijana wa chipukizi mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege mjini Sumbawanga,mkoani Rukwa mapema mchana huu. Katikubu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na Kada maarufu wa CCM,Ndugu Chrisant Mzindakaya,mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege mjini Sumbawanga,mkoan

HABARI+PICHAZ..NI HATARIIIII MTAZAME HAMISA NA UTAALAMU WA KUCHEZA NA NYOKA..

Image
MREMBO aliyeng’ara kwenye Shindano la Miss Tanzania mwaka 2011, Hamisa Hassan ‘Mabeto’ amefunguka kuwa, licha ya baadhi ya wasichana wenzake kutokuwa na ujasiri wa kucheza na nyoka, yeye anao.   Mrembo aliyeng’ara kwenye Shindano la Miss Tanzania mwaka 2011, Hamisa Hassan ‘Mabeto’   Akipiga stori na Ijumaa, Mabeto alisema awali alikuwa muoga lakini taratibu alianza kumzoea kiumbe huyo na sasa humtumia hata katika shughuli zake za kimodo anazofanya.   “Hizo picha nilikuwa kwenye ‘photo shooting’ (upigaji wa picha) ila kiukweli nina utaalam wa kucheza na nyoka, unajua siyo kila mtu anao ujasiri wa kumchezea, kwanza anatisha ila mimi nilianza kumzoea taratibu,” alisema Mabeto.