LIGI KUU TANZANIA BARA :SIMBA YANGA ZACHAPWA
Yanga yafa Mkwakwani, Azam yanusa ubingwa
Yanga |
Azam |
KLABU Ya Azam
imejiweka katika mazingira mazuri ya kutwaa taji la Ligi Kuu Tanzania
Bara kwa mara ya kwanza baada ya jioni hii kupata ushindi wa mabao 2-1
dhidi ya Simba, huku Yanga ikifa Mkwakwani.
Yanga ilikumbana na kipigo cha mabao 2-1
toka kwa Mgambo JKT na kutoa nafasi kubwa kwa Azam kunyakua taji hilo
kama itashinda mechi mbili kati ya tatu ilizosalia katika ligi kabla ya
msimu kuisha.
Mabao ya Mcha Khamis 'Vialli' na John Bocco
'Adebayor' kwa kila kipindi yalitosha kuiwezesha Azam kuendeleza rekodi
ya kutopoteza mechi kwa msimu huu na kufikisha pointi 53.
Bao la Simba lililokuwa la kusawazisha
lilifungwa kwa kichwa na beki wake wa kati, Joseph Owino dakika chache
kabla ya mapumziko.
Nako jijini Tanga bao la mapema la
mshambuliaji mkali, Fully Maganga na jingine la mkwaju wa penati wa
Malimi Basungu lililotosha kuizamisha Yanga kwenye uwanja wa Mkwakwani,
bila kutarajiwa.
Yanga waliokuwa na matumaini makubwa
kuibuka na ushindi dhidi ya 'vibonde' hao, walishindwa kuamini
walipojikuta wakitafuta bao la kusawazisha licha ya Mgambo kucheza
pungufu uwanjani.
Bao la Yanga la kufutia machozi lililokuwa la kusawazisha lilifungwa kwa mkwaju wa penati na Nadir Haroub 'Cannavaro'.
Comments
Post a Comment