DK. MARIA KAMM AIBUKA KIDEDEA TUZO YA MWANAMKE BORA
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewataka wanawake walioteuliwa kwenye Tuzo ya Mwanamke Bora wa mwaka 2013/2014 wasibweteke bali waendeleze juhudi zao na wazidi kung’ara zaidi. Ametoa wito huo jana usiku (Jumamosi, Machi 29, 2014) kwenye hafla ya kumtuza mwanamke bora wa mwaka 2013/2014 iliyofanyika kwenye ukumbi wa African Dream nje kidogo ya mji Dodoma. “Lazima muendelee kuonekana mnazidi kung’ara. Tuzo ni njema kwa upande mmoja lakini pia ina changamoto zake kubwa ikiwa ni ya kuendelea kubaki mnang’ara hadi waliowapigia kura wakawaona mnafaa,” alisema Waziri Mkuu. Utoaji wa tuzo hiyo uliwapambanisha Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka; Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Asha-Rose Migiro; Mwalimu Mkuu Mstaafu na Mbunge Mstaafu, Dk. Maria Kamm pamoja na Mbunge wa Same Mashariki, Bi. Anne Kilango Malecela. Kila mmoja alikabidihiwa Tuzo ya Mwanamke Bora na Waziri Mkuu Pinda lakini Dk. Maria Kamm ndiye aliyeibuka mshindi wa jumla kwa kukabidhiwa