MAUHAJI YA KUTISHA YA MTOTO YAFANYIKA UKO MKOANI MANYARA WILAYA YA MBULU.

Pata kisa hiki cha kusikitisha ambacho kilikuwa hakijawahi tokea katika kijiji hiki kwani kilisababisha vilio kutanda ndani ya mji mzima.

 Jeneza la marehemu Jenefrida likiwa limebebwa na waombolezaji kuelekea makaburi
MAHUAJI.
Mahuaji haya yalitokea mnamo tarehe 25/03/2014 katika kijiji cha GIDEMOSA kata ya DONGOBESH wilaya ya MBULU mkoani Manyara mnamo majira ya saa tisa alasiri ambapo mtoto JENIFRIDA PAULO aliweza kuuwawa Kikatili kwa kuchomwa kisu pemebezoni ya kichwa na hatimaye kuchinjwa shingo na uku kolomea likiwa limening'inia na akisaidiwa kushikiliwa na ngozi tu..
CHANZO CHA KIFO.
Marehemu JENIFRIDA PAULO mnamo trh 25 kabla ya kukumbwa na mauti hayo akiwa nyumbani kwao mchana, akiwa yeye na mama yake mzazi. Mama wa marehemu akiwa ndani ya nyumba kubwa kapumzika kutokana na matatizo ya kiafya yanayomkaribi kwa muda, ilamuagiza mwanae(marehemu) aende katika nyumba ndogo yaani jiko na stoo akatoe kuni zilizokuwa nje ya myumba na akaziweke ndani ili usiku waweze kuzitumia kwani siku hiyo kulikuwa na dalili ya mvua kubwa. 
Marehemu alikuabli na akaenda kupeleka kuni hizo ndani ndani, akiwa katika zoezi hilo pekee yake mara ghafla alitokea kijana mmoja ambaye inasemekana aliwahi kuishi hapo nyumbani kwao na marehemu kwa muda wa miaka minne. ambaye alikuwa amejibana pembezoni mwa nyumba yao hiyo marehemu na akamuita Jeney njoo hapa, basi marehemu bila kusita alienda na yule kijana. 
KABLA YA MAHUTI
Kwa mujibu wa mahojiano na mwandishi wetu wa mtandao wetu wa phars blog Uliweza kuhojiana na mama wa marehemu na alisema kuwa akiwa amemtuma mtoto wake kwenda kuingiza kuni ndani, alisikia sauti kwa mbali ikitoka kwa mwanae ambaye ni marehemu akisema kuwa"SIKUPI FUNGUO BABA ATANIPIGA" tuliendelea kufahamu kwa nini marehemu alisema hivyo. ndipo tulijul;ishwa kuwa marehemu Jenifrida alikuwa ni miongoni mwa watoto waliokuwa wakiaminiwa na baba yake mzazi na kufikia kumkabidhi funguo za nyumba ambayo ndani ya chumba hicho kulikuwa na pesa, pamoja na hati mbalimbali za mashamba na nyumba ambazo muhuaji huyu alikuwa anazitaka na hadi kufikia kufanya mahuaji hayo ya kinyama
 
mama wa marehu Jenifrida akiaweka taji katika kaburi.
TAARIFA ZA KIFO KUSIKIKA
Mara baada ya mahuaji kufanyika yule muhuaji alimfungia mama awa marehemu kwa nje na kisha kutokomea. Lakini ilipofika mnamo majira ya saa 12 jioni alirejea mdogo yake marehemu akitokea machungani akiwa na mifugo yake, ndio alipomaliza kufungia mifugo alienda ndani na kumkuta mama yake akiwa amefungiwa kwa nje alipomfungulia mlangoa alimhoji mama yake mzazi kuwa dada Jenifrida yuko wapi? Ndipo mama mzazi alimwambia alikuja mchana nikamtuma kwenda kuingiza kuni kule jikoni lakini tangu nimtume hajarudi nenda kamuone uko ndani, Basi  ndio mdogo wa marehemu alipoingia kule jikoni alikuta dada yake akiwa tayari ni marehemu amechinjwa amelazwa uvunguni mwa kijitanda kidogo na wakati huo akiwa amekwisha kauka na damu zile,kutokana na mshtuko wa mdogo wake marehemu kusikika ulimuinua mama mzazi na kuja ndani ndio naye alikuta mahuaji hayo na kuanza kipiga AYODAHA( Yowe)ili kupata msaada zaidi kutoka kwa majirani.
KUKAMATWA KWA MUHUSIKA/MUHUAJI
Kwa kutokana na uzito wa damu ya mtoto Jenifrida ilimsababisha muhuaji huyo kushindawa kukimbia na madhara yake hata wakati wananchi wakiwa wanapiga yowe naye alikuwepo japo siku hiyo alionekana ni mtu asiyekuwa na furaha yakutosha kama jinsi anavyofahamika pale kijijini.Hivi sasa muhuaji huyo anashikiliwa na jeshi la polisi wilayani Mbulu kwa uchunguzi na Mahojiano zaidi kabla yakufikishwa mahakani kusomewa shitaka linalomkabili.
HISTORIA YA MAREHEMU
Marehemu Jenifrida ni miongoni mwa watoto watano wa mzee Paulo,ambaye ni mtoto wa tatu kuzaliwa .
Jenifrida alizaliwa mnamo tarehe  30/05/2006.Marehemu alijiunga darasa la kwanza mnamo mwa 2013 katika shule ya msingi GIDEMOSA iliyoko katika kijiji cha Dongobesh.


picha ya marehemu Jenifrida enzi za uhai wake
Baba mzazi wa marehemu Jenifrida aliyevaa koti akiwa kwenye majonzi makali cna
 
Padri akisoma misa ya mwisho kabla zoezi lakufukia mwili wa marehemu kufanyika
 

mwili wa marehemu ukiingizwa kwenye nyumba yake ya milele, ambapo marehemu alizikwa kwenye makaburi ya kanisa katholiki dongobesh


Wazazi wa marehemu wakiwa na mchungaji maleko tayari kwa kuweka shada la maua katika kaburi
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE



Comments

Popular posts from this blog