JE WAJUA KUA NGUO ZA NDANI HUCHANGIA, UGUMBA? SOMA MAKALA HII UJUE MENGI

TAFITI Za Kisayansi Zimebaini Kuwa Nguo Za Ndani Hasa Zinazobana Kwa Wanaume Na Zile 
Za Aina Ya Nailoni (Nylon) Zinaathiri Uwezo Wa Mbegu Za Kiume, Hivyo Kushindwa Kutunga Mimba.

Utafiti huo uliofanyika katika nchi za Ufaransa na Uingereza na kuchapishwa katika Gazeti la Daily Mail la Uingereza unabainisha kuwa, wanaume wanaovaa nguo za ndani zinazobana na zile zilizotengezwa kwa malighafi ya nailoni, mbegu zao za kiume (manii) huwa nyepesi na kupoteza uwezo wa kutunga mimba
Vazi la ndani la wanaume linalojulikana kama boksa na nguo nyingine za ndani za kubana zenye asili ya nailoni, zinakuwa na athari kubwa zaidi hasa zinapovaliwa katika sehemu zenye joto, kama Dar es Salaam.
Kutokana na matokeo hayo, wanasayansi wameonya kuwa wanaume wanapaswa kuchukua tahadhari, hasa kutokana na tafiti nyingi za karibuni kuthibitisha kuongezeka kwa matatizo ya mbegu za kukosa uwezo wa kutunga ujauzito katika nyumba ya uzazi ya mwanamke.
Akizungumzia utafiti huo jana, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Uzazi katika Hosipitali ya Taifa Muhimbili, Dk Cyril Massawe, alisema una ukweli kutokana na mbegu za kiume kuwa nje ya mwili wa mwanamume tofauti na mwanamke ambaye kizazi chake kipo ndani.


“Kwa kawaida mwanamume anayeishi maeneo ya joto anapaswa kuwa makini sana, ili kuhifadhi vizuri manii yake anatakiwa kutumia mavazi yenye kupitisha hewa,” alisema Dk Massawe.
Ufaransa na Uingereza
Utafiti uliofanywa Ufaransa umebaini kuwa, upungufu wa nguvu za kiume kwa wanaume wengi ulianza kutokea tangu mwanzoni mwa 1990.
Awali, ilikuwa ikiaminika kuwa kupungua kwa uwezo wa mbegu za kiume kulitokana na sababu kama vile mtindo wa maisha, ulaji na matumizi ya dawa kupindukia na matumizi ya vyakula vyenye kemikali nyingi, lakini safari hii utafiti umebaini kuwa matumizi ya nguo za ndani yamekuwa yakiwaathiri wanaume wengi.
Mtafiti wa Uingereza, Profesa Richard Sharpe anasema tatizo hilo linaweza kuepukwa ikiwa mhusika atajitahidi kuvaa nguo zinazokubalika na mahala alipo. Hata hivyo, anapendekeza uchunguzi zaidi ufanywe ili kulinda kizazi cha sasa na kijacho.
Mtafiti huyo kutoka Chuo Kikuu cha Edinburgh anasema: “Uingereza suala hili halijawahi kuonekana wala kutiliwa mkazo na kuwa kipaumbele katika afya, labda kwa sababu ya wasiwasi kwamba sehemu za mwanamume zinatakiwa kubanwa. Hivi sasa hakuna shaka kwamba suala hilo ambalo liliongelewa hapo awali lina ukweli ndani yake, hivyo ni wakati kwa watu wote kuchukua hatua.”
“Kutokuchukua hatua kutasababisha familia nyingi kukosa watoto na hivyo idadi ya watu itapungua, lakini katika hali ya kawaida, ni vyema watu wakaelimishwa namna ya uvaaji. Sehemu za joto mtu anatakiwa kuvaa pamba na si nailoni ili kulinda mbegu zake.”
Profesa Sharpe anasema bado wanasayansi wana kazi kubwa kwani mpaka sasa karibu kila eneo ambalo wanasayanasi wamelichunguza limebainisha kuchangia tatizo hilo, lakini mpaka sasa wanafikiri kuwa vyakula vyenye mafuta na vile vyenye kemikali nyingi vina mchango mkubwa zaidi katika tatizo hilo.
Watafiti ambao walitumia takwimu kutoka katika vituo vya afya 126, waligundua kuwa tangu mwaka 1989 mpaka 2005, kulikuwa upungufu wa uwezo wa manii kwa mwanamume kufanya kazi kwa asilimia 32.2, kiwango ambacho ni karibu asilimia mbili kwa mwaka.
Watafiti walisema: “Kwa ufahamu wetu, ni utafiti wa kwanza kufanyika na umehusisha mbegu za kiume hai na uwezo wa manii katika nchi nzima kwa kipindi kirefu.”
“Huu ni utafiti mkubwa na unatoa onyo kali kiafya kwa jamii. Lakini huwezi kumlazimisha mtu kuhusu matumizi ya nguo za ndani,” wanasema.
Profesa Sharpe aliongeza: “Wanandoa wengi hivi sasa huchelewa sana kupata watoto na wengine mpaka wanafikia umri wa miaka 30, wakati huo umri wa uzazi kwa mwanamke unakuwa umepungua kiwango katika ufanisi.”
“Hii ni pamoja na kupungua kwa manii katika utengenezaji wa mtoto wa kiume na ni mara mojamoja sana huweza kubahatika kupata, hata hivyo, tatizo hili ni kubwa kwa wanandoa wengi.”
Utafiti huu uliwekwa hadharani wiki iliyopita na Jarida la ‘Medicine Journal for Human Reproduction.”
Ushauri kwa Watanzania
Dk Massawe katika maelezo yake alisema, wanaume wanaoishi maeneo ya joto hapa nchini hususan Dar es Salaam, wanapaswa kutumia nguo za ndani zilizotengenezwa kwa pamba halisi ili kutunza uwezo wa manii kiuzalishaji.
“Mbegu za kiume zinahifadhiwa nje tofauti na mwanamke. Hivyo nguo ya ndani anayoivaa inaweza kuhusika kuchangia kile kinachotajwa katika utafiti huo,” anasema Dk Massawe na kuongeza:
“Unapovaa mavazi yenye kubana au hata yasipobana na yakawa si pamba halisi ni mwanzo wa mbegu kupoteza sifa za kuzalisha.”
Alisema mfumo wa uzazi wa mwanamume huzitaka mbegu kuhifadhiwa sehemu yenye joto la wastani, hivyo matumizi ya nguo za nailoni kwenye mazingira ya joto, pia yanachangia ongezeko kubwa la ugumba kwa wanaume.
“Mpaka sasa tunapokea kesi nyingi kama hizo, idadi kubwa ya wanaume wanaokosa sifa za kuzalisha inazidi kuongezeka na ndiyo maana watu wanaotafuta watoto hivi sasa ni wengi,” alisema.
Hata hivyo, Dk Massawe alisema sababu za ugumba ni nyingi, lakini hiyo inaweza kuwa mojawapo.
Tafiti nyingine
Matokeo ya utafiti yaliyotolewa mwaka juzi yalionyesha kuwa wastani wa asiliamia 30 mpaka 35 ya wanaume wamekuwa wakifika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kati ya 2010-2011 kwa ajili ya vipimo vya ugumba. Hiyo ni kwa mujibu wa takwimu za Kitengo cha Masuala ya Uzazi na Magonjwa ya Wanawake cha hospitali hiyo.
Hali kadhalika, utafiti huo ulioitwa: “Utasa katika jamii na kliniki ya misingi ya sampuli ya wanandoa katika Wilaya ya Moshi,” uliofanywa na Dk G. Marseng, Januari 2006 kwa wanandoa 269, ulibaini kuwa asilimia 30 ya wanaume walikuwa wanakabiliwa na matatizo ya ugumba.
Utafiti mwingine ni ule uliofanywa na Dk Yahaya Kapona wa Muhimbili wakati alipokuwa katika Hospitali ya Tumaini, Upanga, Dar es Salaam mwaka 2003 ambao ulibainisha kuwa ni asilimia 24.9 tu ya wanaume wanaoishi Dar es Salaam wenye manii yenye uwezo wa uzalishaji kwa asilimia 100.
Dk Kapona alisema jana kuwa utafiti huo ni wa muda mrefu na hali inaweza kuwa imebadilika lakini akasisitiza kuwa katika utafiti wake huo unaoitwa: “Utasa kwa wanaume Dar es Salaam,” ulibaini kuwa hata wanaume wanaobahatika kuzalisha, mbegu zao si imara kwa asilimia 100

Comments

Popular posts from this blog