Mchakato wa kumrejesha Alex Massawe waiva
Mchakato wa kumrejesha nchini, mfanyabiashara maarufu Alex Massawe, aliyekamatwa Dubai, Falme za Kiarabu, umeanza rasmi baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kutoa hati ya kumkamata na kumrejesha nchini kujibu mashtaka. Hati hiyo ilitolewa juzi na Hakimu Mkazi Geni Dudu, kufuatia maombi ya Jamhuri, yaliyotolewa na Wakili Mwandamizi wa Serikali Tumaini Kweka, baada ya kumfungulia kesi ya jinai. Katika kesi hiyo namba 150 ya mwaka 2013, Massawe anakabiliwa na mashtaka ya kughushi na kuwasilisha hati za nyumba. Massawe ambaye alikamatwa hivi karibu na Shirika la Kimataifa la Polisi (Interpol), amekuwa akitafutwa akihusishwa na matukio ya uhalifu. Mahakama hiyo ilitoa usahihi wa majina yake, kuwa ni Alex Siryamala Massawe. Kwa mujibu wa Kweka, mtuhumiwa anayeshikiliwa katika nchi nyingine anapoombwa kurejeshwa nchini,lazima kuwe na kesi ambayo anatakiwa kujibu mashtaka, vinginevyo inaweza kuwa vig