Posts

MCL sasa kuwajaza wasomaji mamilioni, magari matatu;

Image
Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), imezindua promosheni kabambe ya 'Chomoka na Mwananchi' itakayowawezesha wasomaji wa gazeti la Mwananchi, kujishindia zawadi zenye thamani ya Sh250,000,000.Zawadi hizo ni pamoja na fedha taslimu na magari matatu mapya. Akizungumza katika uzinduzi huo jana, Mkurugenzi Mtendaji wa MCL, Tido Mhando, alisema promosheni hiyo itakayoanza leo, itafanyika nchini kote kwa siku 100 na kila siku kutakuwa na mshindi ambaye atajinyakulia Sh1,000,000. P.T "Hii ni promosheni ambayo lengo lake ni kuwashukuru wasomaji wetu kwa kuendelea kulipenda gazeti lao na kuliweka juu hapa nchini," alisema Mhando. Alisema hadi mwisho wa promosheni hiyo (Novemba 30, mwaka huu), wasomaji 100 watakuwa wamejinyakulia fedha taslimu Sh100,000,000 na wengine watatu watapata magari mapya. "Lengo letu ni kuwawezesha wasomaji siyo tu kupata habari na kufikiri tofauti, bali pia kuweza kuwajenga kimaisha," ali

Miss Tanzania 2012 aanza ujenzi wa bweni la Albino Shinyanga

Image
Brigette Alfred pamoja na baadhi ya wanafunzi walemavu wa ngozi wa shule ya msingi Buhangija wakinyanyua moja kati ya mabati 200 aliyonunua kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wavulana katika shule hiyo,CHANZO:Majuto Omary. Na Mwandishi wetu, Shinyanga MREMBO wa Tanzania, Brigitte Alfred ameonyesha mfano wa kuigwa nchini katika tasnia hiyo baada ya kuanza ujenzi wa bweni la wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi (albino) katika wilaya ya Shinyanga wanaoishi katika shule maalum ya Buhangija. Tayari mrembo ameweka jiwe la msingi na kupandisha ukuta sambamba na kukabidhi mabati 200 kwa ajili ya kujengea paa la bweni hilo la wavulana lenye uwezo wa kulaza wanafunzi 50. Makabidhiano hayo yalifanywa na mrembo huyo kwa katika hafla fupi iliyohudhuriwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Annarose Nyamubi, afisa elimu wa manispaa ya Shinyanga Honoratha Ruhumbika na walimu wa shule hiyo wakiongozwa na mwalimu mkuu, Peter Ajali. Briggite alisema kuwa ameamua ku

CLOUDS MEDIA GROUP YAANDAA SEMINA YA FURSA MKOANI TABORA LEO

Image
Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya, Diamond, akiwaimbisha washiriki wa semina ya Fursa waliojitokeza kwa wingi mapema leo kwenye ukumbi wa Student's Center uliopo katikati ya mji wa mkoa wa Tabora, kushoto kwake ni Bwa. Marco Vingila kutoka shirika la TPSF. Mghani mahiri wa mashairi hapa nchini Mrisho Mpoto akizungumza kwa msisitizo, masuala ya fursa mbalimbali zinazopatikana katika suala zima la ujasiliamali mapema leo kwenye semina ya Fursa iliyofanyika katika ukumbi wa Student's Center, uliopo katikati ya mji wa mkoa wa Tabora. Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group, imefadhiriwa na shirika la NSSF; Zantel, MaxMalipo, Lake Oil.  Baadhi ya Wasanii wa muziki wa kizazi kipya wakishiriki semina ya Fursa kwa vijana ililiyofanyika leo kwenye ukumbi wa Student's Center katikati ya mji wa mkoa wa Tabora mapema leo, kutoka kulia ni Msanii Godzilla, Baba Levo, Amin

EDWARD LOWASSA AMBANA BERNAD MEMBE KWENYE KIKAO CHA KAMATI YA BUNGE

Image
 Mhe. Edward Lowassa (Mb.)Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa  na Mbunge wa Monduli akizungumza wakati wa kikao na Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika kupitia Taarifa ya Utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi ya Wizara. Kikao hicho kilifanyika katika  Ofisi Ndogo za Bunge tarehe 19 Agosti, 2013.   Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, akiwasilisha  Taarifa ya Wizara ya Utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge (hawapo pichani).   Baadhi ya Waheshimiwa wa Wabunge ambao pia  ni Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani).  Kikao kikiendelea. Baadhi ya Wakurugenzi na Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakifuatilia kwa karibu taarifa iliyokuwa ikiwasilishwa na Mhe

IVANOVIC AEPUKA RUNGU LA FA BAADA YA KUMCHEZEA RAFU BENTEKE

Image
BEKI wa Chelsea, Branislav Ivanovic hatakutana na adhabu zaidi kwa rafu aliyomchezea Christian Benteke jana usiku katika mchezo wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Astin Villa. (HM) Kocha wa Aston Villa, Paul Lambert 'alimuwakia' refa Kevin Friend kwa kutomtoa beki huyo baada ya rafu hiyo mbaya, kiasi cha sekunde tu kabla hajaifungia wenyeji bao la ushindi Uwanja wa Stamford Bridge. Lakini kwa sababu, Friend alimuonyesha kadi ya njano beki huyo Mserbia baada ya kuona tukio alilomfanyia Benteke, Chama cha Soka (FA ) hakitachukua hatua zaidi. Lambert, ambaye baada ya mechi alilalamika timu yake kuonewa katika mechi hiyo, alisema: "Nafikiri Ivanovic alicheza rafu. Nafahamu ni mchezo wa maguvu. Lakini hicho ndicho nachofikiria,". Mourinho, pamoja na hayo, alipuuza madai hayo akisema: "Hii soka soka ya England. Kwa sababu fulani, dunia inaipenda hii kuliko ligi yoyote,". Sheria za FA zimebadilika majira ya

as cannes yamwagia sifa kapombe

Image
Shomari Kapombe akitambulishwa rasmi AS Cannes RASMI, klabu ya Daraja la Nne Ufaransa, AS Cannes imetangaza katika tovuti yake kwamba katika kujiimarisha ili kutoka katika kipindi kigumu, imeboresha kikosi chake kwa kumsajili kiungo Mtanzania, Shomari Salum Kapombe. (HM) Klabu hiyo imesema hiyo pia itakuwa fursa kwa mchezaji huyo kutoka Simba SC ya Tanzania kujipatia uzoefu wa kimataifa akiwa na Weupe hao Ufaransa. Imemuelezea Kapombe, kama kinda mwenye umri wa miaka 21, ambaye hadi sasa amekwishachezea mechi 14 timu yake ya taifa, Taifa Stars pamoja na kumkabidhi jezi kuanza rasmi mazoezi na wenzake. Na imevutiwa naye zaidi baada ya wasifu wake kusema anaweza kucheza nafasi nyingine pia, zikiwemo za ulinzi, hivyo atakuwa msaada mkubwa kwa kocha Jean-Marc Pilorget msimu huu. Imesema viongozi wanafanya jitihada kubwa kuhakikisha wanainua kiwa

NITATUMA OFA NYINGINE KWA UNITED KUMSAJILI ROONEY"MOURINHO"

Image
Jose Mourinho amethibitisha kwamba Chelsea kwa sasa watasitisha mbio zao za kumuwania mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney mpaka klabu hiyo itakapocheza na United kwenye dimba la Old Trafford siku ya jumatatu. (HM) The Blues wameshuhudia ofa zao mbili zikikataliwa na mabingwa wa premier league, huku kocha David Moyes akisisitiza kwamba mshambuliaji huyo wa England hauzwi. Jana jumatano zilitoka taarifa kwamba United wapo tayari kuzungumza na Chelsea katika dili la uhamisho wa Rooney lakini ikiwa tu litamhusisha Juan Mata - lakini Mourinho amesema hakuna mazungumzo yatakayofanyika mpaka baada ya mechi ya jumatatu. "Tulituma ofa kwa ajili [Rooney] huko nyuma na tutfanya hivyo tena baadae," kocha huyo wa kireno aliwaambia waandishi wa habari baada ya ushindi wa 2-1 dhidi Aston Villa. "Lakini sitaki Chelsea ifanye kitu chochote kabla ya mechi ya Jumatatu tutakapoenda Old Trafford."  Chanzo: Shaffihdaud

WATU MILIONI 2.9 KUCHUKULIWA ALAMA ZA VIDOLE, PICHA.

Image
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imeanza zoezi la uchukuaji alama za vidole, picha na saini za kielekroniki kwa waombaji wa Vitambulisho vya Taifa katika mkoa wa Dar es Salaam ambapo watu wapatao milioni 2,900,000 wanatarajiwa kupatiwa huduma hiyo. Zoezi hili lilianza Julai 15 katika wilaya ya Temeke ambayo imegawanywa katika kanda tano, itafuatiwa na Wilaya ya Ilala na kuhitimishwa na Kinondoni. Kila Wilaya imegawanywa katika kanda, ili kuhakikisha wananchi wanahudumiwa vizuri na kurahisisha zoezi kwa kuwapunguzia wananchi usumbufu wa kukaa muda mrefu kusubiri katika foleni. Zoezi la uchukuaji alama za vidole linakwenda sambamba na ujazaji fomu kwa waombaji wapya ambao hawakupa fursa ya kujaza fomu wakati wa zoezi la ujazaji fomu za maombi ya vitambulisho vya Taifa. Waombaji wanatakiwa kufika kwenye vituo vya usajili na nyaraka halisi za kuthibitisha uraia na umri mathalan, cheti cha kuzaliwa, pasipoti, v

WENGER AMGEUKIA FLAMINI, AMREJESHA EMIRATES

Image
Mathieu Flamini KOCHA Arsene Wenger yuko katika siku 12 ngumu za kukimbizana kukamilisha usajili kabla ya dirisha kufungwa na sasa amehamishia ndoana zake kwa Mathieu Flamini, kiasi cha miaka mitano tangu aondoke Arsenal kuhamia AC Milan. (HM) Klabu hiyo ya Italia imemtema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 mwishoni mwa msimu na sasa kiungo huyo kiasi cha wiki mbili amekuwa akifanya mazoezi na kikosi cha Wenger. Kocha wa Arsenal amevutiwa kiasi cha kutosha na hali ya mchezaji huyo na yuko tayari kumpa ya Mkataba Flamini baada ya kukubali kurejea nyumbani licha ya kutakiwa na klabu nyingine. Atakuwa mchezaji wa pili kusainiwa na Wenger majira haya ya joto— wote wachezaji huru — na mchezaji wa nne wa zamani wa timu hiyo kusainiwa tena na kocha huyo, baada ya awali kuwarejesha Sol Campbell, Jens Lehmann na Thierry Henry Emirates.

HUYU NDO MKENYA ANAYEDAIWA KUWA DEMU WA DIAMOND PLATINUMZ ATUPIA PICHA ZA UTATA.

Image
 Angel Maggie ni Mkenya ambaye wiki hii amepamba mitandao kadhaa ya nchini kenya akisemekana kuwa mpenzi wa mwanamuziki Diamond Platinumz ingawa Diamond mwenyewe bado hajaweka wazi kama ni kweli au lah! licha ya kwamba wanajuana muda sasa. Hata katika shows alizofanya Diamond hivi karibuni Nairobi na Mombasa alikuwa na Angel muda mwingi. Angalia picha zake mpya.......................

SHILOLE AAMBULIA MATUSI BAADA YA KUANIKA TUMBO LAKE MBELE ZA WATU......!!

Image
  Msanii wa filamu za Kibongo,na mwanamuziki wa Bongo Fleva Zuwena Mohamed‘Shilole’amenangwa kwenye mtandao wa instagram baada ya kupost picha akiwa na madansa wake huku wakiacha matumbo yao wazi.

BUNGE KUANZA VIKAO VYAKE JUMANNE DODOMA

Image
Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa tanzania linataraji kuanza vikao vyake kwa wiki mbili mjini Dodoma.Wabunge wamehitimisha vikao vya kamati za bunge leo ikiwa ni utekezaji wa shuguli mbalimbali za Bunge ikishiria kuanza kwa vikao vyake jumanne ijayo mjini Dodoma, Ambapo miswada mbalimbali itawasilishwa katika vikao hivyo  

WASTARA HATAOLEWA BONGO TENA

Image
Na Imelda Mtema KAKA wa staa wa Filamu za Kibongo, Wastara Juma aitwaye Juma Juma ameliambia Risasi Mchanganyiko kwamba dada yake hatafunga  tena ndoa nyingine hapa nchini. “Iwapo dada yangu akitaka kuolewa atafanya hivyo Uarabuni siyo hapa kabisa,” alisema kaka huyo na kudai kuwa ameshuhudia mateso mengi ya dada yake kwa wanaume wa Kitanzania. Kaka huyo amesisitiza kwamba wanaume wasipate tabu ya kumuuliza dada yake kuhusu suala la ndoa kwani watajisumbua bure. Juma alizungumza kwa niaba ya dada yake ambaye awali alipigiwa simu ili kuulizwa kama alikuwa na mpango wa kufunga ndoa nyingine hapa nchini. Hata hivyo, Wastara alimwachia kaka yake huyo kujibu badala yake, ingawaje kaka huyo hakufafanua kama dada yake ameshapata mtu wa kufunga naye ndoa huko Uarabuni. Wastara alifunga ndoa tatu na wanaume tofauti na mume wake wa mwisho alikuwa msanii wa filamu, Juma Juma Kilowoko ‘Sajuki’ aliyefariki dunia mapema mwaka huu.

MKENYA AKIRI KUUA MTU NA KULA MOYO NA UBONGO MAREKANI

Image
Alexander Kinyua (kushoto) na mwanamume aliyekuwa akiishi naye nyumba moja Kujoe Bonsafo Agyei-Kodie. Picha/MAKTABA Mwanafunzi kutoka Kenya aliyekuwa akiishi Marekani amekiri kwamba alimuua mwanamume waliyekuwa wakiishi nyumba moja na kula moyo wake na ubongo wake. MWANAFUNZI kutoka Kenya aliyekuwa akiishi Marekani amekiri kwamba alimuua mwanamume waliyekuwa wakiishi nyumba moja na kula moyo wake na ubongo wake. Alexander Kinyua, 22, alikiri mashtaka ya mauaji ya Kujoe Bonsafo Agyei-Kodie, 37, katika jimbo la Maryland mwaka jana lakini Jaji akasema hafai kulaumiwa aliposhtakiwa Jumatatu wiki hii. Jaji Stephen Waldron alisema Kinyua hawezi kulaumiwa kwani alikuwa anaugua akili na akaagiza awekwe kwenye hospitali ya watu wenye akili punguani. Kinyua, aliyekuwa mwanafunzi wa uhadhisi katika chuo cha Morgan State, aliambia maafisa kwamba alitumia kisu kuua mwenzake kabla ya kula viungo vyake. Agye

Tuhuma nzito : Magufuli, Mwakyembe, Lukuvi kufikishwa kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge

Image
Dar es Salaam.  Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imesema itawafikisha kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge, Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe akiwatuhumu kwa kulidanganya Bunge. Hatua hiyo ilitangazwa jana na Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe baada ya kumhoji Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Herbert Mrango kuhusu hati ya mashaka waliyoipata kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), mwaka wa fedha 2011/2012. Kamati hiyo ilieleza kuwa kwenye Bajeti ya mwaka huo kiasi cha Sh348,075,000,000 fedha za ndani zilizokuwa zimetengwa chini ya fungu lililotajwa kuwa ni la mradi maalumu (Special Road Construction Project) hazikutumiwa kwa malengo yaliyoelezwa bungeni. “Ni vizuri leo uiambie kamati fedha hizi ziliombwa kwa kitu gani na zilitumika kwa jambo gani. Tunajua kwamba fedha

Mungu aliniamuru nijiuzulu, asema Papa Benedict XVI

Image
Rome, Italia. Miezi sita baada ya kujiuzulu, Papa Benedict XVI, amefungua mdomo na kueleza sababu za kufikia uamuzi huo wa kushangaza. Jana, vyombo vya habari vilimkariri Papa Mstaafu Benedict akimweleza mgeni wake kuwa aliitwa na Mungu kwa miujiza. P.T Kiongozi huyo ambaye alishangaza watu kwa uamuzi huo wa Februari 8, mwaka huu, hata hivyo alisema sauti ya Mungu imejibu kupitia kwa mfuasi wake, Papa Francis. Papa Benedict alitangaza uamuzi wa kujiuzulu Februari 11, maelezo yake yalielekeza katika afya yake. Alisema nguvu zake zilikuwa zimepungua kiasi cha kutokuweza kumudu majukumu yake ipasavyo. Alisema, "Mungu aliniambia 'niondoke,' nami nikatimiza wajibu huo bila kusita," alisema Papa Benedict ambaye amekuwa kiongozi wa kwanza kufikia uamuzi huo baada ya miaka 600 ya Kanisa Katoliki. Alisema tangu wakati huo ameishi maisha ya sala. Mkongwe huyo mwenye umri wa mi