IVANOVIC AEPUKA RUNGU LA FA BAADA YA KUMCHEZEA RAFU BENTEKE
BEKI wa Chelsea, Branislav Ivanovic
hatakutana na adhabu zaidi kwa rafu aliyomchezea Christian Benteke jana
usiku katika mchezo wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Astin Villa. (HM)
Kocha wa Aston Villa, Paul Lambert
'alimuwakia' refa Kevin Friend kwa kutomtoa beki huyo baada ya rafu hiyo
mbaya, kiasi cha sekunde tu kabla hajaifungia wenyeji bao la ushindi
Uwanja wa Stamford Bridge.
Lakini kwa sababu, Friend alimuonyesha kadi ya njano beki huyo Mserbia baada ya kuona tukio alilomfanyia Benteke, Chama cha Soka (FA ) hakitachukua hatua zaidi.
Lambert, ambaye baada ya mechi alilalamika timu yake kuonewa katika mechi hiyo, alisema: "Nafikiri Ivanovic alicheza rafu.
Nafahamu ni mchezo wa maguvu. Lakini hicho ndicho nachofikiria,".
Mourinho, pamoja na hayo, alipuuza madai hayo akisema: "Hii soka soka ya England. Kwa sababu fulani, dunia inaipenda hii kuliko ligi yoyote,".
Sheria za FA zimebadilika majira ya joto kufuatai tukio kama hili lililomhusisha mchezaji wa Wigan, Callum McManaman aliyenusurika adhabu kwa kumchezea rafu mchezaji wa Newcastle, Massadio Haidara.
Pamoja na hayo, waliamua kwamba, FA inaweza kuchukua hatua, tu iwapo refa hakuona tukio vyema

Comments
Post a Comment